TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 15, 2014

Chadema kimeshindwa kwa mengi uchaguzi madiwani

  Ni kicheko kwa CCM kwa sababu kimeshinda katika kata 24, huku Chadema kikiambulia ushindi katika kata tatu na NCCR-Mageuzi kata moja.
Wapo wanaosema uchaguzi mdogo uliofanyika Februari 8 mwaka huu katika kata 27 zilizopo ndani ya mikoa 15 nchini umepeleka chereko CCM na majonzi Chadema.
Ni kicheko kwa CCM kwa sababu kimeshinda katika kata 24, huku Chadema kikiambulia ushindi katika kata tatu na NCCR-Mageuzi kata moja.
Wengi walidhani kuwa Chadema kingeweza kufanya vyema, kutokana na kwamba uchaguzi ulifanyika ikiwa zimepita siku kadhaa tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kufanya Operesheni Pamoja Daima na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), katika mikoa mbalimbali nchini.
Wapo waliogusia helikopta tatu zilizotumiwa na chama hicho katika operesheni hizo, hasa ile ya Pamoja Daima, pamoja na mpasuko uliokikumba baada ya kumvua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.
Mbali na Kabwe, pia kiliwafukuza uanachama aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wake mkoani Arusha, Samson Mwigamba.
Binafsi naamini kuwa zipo sababu nyingi zilizosababisha Chadema kishindwe kufanya vyema katika uchaguzi huu, ikilinganishwa na uchaguzi mdogo wa madiwani wa Julai mwaka jana ambapo kilishinda katika kata zote nne za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi mkoani Arusha.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya chama hicho  kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni).
Katika uchaguzi wa Februari 8, Chadema kimepoteza Kata ya Nyasura iliyopo mkoani Bunda na Kata ya  Mkongolo iliyopo jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ambazo wameshinda CCM.
Lakini kimeibuka na ushindi katika kata mbili za Sombetini na Njombe Mjini ambazo awali zilikuwa za CCM. Pia kiliibuka na ushindi katika Kata ya Kiborloni ambayo hata kabla ya uchaguzi huo, diwani wa kata hiyo alikuwa wa Chadema.
NCCR-Mageuzi chenyewe kiliweza kutetea Kata ya Kilelema mkoani Kigoma huku CCM kikipoteza Kata ya Njombe Mjini ambayo ilikwenda kwa Chadema.
Chadema kimeangushwa na daftari la kudumu la wapiga kura.
Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haijawahi kulifanyia maboresho daftari hilo jambo ambalo naamini limeathiri uchaguzi huo na watu wengi wamepoteza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Katika kipindi hicho chote NEC imeendelea kujificha kwenye kichaka cha Sheria iliyoianzisha (Sura ya 343). Sheria hiyo inaeleza kwamba uboreshaji wa daftari hilo utafanyika mara mbili kwa miaka mitano, yaani baada ya Uchaguzi Mkuu kupita na kabla ya uchaguzi unaofuata.

No comments:

Post a Comment