TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 12, 2014

KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA ATEMBELEA MAGEREZA TANZANIA

PIX 1Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (wa nne kulia) akiwa na  Jenerali wa Magereza Tanzania John Minja (katikati)  wakimsiliza kwa makini Mnadhimu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta Manyara akijitambulisha. Kamishna Chato  ametembelea Makao Makuu ya Magereza ikiwa kni ziara ya siku sita nchini Tanzania.Wa tatu kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Yumbe, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Tebuho Nyambe na wa kwanza ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza James Nkoloma wote kutoka Makao Makuu ya Magereza nchini Zambia. PIX 2Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato ( wa nne kushoto), akipokea taarifa fupi kutoka kwa mmoja wa maofisa  kiwandani Ukonga. Kamishna Percy alitembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, Dar es salaam kuona shughuliza za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanyika. PIX 3Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato akisaini kitabu cha wageni Kiwandani Ukonga, wa pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Tanzania Dkt Juma Ali Malewa.
PIX 4 Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (katikati) akifurahia kukaa katika moja ya samani zinazotengenezwa kiwandani Ukonga, kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Tanzania, Dkt Juma Ali Malewa na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza wa Zambia John Yumbe. PIX 6Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato wa (pili kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa mafundi katika Karakana ya magari ya Magereza iliyoko Ukonga Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa.
PIX 7Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Paredi maalum (halipo pichani) lililoandaliwa maalum kwa jairi yake katika uwanja wa paredi wa Chuo Cha Maafisa wa Magereza Ukonga.Nyuma yake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa na mwenye nguo za kijani ni Kaimu Mkuu wa Chuo  Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundi.
PIX 8Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akikagua paredi maalum lililoandaliwa kwa heshima yake katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar es salaam.
PIX 9

Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) cha Ukonga jijini Dar es salaam wakionesha aina mbalimbali za mzoezi ya kujihami na kuanguka bila kuumia katika kukabiliana na hatari yoyote, mblele ya Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (hayupo pichani)
PIX 10Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (katikati) akifurahia “juice” ya madafu aliyoandaliwa katika viwanja vya Garden Ukonga Dar es salaam wa pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini Dkt. Juma Ali Malewa na wa Kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza nchini Zambia John Yumbe kwa pamoja wakifurahia “juice” ya madafu. PIX 11kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Kikosi Maalum cha KMKGM jinsi ya kujiandaa ktuliza ghasia magerezani au popote pale itakapohitajika. Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja wa Magereza.

Kamishna wa Magereza nchini Zambia yuko katika ziara ya siku sita nchini kufuatia mwaliko uliotolewa kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza wa Tanzania John Minja mwezi Septemba mwaka, 2013 alipotembelea Magereza nchini Zambia. Ziara ya Kamishna Percy pamoja na maafisa wengine watatu ni kudumisha ushirikiano uliopo kwa muda mrefu baina ya nchi hizi mbili na magereza kwa ujumla. Akiwa nchini Tanzania Kamishna Percy atatembelea baadhi ya Magereza na Vyuo vya Mkoa wa Dare es salaam, Kilimanjaro na Arusha ili kujionea shughuli za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanywa kwa vitendo na kuona maeneo ambayo taasisi hizi mbili zinaweza kubadilishana uzoefu.PIX5Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (wa pili kulia) akiangalia samani maridadi kabisa zinazotengenezwa kiwandani Ukonga ikiwa ni sehemu ya huduma ya urekebishaji wa wafungwa kwa vitendo.
======================================================

KAMATI KUU YATEUA MGOMBEA WA CCM KALENGA

==================================

MGIMWA 2 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha kwa waandishi wa habari, mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa, Godfrey William Mgimwa (kushoto), leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Nape amemtambulisha Godfrey ambaye ni mtoto wa Marehemu Dk. William Mgimwa, baada ya Kamati Kuu ya CCM kumpitisha, leo kuwania nafasi hiyo ya Ubunge.
=============================================================

MAGEREZA YAZINDUA DUKA LA “DUTY FREE SHOP” – RUANDA, MBEYA

===================================

photo 1(1)Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil anatarajia kuzindua rasmi Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya kesho saa 3:30 asbuhi Februari 12, 2014 katika Viwanja vya Ofisi ya Magereza Mkoa wa Mbeya ambapo shughuli hiyo itashuhudiwa na Viongozi mbalimbali toka Ofisi za Serikali, Binafsi pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya Gereza Kuu Ruanda, Mbeya.
Mpango huu wa ujenzi wa Magereza “Duty Free Shops” katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala unatekelezwa  kwa Mafanikio makubwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza unaosimamiwa kimkakati na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja hivyo kutimiza adhima  ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa  Maafisa, Askari wa Jeshi la Magereza pamoja na familia zao katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, mpaka sasa jumla ya “Duty Free Shops” tano (05) zimezinduliwa sehemu mbalimbali hapa nchini hususani katika Mikoa ya Dar es Salaam(Ukonga), Dodoma(Gereza Isanga), Morogoro(Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira), Kilimanjaro(Gereza Karanga, Moshi) na Mwanza(Gereza Butimba).
Kuzinduliwa kwa Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya kunafanya idadi yake kuongezeka na kufikia jumla ya Magereza “Duty Free Shop” sita(06) ambazo zimekamilika hapa Nchini katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala.
Vyombo vya Habari ikiwa wadau muhimu katika dhima ya kuuhabarisha umma vinakaribishwa kwenye tukio la uzinduzi rasmi wa Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya kesho Februari 12, 2014 kuanzia saa 3:30 asbuhi katika Viwanja vya Ofisi za Magereza Mkoa wa Mbeya.
=============================================================

Mabingwa Airtel Rising Stars wasichana wajazwa noti

==================================

indexTIMU ya wasichana ya Tanzania imekabidhiwa zawadi ya Sh milioni 16 baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika Septemba mwaka jana nchini Nigeria.
Timu hiyo ilitwaa taji hilo baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 lililofungwa na Donisia Daniel katika fainali hiyo.
Akipokea fedha hizo jana (Februari 10, 2014) Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Msanifu Kondo alisema wanaishukuru Kampuni ya Airtel kwa kutimiza ahadi yao ya zawadi ya fedha hizo na tayari wamezikabidhi kwa makocha na wachezaji wa timu hiyo.
Alisema kila mchezaji amepewa Sh 850,000 wakati kocha mkuu wa timu hiyo Rogasian Kaijage amepewa Sh milioni moja na laki mbili na kocha msaidizi amepewa Sh milioni moja.
“Tunawashukuru Airtel kwa kutoa fedha hizo za zawadi kwa timu hii na sisi tumewakabidhi wahusika,” alisema.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wao kama wadhamini wa mashindano hayo wametimiza ahadi yao kwa kukabidhi fedha hizo kwa mabingwa hao.
“Kwa niaba ya Airtel Tanzania tunaipongeza timu ya wasichana ya Tanzania kwa kutwaa ubingwa huo, lakini pia tumetekeleza ahadi yetu ya kukabidhi zawadi, kama mnavyofahamu kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mambo ya kijamii lakini pia michezo ikiwemo soka kupitia michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwa kushiriki na klabu ya Manchester United,” alisema.

No comments:

Post a Comment