TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 8, 2015

TAARIFA YA NYALANDU VYOMBO VYA HABARI

Waziri Nyalandu
SIKU ya Mkesha wa Mwaka Mpya, Desemba 31, 2014, nilikaribishwa kushiriki ibada ya Mkesha na Baba Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ephata, Josephat Mwingira, iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mkesha huo ulitangazwa moja kwa moja kwenye kituo cha luninga cha Star TV na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
Katika Mkesha huo, nilipewa fursa ya kuwasalimia waumini na kushirikiana nao katika neno la Mungu, ambapo huku nilieleza matumaini yangu kwa Taifa letu na ushiriki wa vijana katika uongozi wa nchi,kama yanenanvyo maandiko ‘vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataona ndoto’.Hata hivyo, jana nimesikitishwa sana na kuumizwa na habari ambazo hazina mashiko, za uzushi na za kutunga zenye lengo la kunipaka matope kwa kunihusisha na maneno ambayo kinywa changu hakikuyatamka wala kuyafanyia rejea. Nimeshangazwa sana.
Katika maisha yangu kama mtanzania,kiongozi na mkristo, kamwe sijawahi na sitarajii kutoa kauli hasi dhidi ya imani za dini nyingine, ikiwepo dini ya kiislamu. Nisisitize kuwa ninawapenda watu wa dini zote na makabila yote na kamwe sina ubaguzi kama inavyojaribu kuwekwa ili kunipaka matope katika jamii. Naamini taarifa hizo potofu zina malengo binafsi na watu wasionitakia mema.
Katika jimbo langu la Singida Kaskazini, nimeshiriki kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo makanisa na misikiti kwa uwazi kwa kuboresha miundombinu na kuziwezesha taasisi hizi kutoa mchango katika elimu.
Sio hivyo tu, kuonyesha ninachojaribu kuzungumzwa kuwa ni uongo na uzushi mtupu, katika Jimbo la Singida Kaskazini,nimepeleka masheikh wa vijijini mbalimbali kwa ajili ya kuhiji Mecca, mpango ambao ni endelevu kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Ni muhimu demokrasia ikaendelezwa kwa kuhimiza mijadala ya kuwaletea wananchi maendeleo na sio kwa kueneza chuki za kidini, kijinsia au kikabila.
Mungu ameliweka Taifa letu kuwa heri katikati ya mataifa na ni muhimu sote kudumisha amani na mshikamano badala ya kusingiziana uongo. Imeandikwa katika vitabu, usimsingizie jirani yako uongo’.
Imetolewa naLazaro Nyalandu,MNEC,CCM

No comments:

Post a Comment