WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU
Mwananchi
 kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani 
Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa 
Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji 
hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini 
uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye 
thamani ya shilingi bilioni 25.7. 
Sehemu
 ya watoto kutoka katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa 
mkoani Simiyu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme 
uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili. 
Wananchi
 wa kata ya Shishiyu wakinyanyua mikono juu kama ishara ya kuridhishwa 
na utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA kabla ya 
kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo na Waziri wa Nishati na Madini Profesa 
Sospeter Muhongo. 
Waziri
 wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akihutubia wananchi wa 
kata ya Shishiyu (hawapo pichani) kabla ya kuzindua rasmi mradi wa 
umeme. 
Mtaalamu
 kutoka kampuni ya LTL (PVT) LTD Michael Marenye akitaja orodha ya 
vijiji vilivyonufaika na mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA 
Awamu ya Pili. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter 
Muhongo. 
Mbunge
 wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda akimpongeza Waziri wa Nishati na
 Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza
 umeme katika jimbo lake. 
Mbunge
 wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto) akitafsiri hotuba ya 
shukrani iliyotolewa kwa lugha ya kisukuma na mmoja wa wakazi wa kijiji 
cha Shishiyu mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter 
Muhongo kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo 
Waziri
 wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikata utepe 
kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA 
Awamu ya Pili. 
Waziri
 wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye tisheti ya 
kijani) akisoma maandishi kwenye jiwe la msingi mara baada kukata utepe 
kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo 
Waziri
 wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) Mbunge wa 
Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto mwa Waziri) na mmoja wa 
wakazi wa Shishiyu wakibonyeza kitufe kama ishara ya uzinduzi wa mradi 
huo. 
 
Waziri
 wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati aliyeshika 
mtoto); Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (wa pili kutoka 
kulia waliokaa mbele) na Diwani wa Kata ya Shishiyu wilayani Maswa Pili 
Kidesela (wa kwanza kulia waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja 
na baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara baada 
ya kumalizika rasmi kwa uzinduzi wa mradi huo. 
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment