TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, May 5, 2012

SPIKA WA BUNGE AWA MGENI RASMI KILELE CHA MAADHIMISHO YA ALBINO MKOANI LINDI


  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Ndg. Abdalah Omar kutoka Chama cha Albino Tanzania juu ya matumizi ya mafuta maalum ya ngozi kwa ajili ya watu wenye ulemevu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za watu wenye ulemavu wa Ngozi. Spika alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.
(Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge)

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akipokea DVD maalumu kuhusu Albino na Maisha yao kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Under the Same Sun Bi. Vicky Mtetema wakati wa maadhimisho ya  Siku ya Albino yaliyofanyika Lindi. Shirika la ni mdau mkubwa wa watu wenye ulemavu wa Ngozi na linajishughulisha na kutoa elimu kwa watu wenye Ulemavu wa Ngozi pamoja na Misaada mbalimbali. Spika walikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.

Dk. Mashingo Lerise kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Ngozi na Saratani (Ocean Road) akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na taasisi hiyo kwa watu wenye ulemavu (Albino) baada ya Mhe. Spika kutembelea banda lao wakati wa kilele cha Siku ya Albino kitaifa iliyofanyika Lindi. Kulia ni baadhi ya madaktari wa saratani ya Ngozi kutoka taasisi hiyo katika Hospitali za KCMC na Mkoani Lindi.
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila, Spika wa Bunge  Mhe. Anne Makinda, Mweneyikiti wa Chama cha albino Tanzania Ndg. Ernest Kimaya, na Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ndg. Danford Makala wakipokea maandamano wakati wa kuadhimisha siku ya Albino Mkoani Lindi ambapo Spika alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.
Bi. Zakia Matimbwa kutoka Albino Revolution Cultural Troup cha Dar es Salaam akighani Ngonjera iliyobeba ujumbe wa kulaani mauji ya Albino wakati wa katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana. Mhe Spika alikuwa Mgeni rasmi katika kilele hicho.

UWT KIVUKONI WATANGAZA NAFASI ZA UONGOZI


UMOJA wa Wanawake nchini (UWT),  Kata ya Kivukoni wilaya ya Ilala umetangaza nafasi mbalimbali za uongozi kwa wanachama wake katika kata hiyo ambapo uchukuaji fomu umekwishaanza tangu Mei 4 mwaka huu.Katibu wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kata hiyo, Omary Omary alisema hayo jijini Dar es Salaam leo, kuwa mwisho wa uchukuaji fomu hizo utakuwa Mei 11 mwaka huu.
Alisema nafasi zinazopaswa kugombaniwa na wanachama wa chama hicho ziko nane (8), ambapo kila mwanachama hai anayo nafasi ya kujitokeza katika kuomba moja ya nafasi hizo.
Omary alizitaja nafasi hizo kuwa ni pamoja na Mwenyekiti nafasi moja, Katibu nafasi moja, wajumbe wa kamati ya utekelezaji wanatakiwa wanne, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata nafasi moja.
Nafasi nyingine ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya nafasi mbili , mjumbe wa Halmashauri ya Kata nafasi moja , mwakilishi kutoka UWT kwenda Wazazi nafasi moja na mwakilishi kutoka UWT kwenda Uvccm nafasi moja .
Omary alitanabaisha kuwa fomu zinapatikana katika ofisi ya CCM kata ya Kivuko kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:jioni ambapo kila fomu moja muombaji atapaswa kuilipia shil. 10,000/=.

WATANZANIA WAFANYA MATEMBEZI YA AMANI KATIKA JIJI LA YOKOHAMA NCHINI JAPAN

  Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani, Jilly Maleko na Francis Mossongo wakijiandaa tayari kwa matembezi ya hisani yenye lengo la kuhamasisha juhudi za kufufua uchumi na utalii wa jiji la Yokohama.
      Maandalizi yakiendelea
Watanzania wanaoishi nchini Japani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wengine kutoka mataifa ya Afrika katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa matembelezi hayo.
Watanzani wakipeperusha bendera ya Tanzania katika Matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na jiji la Yokohama
Matembezi yamekolea, Mwenyekiti wa watanzania wanaoishi nchini Japani Radhid Njenga (mwenye kanzu) naye alikuwemo.
Noboru Ninomiya (mwenye picha ya tingatinga) mwenyeji wetu katika matembezi haya akiwa sambamba na Francis Mossongo, Afisa Ubalozi.
Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani, wamewaongoza watanzania wanaoishi hapa kushiriki katika matembezi ya hisani ya mji wa Yokohama, ikiwa ni moja ya hatua za kukuza urafiki kati ya jijini hilo na Tanzania.
 
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na hata mataifa ya Afrika kushiriki rasmi kwenye matembezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka. Mwaka huu, Tanzania kutokana na historia yake ya kupenda, kusimamia na kutetea amani, umoja na mshikamano duniani.
Aidha katika siku za usoni, mji wa Yokohama una mpango wa kuanzisha uhusiano (Sistercity Friendship) na moja ya miji ya Tanzania, uhusiano ambao utajumuisha kupanda miti aina ya Cherry blossom katika mji utakaochaguliwa Tanzania.
Matembezi hayo yalianzishwa mwaka 1953 kwa lengo la kuhamasisha jitihada za kufufua uchumi na utalii wa mji wa Yokohama kufuatia uharibifu uliotokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Friday, May 4, 2012

RASMI SIMBA BINGWA, AZAM WATOKOTA UWANJA WA TAIFA BAADA YA KUCHAPWA GOLI 2-1 NA MTIBWA SUGAR


SIMBA leo wanaanza kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Azam FC kufungwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ina pointi 59, ambazo sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote msimu huu na imebakiza mechi moja dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumapili ambayo kwao itakuwa ya kulinda heshima tu.
 Lakini Azam tayari imejihakikishia nafasi ya pili kwenye ligi hiyo na hivyo kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
Waliokuwa mabingwa watetezi Yanga, hawana tena chao- kwani hata wakiifunga Simba keshokutwa watabaki nafasi ya tatu tu, hivyo mwakani hawavuki mipaka ya nchi.

Tumaini pekee la Yanga kucheza michuano ya Afrika mwakani ni iwapo Simba SC itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu- ikiwa imebakiza mitihani miwili kufikia mafanikio hayo.
Inatakiwa kuitoa Al Ahly Shandy ya Sudan- na baadaye iitoe timu itakayokutana nayo kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua hiuyo, ambayo itakuwa imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
Hapo, Tanzania itakuwa na nafasi mbili kwenye Kombe la Shirikisho mwakani, kwa mujibu wa kanuni mpya za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Tayari Simba imeifunga Shandy mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza na inahitaji sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kusonga mbele.

Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Awadh Issa dakika ya 25, wakati kipindi cha pili, Wakata Miwa hao wa Manungu waliokuwa wanashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa Simba, walipata bao la pili dakika ya 59, mfungaji akiwa ni Juma Abdul.

Awadh alifunga bao lake akiunganisha kona iliyochongwa na nyota wa mchezo wa leo, Juma Abdul ambaye naye alifunga bao la pili kwa mpira wa adhabu, baada ya Luckson Kakolaki kumchezea rafu Vencent Barnabas Saramba. John Raphael Bocco aliifungia Azam bao la kufutia machozi.

RAIS JAKAYAKI KWETE AKITANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri leo April 4, 2012
(PICHA IKULU)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo April 4, 2012
Wapiga picha wakiwa kazini wakati Rais Jakaya Kikwete akitangaza Baraza la Mawaziri leo ikulu
Wanahabari wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo April 4, 2012

Rais Jakaya Kikwete Apangua Baraza la mawaziri



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2.              OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
3.              OFISI  YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4.              WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr.  John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof.  Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5.              NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6.              OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7.              OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8.              WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012

Tuesday, May 1, 2012

SHEREHE ZA MEI MOSI ZAFANYIKA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wanayakazi wa Sekta mbali mbali za
Serikali na Sekta Binafsi wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kilele
cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEY DAY)zilizofanyika jana katika
ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kushoto) Mwenyekiti wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar,Zahrani Mohamed
Nassor,(kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali
Suleiman, {Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi   Fedha tasilim Margreth Peter Mathew
wa Nelia Hotel & Resort Zanzibafr, Shilingi za Kitanzania Laki
Saba,(700,000/=)  kupitia Chama cha wafanykazi (CHODAU) akiwa katika
miongoni mwa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012,wakati wa sherehe za siku
ya wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama
Bwawani Hotel Mjini Unguja. {Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi   Fedha tasilim Kidawa Juma said
Shilingi za Kitanzania Laki Mbili na Hamsini Elfu (250,000/=)
Mfanyakazi Bora,wa Halmashauri  ya Wilaya ya Magharibi kupitia Chama
cha wafanykazi (ZALGWU) akiwa katika miongoni mwa wafanyakazi bora kwa
mwaka 2012,wakati wa sherehe za siku ya wafanyakazi Duniani
zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawani. {Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.}
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati ) akishikana mikono na viongozi wakati
wa Sherehe za  kilele cha Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Duniani,na kuimba wimbo wa (Solidariti Foreva) wakinyanyua juu mikono
kuonesha mshikamano katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
zilizofanyika sherehe hizo  leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati ) akishikana mikono na viongozi wakati
wa Sherehe za  kilele cha Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Duniani,na kuimba wimbo wa (Solidariti Foreva) wakinyanyua juu mikono
kuonesha mshikamano katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
zilizofanyika sherehe hizo  leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 

SHEREHE ZA WAFANYAKAZI MEI MOSI MKOANI DAR ES SALAAM LEO


Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi Mwnantum Mahiza akitoa hotuba wakati wa sherehe za MEI MOSI leo zilofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo kitaifa sherehe hizo zimefanyikia mkoani Tanga mgeni rasmi akiwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Kikwete.Kushoto ni Mwenyekiti wa TUCTA mkoa wa Dar es salaam Bw Hassan Kaumo.
Wafanyakazi kutoka Vyama mbalimbali vya wafanyakazi wakiwa wamefurika katika viwanja vya mnazi mmoja kusherekea MEI MOSI leo huku watu wengine wakijaribu kuingia katika viwanja hivyo kama wanavyoonekana katika uzio.
 Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakisubiri kuanza kwa sherehe hizo jijini Dar es salaam.
Unaweza ukafikiria huyu ni mlemavu Lah. siyo mlemavu ila kijana huyu aliyetambulika kwa jina la Hashimu Ibrahimu aliamua kutoa burudani kwenye sherehe za Mei Mosi ili kujipatia kipato.kama usemi unaosemwa mgeni njoo mwenyeji apone.

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI TANGA


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Mei 1, 2012
(PICHA NA IKULU)
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa wafanyakazi akiwa kashikana mikono na Rais wa Jumuiya ya Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mh, Waziri wa Kazi na Ajira Mh Gaudence Kabaka (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Galawa katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Mei 1, 2012
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu kama zawadi kwa  Mfanyakazi bora wa Tanesco Bi Anetha Chengula  katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Mei 1, 2012
Wafanyakazi wa Ofisi za Bunge wakiigiza kikao cha bunge wakati gari lao lilipokuwa linapita mbele ya Rais Dkt Jakaya Kikwete katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Mei 1, 2012 
 Viongozi mbalimbali wakiwa katika jukwaa kuu wakati wa sherehe hizo kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga leo
 Hii ni sehemu wa wafanyakazi waliojitokeza katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga leo.
 Viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na wabunge pamoja na viongozi wa siasa wakiwa katika wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi katika sherehe za Mei Mosi Mkoani Tanga leo.
Baadhi ya Wafanyakazi na wananchi waliojitokeza kwenyesherehe hizo wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Mkwakwani leo.