TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 15, 2014

MASHABIKI WA MBEYA CITY KABLA YA MECHI DHIDI YA SIMBA MDA HUU NI BALAAA








Mashabiki wa Simba  wakiingia jijini Mbeya



CHADEMA YALE YALE YAMPIGA CHINI MSHINDI WA KURA ZA MAONI, WAWEKA MBEBIZ KWENYE UBUNGE

Wajumbe  wa  mkutano  mkuu  wa uchaguzi  jimbo la Kalenga  walivyompongeza Sinkala Mwenda  siku ya  kura za maoni  baada ya  kushinda wenzake 13.
KAMATI kuu   ya  chama cha  Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemteua aliyekuwa  mshindi  wa  pili  wa  kura  za maoni katika zoezi la kura  za maoni Bi Grace Tendega kupeperusha bendela ya Chadema katika uchaguzi mdogo  jimbo la Kalenga.

Habari za uhakika  kutoka ndani ya  kamati  kuu ya  Chadema iliyoketi  jijini Dar es Salaam leo zinadai  kuwa  aliyekuwa mshindi   wa  kura za maoni  mwanasheria  Sinkala Mwenda  hajateuliwa na kamati  kuu  hiyo mbali ya  kuongoza kwa kura  kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani  wake wa karibu Grace Tendega 

Katibu  wa  Chadema wilaya  ya  Iringa vijijini Felix  Nyondo ameuthibitishia  mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com  kuwa amepata  taarifa  hizo  za  kuteuliwa Bi Grace  Tendega  kuwa  mgombea wa Chadema  jimbo  hilo la Kalenga .

Hata  hivyo  alisema anapongeza maamuzi ya kamati  kuu na  kuwataka wana Chadema Kalenga kujiandaa kwa   kampeni  za uchaguzi huo na kuanza  kumnadi  mgombea  wao ili  kuweza kushinda  uchaguzi  huo mdogo.

Kutokana na uteuzi sasa Tendega  atavaana  Godfrey Mgimwa wa  CCM katika uchaguzi  huo   ili kuziba nafasi iliyoachwa  waziri na aliyekuwa mbunge wa  jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa  mwaka  huu.

Hata  hivyo  duru  za kisiasa kutoka ndani  ya  Chadema  zinadokeza  kuwa sababu ya kuachwa kwa mgombea  huyo aliyeshinda kura za maoni mwanasheria Mwenda ni kutokuwa na mtaji wa  watu  kwa maana ya  kutokubalika ndani na nje ya  chama hicho hivyo  Chadema  kuona kumsimamisha Mwenda ni kulipoteza jimbo  hilo.

Huku kwa upande wa mteule  wao Bi Tendega  amekuwa na sifa ya  kugombea  katika  jimbo hilo kupitia chama cha Jahazi Asilia na kufanya vema  japo si kwa  kushinda hivyo nin imani  yao kupitia Chadema  anaweza  kufanikiwa  kushinda.

Chadema kimeshindwa kwa mengi uchaguzi madiwani

  Ni kicheko kwa CCM kwa sababu kimeshinda katika kata 24, huku Chadema kikiambulia ushindi katika kata tatu na NCCR-Mageuzi kata moja.
Wapo wanaosema uchaguzi mdogo uliofanyika Februari 8 mwaka huu katika kata 27 zilizopo ndani ya mikoa 15 nchini umepeleka chereko CCM na majonzi Chadema.
Ni kicheko kwa CCM kwa sababu kimeshinda katika kata 24, huku Chadema kikiambulia ushindi katika kata tatu na NCCR-Mageuzi kata moja.
Wengi walidhani kuwa Chadema kingeweza kufanya vyema, kutokana na kwamba uchaguzi ulifanyika ikiwa zimepita siku kadhaa tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kufanya Operesheni Pamoja Daima na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), katika mikoa mbalimbali nchini.
Wapo waliogusia helikopta tatu zilizotumiwa na chama hicho katika operesheni hizo, hasa ile ya Pamoja Daima, pamoja na mpasuko uliokikumba baada ya kumvua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.
Mbali na Kabwe, pia kiliwafukuza uanachama aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wake mkoani Arusha, Samson Mwigamba.
Binafsi naamini kuwa zipo sababu nyingi zilizosababisha Chadema kishindwe kufanya vyema katika uchaguzi huu, ikilinganishwa na uchaguzi mdogo wa madiwani wa Julai mwaka jana ambapo kilishinda katika kata zote nne za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi mkoani Arusha.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya chama hicho  kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni).
Katika uchaguzi wa Februari 8, Chadema kimepoteza Kata ya Nyasura iliyopo mkoani Bunda na Kata ya  Mkongolo iliyopo jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ambazo wameshinda CCM.
Lakini kimeibuka na ushindi katika kata mbili za Sombetini na Njombe Mjini ambazo awali zilikuwa za CCM. Pia kiliibuka na ushindi katika Kata ya Kiborloni ambayo hata kabla ya uchaguzi huo, diwani wa kata hiyo alikuwa wa Chadema.
NCCR-Mageuzi chenyewe kiliweza kutetea Kata ya Kilelema mkoani Kigoma huku CCM kikipoteza Kata ya Njombe Mjini ambayo ilikwenda kwa Chadema.
Chadema kimeangushwa na daftari la kudumu la wapiga kura.
Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haijawahi kulifanyia maboresho daftari hilo jambo ambalo naamini limeathiri uchaguzi huo na watu wengi wamepoteza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Katika kipindi hicho chote NEC imeendelea kujificha kwenye kichaka cha Sheria iliyoianzisha (Sura ya 343). Sheria hiyo inaeleza kwamba uboreshaji wa daftari hilo utafanyika mara mbili kwa miaka mitano, yaani baada ya Uchaguzi Mkuu kupita na kabla ya uchaguzi unaofuata.

EPL News: Winga wa zamani wa Preston na England Sir Tom Finney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91

Winga wa zamani wa Preston na timu ya taifa ya England Sir Tom Finney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Finney ambaye ameichezea Preston North End zaidi ya michezo 400 ya ligi kati ya 1946 na 1960 na kuichezea michezo 76 timu ya taifa ya England, aliifungia timu ya taifa ya England magoli 30 na kuingia kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote wa timu yaifa ya England akishikilia nafasi ya sita ambapo anafungana na Alan Shearer na Nat Lofthouse.





WASSIRA,MAKAMBA, NAO WAHOJIWA NA KAMATI NDOGO YA MAADILI CCM

 Naibu Waziri wa Mawasiliano  Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa White House mjini Dodoma mara baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili CCM jana.
January Makamba akiondoka kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira akitoka nje ya ukumbi wa White House baada ya kumaliza mahojiano na Kamati Ndogo ya Maadili CCM mjini Dodoma jana.
Stephen Wassira akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi. Wassira aliwaeleza waandishi kuwa hakukuwa na tuhuma juu yake.
Wassira akifurahia jambo na Kada maarufu wa CCM, Adam Soud mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari mjini Dodoma.

AJIRA HIZI HAPA: WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA UHAMIAJI


Kamishna Mkuu wa idara ya Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji kwenye
vyeo vya Koplo na Konstebo wa uhamiaji.

A: MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI NAFASI 70
1. SIFAZINAZOHITAJIKA
Awe na shahada ya kwanza au Stashahada ya juu kutooka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo; Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa habari, Ualimu, Usafirishaji, Rasilimali watu, Sayansi ya kompyuta, Teknolojia ya mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi majengo na Uhandisi Mitambo.
Awe na umri usiozidi miaka 35
2. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kusimamia doria sehemu za mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.
(ii) Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa hati ya mashitaka na kuendesha mashitaka.
(iii) Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya hati za uhamiaji
(iv) kufanya ukaguzi wa mwanzo wa maombi mbalimbali
(v) kupokea na kukagua hati za safari, fomu ya kuingia na kutoka nchini.
(vi) kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za uhamiaji kwa wanaostahili
(vii) kuagiza ufunguaji wa majalada ya watumiaji
(viii) kutunza kumbukumbu za ruhusa kwa wanaongia na kutoka nchini
(ix) kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za uhamiaji na uraia
(x) Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa
B. KOPLO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA
(i) Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 30
C. KONSTEBO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA
(i) Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 25
D. SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI
(i) Cheti cha ufundi stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya umeme na mitambo.
(iii) Cheti au Stashahada ya Uhazili (Certificate or Diploma in Secretarial Studies)
katika chuo kinachotambulika na Serikalì.
(iv) Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statistics) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(v) Cheti au Stashahadayavyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation
and Operation) kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali.
(vi) Cheti au Stashada katika fani ya uchapaji (Printing)
(vii) Ujuzi na elimu ya kompyuta na uandishi mzuri utazingatiwa.
E. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kufungua, kupanga na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa huduma
za Uhamiaji.
(ii) Kuandika Hati mbalímbaLi za Ubamiaji
(iii) Kufanya Doria schcme za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, treni na sehemu zenye
vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwcmo vya majini.
(iv) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni
wanaofukuzwa nchini (Deporters).
Kufanya ukaguzi kwcnye mahoteli, nyumba za kulaLa wageni na sehemu za biashara.
(vi) Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila
siku za Uhamiaji.
(vii)Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji.
F: MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATANISHO VIFUATAVYO. 
(i) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masonia kwa mujibu wa sifa zilizotajwa.
(ii) Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
(iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
(iv) Picha mbili (passport size)
(v) Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa.
G: UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yapite posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.
(i) Maombi ya nafasi ya mkaguzi msaidizi wa uhamiaji yatumwe kwa;
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM
(ii) Maombi ya nafasi ya Koplo wa uhamiaji na konstebo wa uhamiaji yatumwe kwa;
KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P 512,
DAR ES SALAAM

Wednesday, February 12, 2014

KONGAMANO LA TAFAKURI MARIDHIANO KUELEKEA KATIBA MPYA, JIJINI DAR ES SALAAM MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA RASMI LEO


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia
 Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo. 
 
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakijadiliana jambo
 Meza Kuuu.
 Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiagana na wajumbe walioshiriki Kongamano hilo baada ya ufunguzi uliofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.  Picha na OMR

TAMASHA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA MAANDALIZI YANAENDELEA

WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI 

Pichani wa tatu kulia ni  Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Serena Hotel,kuhusiana  tamasha la kwanza na la aina yake kufanyika nchini Tanzania, lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.
 “Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Pamela. Pichani kulia ni Meneja  Mawasiliano wa kampuni ya Angels Moment,Bi.Beatrice Millinga,Mratibu wa Matangazo na Mahusiano kutoka kampuni ya AZAM/Bakharessa,Bwa.Mohameda Ramadhani (Mdhamini wa tamasha hilo),pamoja na mwisho kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya MONTAGE LTD,Bi,Teddy Mapunda.
Pichani ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar wakiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya mkutano kumalizika.
==========================================================
WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KWANZA LA KIPEKEE LA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Beatrice Millinga
Kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa wadau wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo kujitokeza na kudhamini tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalotarajiwa kufanyika kuanzia Februari 19 - 21, 2014 kwenye Ukumbi wa  Dar Live - Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Serena leo, Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya hiyo, Bibi Pamela David amesema kuwa makampuni na mashirika mbalimbali yatapata fursa ya kujitangaza,  na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao kwa wanawake na vijana wa Kitanzania.
“Kwa kudhamini Tamasha hili wadau watapata sio tu fursa ya kutangaza biashara na huduma zao bali kujitangaza wao wenyewe na kutoa elimu kwa umma maana si wananchi wote wanauelewa wa huduma zitolewazo na mashirika na makampuni mbalimbali hapa nchini,” alisema Bi Pamela.
Kwa mujibu wa Bi Pamela, Tamasha hilo ni la kwanza na la aina yake kufanyika nchini Tanzania lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.
“Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Pamela.
Aliongeza kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha tamasha hilo, msemaji wa kampuni, Bi Pamela alisema “Tamasha litakuwa kwenye mfumo wa maonesho pamoja na vipindi vinne vya uwasilishaji wa mada mbalimbali toka kwa wanawake wafanyabiashara waliofanikiwa na wataalamu waliobobea kwenye nyanja hizo.
Kwa mujibu wa msemaji huyo watoa mada wanaotarajiwa kuwasilisha ni pamoja na Naibu Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Natu Mwamba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)  Bibi Irene Isaka.
Tamasha linatarajia kuwavutia washiriki 5,000 na waonyesha bidhaa 50 kutoka maeneo mbalimbali katika sekta ya usimamizi wa fedha. Pia, inatarajiwa kuvutia washiriki toka sekta nyingine ikiwemo biashara zenye mahusiano na suala zima la uhifadhi wa fedha na uwekaji wa akiba kwa wanawake.
Mgeni rasmi wa Tamasha hili anategemewa kuwa Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal.
Mualiko wa Mama Asha kwenye Tamasha hili unachagizwa na ujasiri na mchango wake, pamoja na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kusaidia wanawake, vijana na makundi mbali mbali yenye uhitaji nchini Tanzania.
Tamasha limedhaminiwa na Said Salim Bakhresa (SSB), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Benki ya CRDB, STANBIC, FINCA, Mamlaka ya  Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Wadhamini wengine ni pamoja na Mfuko wa UTT, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) na Kampuni ya Ashton Media.

Mvua yazidi kukwamisha vyombo vya Usafiri Masasi kuelekea Mtwara


Magari yakipishana kwa shida katika eneo hilo la Kijiji cha Mkalapa,Mkoani Mtwara kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo.
Wakazi wa kijiji hicho pamoja na Abiria wanaosafiri kwenda Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru wakiwa wamesimama bila kujua cha kufanya wakati magari yakiwa yamekwama.
*******
Na:Abdulaziz Video,Masasi.

Barabara ya Ndanda kwenda Masasi eneo la Kijiji cha Mkalapa,limekuwa ni majanga matupu kama inavyoonekana katika picha hapo chini,kwani barabara hiyo imeharibika vibara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha matika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Abiria wanaofanya safari katika maeneo hayo,inapaswa wajiandae kwa kupoteza masaa kadhaa katika eneo hilo,kwani mambo hayajakaa sawa.

Hivyo wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara (TANROADS),wanapaswa kulishughulikia swala hili haraka iwezekanavyo ili kuwaepusha watumiaji wa barabara hiyo kuondokana na hadha hii inayowaathiri wasafiri waendao Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru

mkuu wa mkoa wa Njombe akunwa na ufanisi wa shule ya makete girls

 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi(katikati) akikagua majengo ya shule mpya wa wasichana wilayani Makete, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka.
 Ukaguzi huo ukiendelea.
 Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Msangi(hayupo pichani) akizungumza nao
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza kwenye mkutano shuleni hapo
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi akizungumza na wananchi shuleni hapo.
============================================================
Habari/picha na  Edwin Moshi, Makete.

Kufuatia kukamilika kwa kiasi kikubwa majengo ya shule mpya ya sekondari ya wasichana Makete iliyojengwa katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete, mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Asseri Msangi ameagiza shule hiyo iandikishwe ili ianze kutumika.

Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo hii leo Februari 11, 2014 wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu wilayani Makete, ambapo baada ya kufika shuleni hapo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuona haina sababu ya shule hiyo kuendelea kukaa bila kuandikishwa ili ianze kupokea wanafunzi.

Akizungumza na wananchi wa vijiji viwili vinavyojenga shule hiyo ambavyo ni Utweve na Masisiwe, mkuu huyo wa mkoa mbali ya kupokea na kutjibu kero za wananchi, amekasirishwa na tabia ya wazazi wa vijiji hivyo kuwaambia watoto wao wafeli kwa makusudi ili wasiendelee na masomo ya sekondari.

"Ndugu zangu dunia tuliyopo sasahivi, si ile tuliyoishi zamani, mtoto asiposoma ni matatizo kwake, na ninyi wazazi wenye tabia ya kuwaambia watoto wenu wafeli kwa makusudi mnatupelekea taifa letu kaburini na sisi hatutakubali, tunaomba muiache hiyo tabia, somesheni watoto wenu" alisema Msangi.

Katika hatua nyingine Kapteni Msangi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya shule hiyo maalum kwa ajili ya wasichana kama njia mojawapo ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Shule hiyo pekee ya wasichana wilayani Makete inajengwa na serikali kwa kushirikiana na wazawa wa Makete wanaoishi nje ya wilaya hiyo, wananchi pamoja na wadau mbalimbali.

MWALIMU AJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA KUPITIA CHADEMA

Katibu wa Chadema  Wilaya ya Iringa Vijijini, Felix Nyondo (kulia) akipokea fomu kutoka kwa Mwalimu Vitus Lawa (kushoto). Fomu hizo ni kwa ajili ya kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa Chadema Jimbo la Kalenga, Iringa. Baadhi ya wadau waliomsindikiza Mwalimu Vitus Lawa kurejesha fomu za kuchaguliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Kalenga katika ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga, Iringa. Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na waandishi (hawapo pichani) baada ya kurudisha fomu za kuwania kuchaguliwa Ubunge wa Jimbo la Kalenga katika ofisi za chama hicho zilizoko Kata ya Gangilonga, Iringa.

Vituko Vyuoni na Mifano ya Mitandao ya Umbea