Viongozi mbalimbali wa TPDC wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka Kushoto ni Kamishna Msaidizi-GAS, Mhandisi
 Norbert Kashozya , Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, James Andilile, Mwenyekiti
 wa Bodi TPDC, Michael Mwande, Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO, Mhandisi 
Kapuulya Musomba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleleo ya Mafuta Gesi,
 Mhandisi, Joyce Kisamo.   
 Kaimu
 Mkurugenzi wa TPDC, James Andilile akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya 
TPDC kuongea na waandishi wa habari katika Mkutano wa Taarifa ya 
Utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya Gesi Asilia kutoka Madimba 
Mtwara , Songo Songo, Lindi,na Pwani hadi Dar es salaam.
 Mwenyekiti
 wa Bodi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael 
Mwande akielezea kwa kina juu ya Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa 
Miundombinu ya Gesi Asilia kutoka Madimba Mtwara , Songo Songo, Lindi,na Pwani hadi Dar es salaam.
Kaimu
 Meneja Mkuu wa GASCO Injinia Kapuulya Musomba akizungumzia juu ya 
utekelezaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya Gesi 
Asilia kutoka
Madimba Mtwara , Songo Songo, Lindi,na Pwani hadi Dar es salaam leo.
Madimba Mtwara , Songo Songo, Lindi,na Pwani hadi Dar es salaam leo.
Waandishi wa habari wakiwa katika Mkutano wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya Gesi Asilia kutoka
Madimba Mtwara , Songo Songo, Lindi,na Pwani hadi Dar es salaam.
Madimba Mtwara , Songo Songo, Lindi,na Pwani hadi Dar es salaam.
…………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
ZAIDI
 ya dola za Marekani sh.bilioni moja zimetumika katika kukamilisha mradi
 wa ujenzi wa bomba la gesi , kati ya fedha hizo, Benki ya Exim ya China
 imechangia asilimia 95 na Serikali ya Tanzania asilimia 5.
Aidha, mradi huo umekua kwa asilimia 94 ya mradi mzima, ambapo unatarajiwa kukabidhiwa Juni mwaka huu, ambapo unatarajiwa kuondoa tatizo la mgao wa umeme nchini.
Imeelezwa kuwa kwa sasa jumla ya megawati 300 za umeme kila siku zinazalishwa kwa kutumia gesi asilia.

Akizungumza
 katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Kaimu 
Meneja Mkuu wa Gas Supply Company Ltd (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba
 alisema kiasi hicho cha fedha kinatumika kugharamia mtambo wa kusafisha
 gesi asilia wa Songosongo na kuwa  umetumia dola bilioni 151, 735.
Musomba aliongeza kuwa mtambo wa kusafisha gesi asilia wa Mnazi Bay umetumia dola bilioni 197,877 na mradi wa bomba la kusafirishia gesi asilia umetumia dola bilioni 875,715.
Musomba aliongeza kuwa mtambo wa kusafisha gesi asilia wa Mnazi Bay umetumia dola bilioni 197,877 na mradi wa bomba la kusafirishia gesi asilia umetumia dola bilioni 875,715.
“Kila
 siku ni lazima tupate taarifa kuwa ni watu wangapi wameajiriwa, ambapo 
zaidi ya watu 1,000 huajiriwa kupitia mradi huu” alisema Musomba.
Musomba alitaja maeneo ambayo yanatumia gesi asilia kuwa ni viwanda 37, magari 60, nyumba za watu 70, hoteli 1 na taasisi 2 za Mgulani na Gereza la Keko.
Aliongeza kuwa milioni 70 zinahitajika kusambaza miundombinu ya gesi asilia kwa maeneo ya Mtwara na Lindi.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Michael Mwande alisema mradi huo si kwa ajili ya TPDC bali ni wa umma wa Tanzania.
Alisema mradi huo ulitarajiwa kukamilika Desemba mwaka jana, lakini kutokana na ujenzi wa gesi ya Songo Songo na makazi ya waendesha mitambo umesabaisha uchelewe.
Alisema mradi huo ulitarajiwa kukamilika Desemba mwaka jana, lakini kutokana na ujenzi wa gesi ya Songo Songo na makazi ya waendesha mitambo umesabaisha uchelewe.
Hata hivyo, aliwataka wananchi kuelewa kwa undani kuhusu mradi huo ili uweze kuleta manufaa kwa wananchi na nchi kwa ujumla.
Mwenyekiti huyo alitaja hatua zilizochukuliwa kwa ajili ya usalama wa wananchi wanaoishi maeneo ambayo bomba limepita kuwa ni pamoja na kuangalia namna watakavyochimbia chini bomba hilo ili lisilete athari kwa wananchi wa eneo hilo.

Nyingine
 ni kuweka helikopta zitakazokuwa zinazunguka eneo la bomba ili 
kuangalia vitu vitakavyokuwa vinafanywa na wananchi katika eneo hilo 
sanjari na vibao vyenye namba za simu. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment