Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’ kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabondia wanaofanya mazoezi katika GYM ya Uhuru uwanja wa Basket. Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ameipiga tafu
GYM ya mchezo wa ngumi ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Dar es salaam kwa kuwapatia vifaa vya mchezo huo
akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Super D alisema amevutiwa na uanzishwaji wa GYM hiyo ambayo ina uwezo mkubwa wa kuwatoa mabondia wazuri kipindi kijacho
aliongeza
kwa kusema kuwa unajua hizi GYM za mtaani zipo chache sana na wana
uhaba wa vifaa vya kufundishia hivyo mimi nimeamua kujitolea gloves
mikono mitatu kwa kuanzia ili wapate moyo wa kuendelea na mazoezi
pamoja na kujipatia DVD za mafunzo maana ndiyo timu ambazo tunazitegemea kwa siku za usoni kutuletea mabondia wakali watakaoweza kutuletea medali na kutupa sifa nchi hii
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Mohamed Chipota amesema vifaa hivyo pamoja na DVD za mafunzo ya ngumi vimekuja wakati muafaka kwa kuwa kulikuwa nau uhaba wa vifaa kama hivi
hivyo
tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutupa sapoti kama alivyofanya
Super D yeye ni kocha wa Mkoa wa Kimichezo Ilala sasa hapa kama
amewekeza mabondia wa ilala sasa watatokea hapa kwa siku za usoni
tumeanza hivi karibuni lakini mategemeo yangu ni kuibua vipaji vipya kabisa vya mchezo wa masumbwi nchini alisema Chipota
Super D ambaye anajihusisha na uuzaji wa DVD za mafunzo ya ngumi pamoja na vifaa vya mchezo huo zikiwemo, Gloves,Gum shit, Clip bandeji dambel,Protector,bukta, fulana na vifaa vyote vya mchezo wa masumbwi |
No comments:
Post a Comment