TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 8, 2015

Rais Kikwete awaapisha wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

unnamed
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha wajumbe sita wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Walioapishwa leo ni pamoja na mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Bahame Tom Mukiria Nyanduga,Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Iddi Ramadhani Mapuri, na makamishna wa Tume hiyo Bwana Mohamed Khamis Hamad, Dkt. Kevin Mandopi, Bibi Rehema Msabila Ntimizi, na Bibi Salma Ali Hassan.
Pichani Rais Kikwete akiwa pamoja na wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora aliowaapisha leo Watatu Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Bahame Tom Mukiria Nyanduga, Watano Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Iddi Ramadhani Mapuri, na makamishna wa tume hiyo wakwanza kushoto ni Bibi Salma Ali Hassan, Wapili kushoto ni Bwana Mohamed Khamis Hamad, Wasita kushoto ni Dkt.Kevin Mandopi, na kulia ni Bibi Rehema Msabila Ntimizi(picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment