Akipokea maelezo ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa na baadae kuzungumza
na wananchi wa eneo hilo, mkuu wa wilaya aliambiwa na baadhi ya wakazi
wa asili wa eneo hilo kuwa sehemu hiyo ilikua ni bwawa la maji miaka
yote.
Wakazi hao ambao nyumba zao zimezungukwa na maji walimuomba Mkuu wa
wilaya kusaidiwa pampu kubwa ili maji hayo yavutwe na kupelekwa kwenye
mitaro upande wa pili wa barabara.
Akijibu maombi hayo Mh. Hapi aliwaagiza mainjinia wa manispaa
kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta
maji hayo. Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni aliwaambia wananchi
kuwa wale wote waliojenga katika eneo hilo ambalo ramani inaonesha kuwa
ni eneo la wazi wajiandae kuondoka.
"Serikali itawasaidia kutoa haya maji kama hatua ya dharura. Lakini
suluhu ya kudumu ni kuwa waliojenga hapa wote wamejenga eneo la wazi
tena ni bwawa. Hivyo lazima wajiandae kuhama.
Serikali kazi yake ni kuwaambia wananchi ukweli, hata kama ukweli huo
utakua na maumivu. Hivyo ukweli wa jambo hili ni kuwa waliojenga hapa
wahame."
Akitoa rai kwa viongozi wa serikali ya mtaa ambao wameshiriki katika
kuuza eneo hilo kinyume na taratibu mh. Mkuu wa Wilaya aliagiza na
kusema
" kila Mwananchi aliyejenga hapa aende ofisi ya mtaa kujisajili akiwa na
vielelezo vyote vya kumiliki eneo hili na alikonunua. Kisha nipewe
taarifa na uhakiki utafanyika. Kama kuna viongozi wa serikali ya mtaa
walishiriki kuuzia watu viwanja hapa kinyume na ramani ambayo wao wana
nakala yao basi wajiandae kuwajibishwa."
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya alitembelea eneo la Mbweni ambako
Mwananchi asiyefahamika amejenga ukuta kuzunguka eneo la wazi. Hapi
alifika eneo hilo na kujionea ukuta huo kisha akaagiza mtendaji wa mtaa
pamoja na anayejenga ukuta huo kufika ofisini kwake kesho Ijumaa mchana
wakiwa na vielelezo vyote na vibali vya ujenzi kama wanavyo.
Ziara ya mkuu wa wilaya inaendelea muda huu katika maeneo ya barabara za Sinza ambazo wakandarasi walipewa kujenga.






Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akipima afya yake kujua kama ana vimelea vya ugonjwa wa malaria baada ya
kutoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mjini Dododma
Aprili 25 mwaka huu.

Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Bi. Rehema Kilonzi (Kushoto) akielezea mbele ya wanahabari
(hawapo pichani) kuhusu hatua ya kazi ya mkakati wa utozaji wa faini kwa
Wamiliki wa ardhi waliokiuka masharti ya uendelezaji na ulipaji kodi ya
pango la ardhi leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Uliopo
jijini Dar es Salaam.












Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa
Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake
bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na
Biashara, Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa
Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia ) na ujumbe wake kabla ya
mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Muh’d Dahoma akifungua mafunzo ya
siku moja kwa wandishi wa Habari kuhusu maradhi ya kipindupindu katika
Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo( wa pili kulia), Kansela wa ubalozi
wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) na Maneja wa ampuni ya
uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa pamoja wakionesha
kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo-
Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampunia uchimbaji wa Dhahabu ZEM
Tanzania Limited,uchimbaji wa madini hayo utafanyika katika kijiji cha
Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mwezi Desemba mwaka 2016.
Kansela
wa ubalozi wa China, Gou Haodong(kushoto) akiweka saini kitabu cha
wageni ofisi kwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nishati Profesa
Sospeter Muhongo(kulia) mara baada ya kumaliza kutano wao.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum
iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja
la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi
la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa
akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu akizungumza katika moja ya mikutano yake na wanahabari.
akamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama waChama cha Wanasheria
Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa
Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa lengo la
kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya
Chama hicho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT
Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa
Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea
Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo
mbalimbali kwa Mtoto wa kike.