TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 15, 2013

G-8 SUMMIT PUB, KUFURU, YASHEREHEKEA KUTIMIZA MWAKA MMOJA, NA KANGA MOKO NDEMBE NDEMBE

 Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakisherehekea G-8   SUMMIT PUB, kutimiza Mwaka mmoja.
 Wacheza  Shoo wa Kanga Moko Ndembe ndembe, wakipagawisha na Mfalme wa nyimbo za Asili, Mfalme Siboka. 
 Mkurugenzi mkuu wa G-8 SUMMIT PUB, Mama Siliwa, menye kofia, akiwa na baadhi ya mashabiki wa G-8 SUMMIT, na miongoni mwa wadhamini wa Sherehe hizo wakati wa kutimiza mwaka mmoja.
 Mashabiki wa G-8 SUMMIT Wakifuatilia kwa makini sherehe hiyo.
 Mdau wa G.8 SUMMIT PUB, Tomaa Jamaa, kati na mkurugenzi wa G-8 Summit Pub, Mama Siliwa, wakifuatilia Burudani kutoka kwa Mfalme wa ngoma za asili Siboka na kundi la Kanga Moko.
  Mdau wa G.8 SUMMIT PUB, Tomaa Jamaa, kati na mkurugenzi wa G-8 Summit Pub, Mama Siliwa, wakibariki Shampeni muda mfupi kabla ya kuifungua.
 MC- akiwa na mmoja wa washereheshaji katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja G-8 SUMMIT PUB.
  Mdau wa G.8 SUMMIT PUB, Tomaa Jamaa, kati na mkurugenzi wa G-8 Summit Pub, Mama Siliwa, wakgonganisha glass wakati wa kubariki hafla hiyo.
 Keki yenye nembo ya jina la G-8 SUMMIT, muda mfupi kabla ya kuandaliwa.
 Mkurugenzi wa G-8 Summit Pub, Mama Siliwa, akijiandaa kwa ajili ya zoezi la Keki.
 Mama Siliwa akiwa na baadhi ya wafanyakazi wake na Watoto wake Judith Felix Siliwa, Brenda Mushi na Wengine.
 Mkurugenzi wa G-8 SUMMIT, Mama Siliwa akiwalisha baadhi ya wageni waalikwa Keki wakati wa Sherehe hiyo, miongoni mwao akiwa ni mkurugenzi wa MY WAY Entertainment, Poul Mganga na Rose Mwita. pamoja na Chusu.
 Mkurugenzi wa G-8 SUMMIT, Mama Siliwa, akifungua burudani ya muziki kwa watu wote.
Mkurugenzi wa MY WAY Entertainment, Poul Mganga na mke wake  Rose Mwita, wakati wa hafla hiyo
  Mfalme wa Nyimbo za Asili Siboka akipagawisha.
Mashabiki wakipagawa na minenguo ya wanenguaji wa Kanga Moko Ndembendembe, chini ya Mfalme wa Nyimbo za asili Mfalme SIBOKA.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

MAJONZI YATAWALA JIJINI DAR ES SALAAM NI BAADA YA KUWASILI MWILI MAREHEMU DK.MVUNGI

 Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku lililohifandhi mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.
 Waombolezaji waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa Dk. Mvungi.
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.
 Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.
Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe

Ndugu wakilia kwa uchungu...
Na Father Kidevu Blog
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.
Makumi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.
Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake nombemba 2 mwaka huu na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne Mvungi.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya.
Sanduku hilo lilifunikwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi. 
Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unataraji kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao Kisangara juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya jumatatu.
________________
MUDA
TUKIO
LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE
Saa 12:50 jioni
Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
Saa 2:00 – 3:30 asubuhi
Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji
Saa 3:30 asubuhi
Kuwasili Mwili wa Marehemu
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee
Saa 5:45 – 6:55 mchana
Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani
Saa 6:55 – 8:40 Mchana
Kuaga Mwili wa Marehemu
Saa 9:00 Alasiri
Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU - KIBAMBA, MSAKUZI
Saa 2:30 – 4:30 asubuhi
Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu
Saa 5:00 asubuhi
Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro