TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 3, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KAMBI YA VIJANA WAJASILIAMALI YA MKOA WA PWANI KIJIJI CHA MSOGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHBRA), Dkt.Simon Kintingu, kuhusu utengenezaji rahisi wa mabati ya Vigae, wakati Makamu alipofika kuzindua Kambi ya Vijana 400 Wajasiliamali walioanza kambi hiyo leo kwa lengo la kujifunza utengenezaji wa vigae na ujenzi wa nyumba za bei nafuu, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo Februari 03,2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifyatua tofali ikiwa ni ishara ya kuzindua raasmi mashine hizo za kufyatulia matofali ya bei nafuu na uzinduzi wa kambi ya Vijana 400 Wajasiliamali, wakati alipofika kuzindua kambi hiyo iliyopo Kijiji cha Msoga Mkoa wa Pwani, leo Januari 03, 2012 akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Pwani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo ya jinsi ya uandaaji wa tofali la bei nafuu kutoka kwa Fundi Sanifu Ujenzi, Husein Mataka,wakati alipofika kuzindua kambi ya Vijana 400 wajasiliamali iliyopo Kijiji cha Msoga Mkoa wa Pwani, leo Januari 03, 2012 akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Pwani. 

Watoto wanaotoka katika mazingira hatarishi, na yatima wapewa msaada wa milioni 9 na laki sita

Na Gladness Mushi. - Arusha
Mfuko Wa maendeleo ya jamii Manispaa ya Arusha umefanikiwa kutoa msaada kwa mayatima 183 pamoja na wale ambao wanatokea mazingira hatarishi ambao unagarimu million tisa na laki sita kwa kuwapa mahitaji muimu ya shule .ikiwemo suala zima la ada
Akiongea na vyombo vya habari mapema wiki hii mratibu wa mfuko huo Bw Ernest Mkonyi alisema kuwa mfuko huo ulifikia hatua hiyo mara baada ya kuona kuwa watoto hao ambao wengi wao ni mayatima wana umuhimu wa kupata elimu zazidi.
Bw Mkonyi alisema ,kuwa suala la elimu kwa watoto hao ambao ni mayatima ni muhimu sana kwa kuwa wengi wao wanakosa haki zao za msingi za kupata elimu kwa ,kile kinachosababiswa NA MAPUNGUFU mbalimbali ndani ya jam;ii zao
Aliendelea ,kwa kusema kuwa ;hapo awali watoto hao walikuwa hawapati haki zao za msingi kwa kuwa ndani ya jamii zao hawakuweza kuwahudumia mahitaji yao ya muhimu kama vile ada kwa kuwa na hali ngumu ya maishahivyo kushindwa kumudu
“Unajua hawa watoto hawakuweza kwenda shule kwa wakati lakini sisi kama wadau wa sekta ya elimu tunamefanikiwa kuendelea kuwasaidia watoto hawa mahitaji mbalimbali kama vile ada, sare za shule na kwa sasa wanaedelea vema na masomo “alisema Bw. Mkonyi
Pia alisema kuwa watoto hao ambao kati yao ni mayatima na waliotoka katika mazingira magumu wametokea katika kata tatu ndani ya manispaa ya Arusha na kujumuisha kata za Elerai,Ungalmtd, na Sokoni one mjini hapa.
Aidha akielezea mpango makkati wa mfuko huo wa Maendeleo ya ,jamii ni kuhakikisha kiuwa wanchangia sekta ya elimu kwa ,kiwango kikubwa zaidi, huku wakiwakutanisha wazazi na walezi ambao wanajtokea mazingira ya chini kwa kuwapa mbinu za kubuni miradi iliu kujikwamua .kimaisha zaidi.
Alisema kuwa kupitia mpango huo wa kuwakutanisha utaweza kuwasidia wakazi hao na hivyo wao wenyewe kuweza kuinua na kuchangia sekta ya elimu hata kwa ,kuwasomesha watoto ambao wanatokea katika mazingira hatarishi na wengine wakiwa mayatima
Alitoa mwito kwa watanzania wote kuhakikisha kuwa jamii inatambua uwepo wa watoto yatima na wanaotokea katika mazingira hatarishi, kwa kuwapa mahitaji yao muhimu ili kuweza .kufanikisha katika kuinua kiwango cha jamii hapa nchini

Aliyekuwa Refa wa Kimataifa Gratian Matovu amefariki Dunia leo


Aliyekuwa Refa wa Kimataifa hapa nchini, Gratian Hemans Matovu (pichani), amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam. Kwa kujibu wa taarifa zilizoifikia Globu ya Jamii, kutoka kwa mtoto wake Bw. Stephen Matovu, Mzee Matovu amefariki leo majira ya saa 6 mchana huko nyumbani kwa kwake Mbezi Beach (Makonde) na taratibu za mazishi zinaendelea hapo hapo nyumbani kwake. Mzee Gratian Matovu alianza kuwa refarii wa kimataifa tokea miaka ya 1964 na aliendelea na shughuli hiyo hadi miaka ya 1970 na hadi Mwaka 2006 alikuwa bado katika Kamati ya Marefarii Tanzania. HISTORIA FUPI Mzee Matovu alipata Diploma ya Urefarii kunako miaka ya 1956 na akaja kuwa refarii Daraja la Kwanza mnamo Mwaka 1961. Miaka Mitatu baadae alipata Beji ya FIFA. Mzee Matovu alipata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Chama cha Marefarii Tanzania. Kwa Taaria zaidi za wasiliana na STEPHEN MATOVU 0713576666 Mungu Amlaze Mahala Pema Peponi Amina

Rais Jakaya Kikwete katika siku ya Sheria

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana katika viwanja vya Mahakama kuu jijini Dar es salaam leo January 3, 2012 na kupokewa na Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othman nyuma yake, Spika Anne Makinda (anayepeana nae mikono, na viongozi wa juu wa Mahakama kabla ya kuhutubia katika Siku ya Sheria Tanzania jijini Dar es salaam leo January 3, 2012
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiuhtubia katika Siku ya Sheria Tanzania jijini Dar es salaam leo January 3, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kalenda aliyozawadiwa na Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othman baada ya kuhutubia katika Siku ya Sheria Tanzania jijini Dar es salaam leo January 3, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mapendekezo ya Baraza la Taifa la NGOs Ikulu jijini Dar es salaam leo January 3, 2012 kuzungumzia mchakato wa Katiba (PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na viongozi wa Baraza la Taifa la NGOs Ikulu jijini Dar es salaam leo January 3, 2012 kuzungumzia mchakato wa Katiba

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Zamani wa Kibaha Mjini, Zainab Gama kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 3,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIWANDA CHA MAGODOLO CHA PAN AFRICA CHATEKETEA KWA MOTO

Kamanda Misime wa kanda ya kipolisi Wilaya ya Temeke akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kusimamia zoezi la kuzima moto katika kiwanda cha magodolo cha Pan African kilichopo Chang'ombe jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kimeteketea kabisa kwa moto uliolipuka kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mashine za kunolea visu vya kukata magodolo kiwandani hapo, Kamanda Misime amesema hakuna taarifa ya mtu yeyote kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo la moto
Askari wa vikosi vya kuzima moto wakiwa kazini wakati walipokuwa wakizima moto kiwandani hapo
Magari ya vikosi vya kuzima moto yakiwa yamejipanga katika kiwanda hicho yakiendelea na kazi ya kuzima moto.
Hiki ndiyo kiwanda chenyewe kama kinavyoonekana kikiwa kimeteketea kabisa.
Askari wa kikosi cha kuzima moto wakizima moto huo.
Hawani baadhi raia wa kigeni ambao ni wafanyakzi wa viwanda vya jirani na kiwanda hicho.
Watu mbalimbali wakiangalia tukio hilo

Na Mwandishi Wetu Abdalah Mohamed 'Prins Naseem KUTETEA UBINGWA WAKE NA Salehe Mkalekwa .Februari 24 BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prins Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa. Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam. Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuwainua mabondia chipkizi ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo. "Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya. Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Salehe watakaopigana uzito wa kg 55, Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Seleman Shaaban na Abdalah Yusuph atakayepigana na Omari Kijepa. Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’. “Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

SIMBA, OLJORO JKT ZAINGIZA MIL 40

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT lililochezwa Februari Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 40,191,000.
Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 105 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A walikuwa 11,860.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 7,023,171, uwanja sh. 2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 936,423, TFF sh. 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 234,106.
Nayo mechi namba 104 kati ya African Lyon na Polisi Dodoma iliyochezwa Februari Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 45,000 kutokana na watazamaji 15 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 6,864.41 kila timu ilipata sh. 2,591, Uwanja sh. 514, TFF sh. 514, DRFA sh. 205, FDF sh. 257 na BMT sh. 51.

RAUNDI YA 16 LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA KESHO

Mzunguko wa 16 wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Februari 4 mwaka huu) kwa mechi tatu. Coastal Union itakuwa mgeni wa Moro United kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Nayo Villa Squad itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Ruvu Shooting na Polisi Dodoma zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Viingilio kwa mechi ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 15,000 kwa VIP A wakati Uwanja wa Chamazi ni sh. 10,000 kwa Jukwaa Kuu na sh. 3,000 mzunguko. Kwa mechi ya Mlandizi kiingilio ni sh. 2,000 kwa mzunguko wakati Jukwaa Kuu itakuwa sh. 5,000.
Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya muda wa kuanza mechi za ligi hiyo kwa kituo cha Dar es Salaam. Mechi zinazochezwa wikiendi kwenye Uwanja wa Taifa zitaaza saa 10 kamili jioni wakati zile zinazochezwa siku za kazi zitaanza saa 10.30 jioni. Mechi zote za Uwanja wa Azam- Chamazi zitaanza saa 10 kamili jioni.

MAWAKALA WA WACHEZAJI HAPA NCHINI KUFANYA MITIHANI MACHI 29,2012

Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Machi 29 mwaka huu saa 10 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.
Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga. Muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.
Mtihani uliopita ulifanyika Septemba 29 mwaka jana ambapo watahiniwa wanane walijitokeza na kufanya mtihano huo.
Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

NAPE AUKABIDHI TANI ZA SARUJI MKOA WA MARA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARASA


NA: BASHIR NKOROMO, MUSOMA 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeukabidhi mkoa wa Mara tani za saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mkoani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM.
Saruji hiyo itatumika kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi ambao wameshindwa kuanza kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa licha ya kufaulu mwaka huu. Akikabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa mkoa huo, John Tupa, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema saruji hiyo imetolewa na makada wa CCM ambao wameamua kutoa mchango huo kwa kupitia CCM ikiwa ni kuunga mkono maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM. Nape alisema makada hao ni Zulfikar Nanji wa Kampuni ya Mwanza Huduma Ltd (mifuko 400) Joseph 'Msukuma' Kasheku mfanyabiashara ambaye pia Diwani wa Kata ya Nzela, Geita na Mjumbe wa NEC, Vedastus Mathayo ambao wote wametoa mifuko 100 kila mmoja. Alisema kada mwingine ni Dk. Isack Chacha Ng'ariba ambaye aliahidi kutoa tani 200 za saruji ahadi ambayo aliitoa papo hapo wakati wa makabidhiano hayo. Nape aliwashukuru wafanyabiashara makada hao wa CCM kwa kuiunga mkono CCM katika kuhakikisha kwamba sherehe za miaka 35 ya CCM inakuwa na mafanikio makubwa kwa kutekeleza azma ya kuchangia shughuli za maendeleo. Alisema, wafanyabiashara na makada hao wanaichangia CCM pia kama kuonyesha shukurani yao kwa kuweza kufanya biashara zao kwa miaka mingi katika mazingira ya amani na utulivu chini ya uongozi wa serikali ya CCM. "Mkiona vinaelea vimeundwa, amani na utulivu huu uliopo ni mazingira yaliyojngwa na kuendelea kutunzwa na CCM tangu ilipoanza kutawala nchi hii baada ya kurithi uongozi kutoka vyama vya TANU NA ASP miaka 35 iliyopita", alisema Nape. Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa alisema, jumla ya watoto 6486 kati ya asilimia 50.3 ya watoto waliofaulu, wameshindwa kuanza kidato cha kwanza mkoani mwake kutokana uhaba wa vyumba vya madarasa licha ya kufaulu. Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa unahitaji madarasa 718 wakati yaliyopo ni 479 na hiyo kuwa na upungufu wa madawati 239 na kwamba wilaya ya Bunda ndiyo inayoongoza kuwa upungufu wa madarasa. Alisema licha ya kupata msaada huo wa saruji bado mkoa unahitaji mabati, mbao na madawati kwa ajili ya madarasa yatakayojengwa.

KARUME, MSEKWA, WAZINDUA KAMPEIN UZINI ZANZIBAR

Vijana wa umoja wa waendeshaji mapikipiki wa chama cha Mapinduzi wakimsindikiza mgombea wa Uwakilishi wa chama hicho junbo la Uzini Mohamed Raza katika uzinduzi wa kampeni wa kuwania kiti cha Uwakilishi Jimbo hilo hapo juzi
Kijana wa chipukizi Zawadi Mbaraka akimvisha Skafu Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Karume baada ya kuingia katika Uwanja wa Mkutano wa CCM kwa ajili ya kuzindua kampeni ya chama hucho huko Uzini wilaya ya kati Unguja.
Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akibadilishana mawazo na Makamo Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa huko katika kiwanja cha mpira Uzini wakati wa kuzinduakampeni ya kugombea Uwakilishi wa jimbo hilo.
Wananchi mbalimbali pamoja na wakereketwa wa chama cha CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika huko katika kiwanja cha Uzini Zanzibar kwa ajili ya kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo hilo ndugu Mohd Raza.
Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akimnadi mgombea wa Kiti cha Uwakilishi jimbo la Uzini ndugu Mohd Raza Huko katika kiwanja cha Mpira Uzini.
Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akihutubia wananchi pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi baada ya kutambulishwa rasmi kwa wanachama hao hapo jana Kuliani kwake ni Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

Rais azungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi na watendaji wa Wizara ya nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana,katika utekelezaji wa kazi za Wizra hiyo.(Picha na Ramadhan Othman Ikulu.) 02/02/2012
Watendaji wa Wizara ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu,wakiwa katika kikao cha siku moja cha utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo, chini ya Mwenyekti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, jana Ikulu Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman IKulu)

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalum, kuhusu ufugaji wa Kuku wa mayai, wakati alipotembelea na kuweka Jiwe la msingi katika kituo cha Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, leo Januari 02, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mabanda ya kufugia kuku katika kituo hicho cha Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani, leo Januari 02, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la mradi wa Ujenzi wa Kituo cha mnada wa Ng’ombe katika Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo, Januari 02, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa Kituo cha mnada wa Ng’ombe katika Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani, leo Januari 02, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha mnada wa Ng’ombe katika Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani, leo januari 02, 2012.

A round of applause rings after President Jakaya Mrisho Kikwete has officially launched the First National Bank Tanzania (FNB-Tanzania) yesterday at the Kilimanjaro Grand Hyatt hotel in Dar es salaam. Others from left are the High Commissioner of South Africa to Tanzania, Mr Thanduyise Henry Chiliza, the CEO of FirstRand, Mr Sizwe Nxasana and the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Ms Elizabeth Nyambibo. (Photo by State House)
President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech during the official launch of the First National Bank Tanzania (FNB-Tanzania) yesterday at the Kilimanjaro Grand Hyatt hotel in Dar es salaam today February 2, 2012.

NA: ASHURA MOHAMED-ARUSHA
Katika harakati za kuhakikisha kuwa kunakuwepo na taarifa sahihi pamoja na takwimu juu ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa tafiti na utunzaji wa kumbukumbu serikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto imewakutanisha wadau mbalimbali katika warsha kuhusu uanzishwaji wa kituo cha kitaifa cha utafiti na kumbukumbu za wanawake katika eneo la tengeru wilaya ya arumeru mkoani Arusha.
Akifungua warsha hiyo naibu katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Anna .T.Maembe amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho kutaiwezesha serikali kuwa na takwimu za kitaifa juu ya unyanyasaji wa kijinsia hivyo itarahisisha utatuzi wa changamoto hizo kwa kuwa watakuwa bna takwimu sahihi.
Anna amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa vituo vya kitaifa ni kushirikiana na kituo cha kanda katika kufanya tafiti mbalimbali,kuimarisha mahusiano,kubadilisha uzoefu ,kutunza kumbukumbu na kupashana habai zinazohusu haki za wanawake na usawa wa kijinsia.
Aidha amesema kuwa vituo hivi vitahamasisha wadau mbalimbali kuhusu usawa wa kijinsia,ulinzi na kuheshimu haki za wanawake lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili waweze kufanya tafiti wa masuala ya yanayohusiana na usawa wa kijinsia na kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki kikamilifu na wanachangia kuleta maendeleo endelevu katika nchi wananchama hasa ziliathirika na vita.
Pia amefafanua kuwamadhumuni ya warsha hiyo ni kuwapatia taarifa juu ya uwepo wa kituo cha kanda kilichopo katika chuo cha ustawi wa jamii Tengeru kuwa ndicho kilichochaguliwa hapa nchini,kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kakufanikisha shughuli zitazofanywa nakituo cha utafitina kumbukumbu za wanawake.
Naye mwakilishi kutoka shirika la UNESCO Modester Munira amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kutunza nyaraka tume ya taifa unesco iliona ni vyema kikaanzishwa kwa kituo hicho kwa kushirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto hivyo amatakataarifa zitolewe kwa uwazi zaidi.

Na Lydia Churi, MAELEZO, Dodoma
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali inakubali kuwa wastaafu kupewa mkataba wa kuendelea kufanya kazi si sahihi na kuahidi kuwa suala hilo litafanyiwa kazi.
Akifanya majumuisho wakati wa mjadala wa Azimio la kuridhia mkataba wa vijana wa Afrika (The African Youth Charter) waziri Nchimbi alisema hatua ya wastaafu kupewa mikataba ya kuendelea na kazi inawanyima vijana haki ya kupata ajira katika taasisi mbalimbali.
Akizungumzia suala la maadili kwa vijana Mheshimiwa Nchimbi alisema hivi sasa vijana wakiwemo baadhi ya viongozi wanaotoa michango yao juu ya mambo mbalimbali katika mitandao kama vile facebook na twitter wanatumia lugha zisizojenga na badala yake aliwataka kutoa michango isiyokuwa na madhara kwa vijana wa taifa hili hasa ile inayotumia lugha zinazojenga ili kulinda maadili ya Mtanzania.
Aliwataka viongozi kuwa wa kwanza kupiga vita matumizi mabaya ya mitandao na kuacha tabia za kulipiza visasi pale wanapokosana na wenzao kwani hizo si sifa za kiongozi bora. “kiongozi bora na imara ni yule mwenye tabia ya kusamehe, alisema”.
Kuhusu mchakato wa kutafuta vazi la taifa waziri huyo alisema wizara yake inatekeleza maagizo yaliyotolewa na bunge na kuwaomba wabunge kuwa wa kwanza kuunga mkono wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapotekeleza maagizo hayo. Aliongeza kuwa kamati iliyoteuliwa kutafuta vazi la taifa ni makini kwa kuwa imeundwa na watu makini waliotoka kwenye kada mbalimbali.
Awali akichangia mjadala huo, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM) Peter Serukamba alisema suala la wastaafu kupewa mkataba wa kuendelea na kazi halifai kwa kuwa linawanyima vijana haki yao ya kupata ajira. Alitoa mfano kuwa hivi sasa wenyeviti wa bodi wengi ni wastaafu ambapo ilipaswa nafasi hizo kuchukuliwa na vijana.
Alisema suala la uzoefu kuwa miongoni mwa sifa za kupata ajira si haki kwa kuwa linawanyima vijana nafasi ya kupata ajira hizo. Alisema vijana wawapo vyuoni hupatiwa muda wa kufanya mazoezi ya kazi na hivyo kuwa na uzoefu wa kutosha.
Bunge limeridhia mkataba wa kimataifa wa vijana isipokuwa limeridhia kwa stara ibara mbili zinazohusu sera ya taifa ya vijana na suala la vijana wa kike wanaopata ujauzito au kuolewa kabla ya kumaliza elimu zao kupewa fursa ya kuendelea na masomo.
Bunge limeridhia kwa stara ibara hizo kwa kuwa Sera ya Taifa ya Vijana kwa taratibu za nchi yetu hupitishwa na baraza la mawaziri na sheria hutungwa na bunge wakati mkataba unasema Sera itapitishwa na kukubaliwa na bunge na kufanywa sheria.
Kwa upande wa elimu kwa vijana wa kike waliopata ujauzito masomoni, mkataba unataka wasichana wa kike wanaopata ujauzito masomoni kuepwa firsa ya kuendelea na masomo wakati sheria za nchi yetu bado haziruhusu vijana wa kike waliopata ujauzito masomoni kuendelea na masomo.

Wednesday, February 1, 2012

MALIASILI KUSHIRIKIANA NA IDARA NYINGINE ZA SERIKALI KUKOMESHA USAFIRISHAJI HARAMU WA MALIASILI

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi- Zanzibar . Idara ya Wanyamapori nchini kwa kushirikiana na Idara nyingine za Serikali vikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa pamoja vimekubaliana kudhibiti usafirishaji haramu wa nyara za Serikali na mazao ya Maliasili vikiwemo viumbe hai na miti ya uwoto wa asli. Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibat Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa hayo yamesemwa leo mjini Zanzibar na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi. Maimuna Tarishi, wakati akifungua mkutano wa siku mbili kwa Maafisa wa Idara 16 za Serikali kutoka Tanazania Bara na Viisiwani. Bi.Tarishi amesema kuwa Serikali imeazimia kuviunganisha vyombo mbalimbali kama wadau katika kudhibiti vitendo vya uhalibifu na matumizi mabaya ya maliasili zetu ili ziendelee kuwa urithi wa vizazi vya sasa na vijavyo. Amesema changamoto zilizopo hivi sasa ni kuwa kumejitokeza makundi ya watu wachache ambao kwa uchu wao wa kutaka utajiri wa haraka haraka wamekuwa wakishirikiana na magenge ya watu wengine kuzihujumu maliasili zetu. Katibu Mkuu huyo amesema wakati sasa umefika wa kuvishirikisha vyombo vyetu kuhakikisha kwamba kwa pamoja vinalinda maliasli hizo kwani maliasili ni suala mtambuka na linamgusa kila mmoja wetu. Amewataka washiriki wa semina hiyo kuweka mikakati itakayoweza kusaidia kuimarisha ushirikiano kwa vyombo hivyo ili kwa pamoja vishiriki katika kulinda maliasili za nchi yetu zisitoroshwe kwenda nje ya nchi kwa manufaa ya watu wachache. Awali Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasi na Utalii Bw. Paul Sarakikya, amesema kuwa idara yake imeanza kufanya utafiti wa kujua maeneo yenye bandari bubu zinazotumika katika kusafirishia maliasili baharini. Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkataba wa Lusaka wa kuhifadhi wa Wanyamapori na mimea Bw. Timothy Rwegasira, amesema kuwa hali ya ujangili na usafirishaji kwa magendo nyara za serikali ni mkubwa. Amesema Majangili wamekuwa wakishirikiana katika kufanikisha uhalifu huo, hivyo ipo haja pia kwa vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kushirikiana kwa karibu na maafisa wa maliasili katika kukomesha vitendo vya kijangili vinavyofanywa na magenge hayo ya kihalifu. Naye Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar SP Omari Amiri Omari, amesema kuwa ipo haja ya Washiriki wa Semina hiyo wakaweka sawa masuala ya kisheria kwa mfano Zanzibar haina Tembo lakini Meno ya Tembo yanapitia Zanzibar. SP Omari amesema kutokana na hali hiyo kuna haja ya kutajuta mlingano wa pamoja wa kisheria itakayosaidia katika kudhibiti usafirishaji haramu wa nyara za Serikali yakiwemo meno ya Tembo. Semina hiyo inawashirikisha Maafisa kutoka idara mbalimbali za Serikali Kuu na SMZ wakiwemo Maafisa wa maliasili, Jeshi la Polisi, Mahakimu, Waendesha Mashitaka na TAKUKURU. Wengine ni Usalama wa Taifa, KMKM, Shirika la Polisi wa Kimataifa Interpol, Bandari, Shirika la Meli Zanzibar, Viwanja vya Ndege na Kitengo cha Kuzuia Madawa ya Kulevya hapa nchini.

Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu. Damian Lubuva (watatu kushoto) , makamu Mwenyekiti wa Tume, Mh. Hamid M Hamid na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Julius Mallaba. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Februari 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAPE AKAGUA KAMBI YA VIJANA WANAOJIANDAA NA SHEREHE ZA MIAKA 35 YA CCM MWANZA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia vijana waliopiga kambi kujiandaa wa kwaride maalum la sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, alipotembelea vijana hao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, leo. Maadhimisho hayo yanafanyika Jumapili hii, Februari 5, 2012 Kitaifa mjini Mwanza.
Nape akiwashangilia Vijana hao baada ya kuimba wimbo wa Mapinduzi.Kulia ni Katibu mpya wa Umoja wa Viojana wa CCM mkoa wa Mwanza Julius Mpanda na watatu kulia ni Katibu wa zamani wa vijana wa mkoa huo, Josephat Ndulango.
Baadhi ya vijana wakiwa na nyuso za kikakamavu walipompokea Nape
Nape akila chakula kwenye kambi hiyo ya Vijana

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NA POSHO ZA WABUNGE

Kwa upande mwingine Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa juu ya swala la posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na mchakato wa swala hili kuliangalia upya na kutumia busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa. CCM inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya kuwawakilisha bungeni. CCM inaendelea kuwasihi waheshimiwa wabunge walitafakari upya swala hili na busara itumike katika kuliamua huku wakifungua masikio kusikiliza sauti za Watanzania kwani huko bungeni wana wawakilisha hawa Watanzania, ni vizuri kusikiliza hiki kilio chao! Si busara kupuuza kilio cha waliokupa dhamana ya kuwawakilisha. Msimamo wa Rais Kikwete kama sehemu moja ya mamlaka inayohusika na mchakato huo ni uthibitisho wa usikivu wake kwa wananchi anaowaoongoza, yeye katimiza wajibu wake, tunawasihi waheshimiwa wabunge wetu nao walitafakari hili na kuona busara ya kuachana nalo kwasasa.

Kwa muda sasa nchi yetu imepitia kwenye tatizo kubwa la mgomo wa madaktari katika hospitali nyingi hasa za umma ambao kwa kiasi kikubwa mgomo huo umekuwa na madhara makubwa kwa watanzania masikini ambao ni wengi, kiasi cha kugharimu hata maisha yao. Chama Cha Mapinduzi kinachukua nafasi hii kuwapa pole sana wale wote walioathiriwa kwa namna moja ama nyingine na mgomo huu. Na kwakweli tunasikitishwa sana na hali inayoendelea! Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza na kuwashukuru madakitari walioonyesha ubinadamu na uzalendo kwa kuamua kurudi kazini na ambao hawakugoma kabisa. Tunawashukuru na kuwapongeza kwani hakuna masilahi yanayovuka thamani ya uhai wa binadamu mwenzako! Tunachukua fursa hii pia kuwashukuru sana na kuwapongeza askari wetu wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kizalendo wa kuamua kuitikia wito wa serikali kwenda kwenye baadhi ya hospitali kusadia kuwatibu watanzania wenzao. Moyo huu ni wa kizalendo na wa mfano. Tunajivunia uzalendo wa jeshi letu! Tunachukua nafasi hii kuwaomba madaktari wanaoendelea na mgomo kurudi kazini huku wakiendelea na mazungumzo na serikali. Tunaamini madai yao yanawezekana kushughulikiwa ikiwa pande zote mbili zitaamua kukaa chini kwa dhati na kuzungumza. Serikali kwa upande mmoja watafute kwa makini chanzo cha mgogoro huu na kutafuta majibu, na madakitari nao kwa upande wa pili, wawe tayari kukaa mezani na kuzungumza. Tunasisitiza thamani ya maisha ya binadamu ni kubwa kuliko masilahi na madai wanayoyaomba! Serikali ni vizuri ikajenga utamaduni wa kushughulikia matatizo haya ambayo yanaathiri wananchi wengi kwa uharaka na udharura unaostahili badala ya kusubiri hali inapokuwa mbaya zaidi.

ACP Kashai akikagua kikosi cha kutuliza ghasia na mafunzo aliyo toa kukabiriana na majanga
ACP Kashai akikagua kikosi cha kupambana na majambazi kwa kutumia piki piki
Na Pardon Mbwate Mwandishi wa Jeshi la Polisi- kigoma
Askari wa mapokezi katika vituo vya Polisi hapa nchini, wametakiwa kuwa kioo cha Jeshi hilo kwa kuonyesha ukarimu na kauri nzuri wanapowahudumia wananchi wanaofika kwenye vituo hivyo ama wanapoombwa msaada mahala popote wanapoombwa kufanya hivyo.
ACP Frasser Kashai amesema hatua hiyo italiwezesha Jeshi hilo kuendelea kujenga heshma mbele ya Jamii wanayoihudumia na taifa kwa ujumla.
Akizungukia na Askari polisi, wakuu wa idala mbali mbali za polisi posti, Kamanda Kashai amesema dhamira ya Jeshi hilo ni kutaka kila askari kubadilika na kutoa huduma bora kwa wananchi. na kuwa makini katika utendaji wao wa kazi za kila siku kutoa huduma kwa mteja iliyo bora
Kamanda Kashai amesema hayo akiwa anakagua paledi ukaguzi huo uliofanyika na maafisa wake Kihenya Kihenya SSP na RCO Josephu Konyo SSP OCD Wilaya kigoma Jafeti Kibona D/SSGT Silvanusi Mazengo D/SSGT Deusidedith Magogo D/SGT Menas Temba ukaguzi huo uliowahusisha askari wa vikosi vyote pia ukaguzi huo ni pamoja na kesi wanazo peleleza na kutaka kujua wapi zimefikia na kuona hatua walizo chukua mazingila utabadili mwelekeo wa kiutendaji wakimazoea bali kuboresha huduma kwa jamii.kumarisha wawapo vituoni mwao na kuwafanya wananchi kuona kuwa vituo vya Polsi ni kimbilio la watafuta haki.
Amesema Kamanda Kashai jukumu la kuwafundisha askari ni la kila Afisa wa polisi, il askari wawe waadifu katika utendaji kazi wao na kuwaudumia wananchi wanapokwenda katika kituo cha Polisi anatarajiwa kupata huduma anayoitegemea na kwamba kama atakuwa na tatizo anaamini atapata mapokezi mazuri na kutatuliwa tatizo lake.
Kamanda Kashai amesema kutokana na mabadiliko ya mifumo ya Majeshi ya Polisi Duniani Kote, Polisi anatakiwa kumuona Raia kama sehemu ya Polisi kwani ni Raia huyo huyo atalazimika kutoa taarifa za wahalifu Polisi na hivyo kurahisisha utendaji wa Jeshi zima.sambamba na hilo ataendelea kufundisha askari kila juma tano ili kuwa na askari wazuri katika Mkoa wa Kigoma amewataka askari wote kunza siri za watoa taarifa ili kulifanya Taifa letu kuwa na amani iliyopo iendelee
Kamanda alisema kuwa washiiriki hao watalisaidia Jeshi la Polisi katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi katika maeneo mbalimbali hasa katika kila kata hadi tarafa kuendelea kufundisha polisi jamii katika kila maeneo waoyopangiwa.
Mafunzo hayo yanayo tolewa mala moja kwa kila wiki moja yanawashirikisha Wakuu wa Vituo vya Polisi 18 na Askari 132 wa Vyumba vya Mashtaka kutoka vituo mbalimbali vya Polisi katika Wilaya zote tatu Kigoma mjini Kasulu,na Kibondo.