TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, April 28, 2016

WAKAZI 267 WA MKOANI NJOMBE WANUFAIKA NA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA

Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO-Dar es salaam

Jumla ya wagonjwa 267 wa mkoani Njombe wamenufaika na huduma za matibabu za madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali za hapa nchini.

Takwimu hizo zimetolewa leo mkoani Njombe na Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu wakati akitoa taarifa za maendeleo ya zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa wananchi chini ya ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Amesema kuwa kati ya wagonjwa hao, 13 wamepatiwa huduma ya upasuaji kutoka kwa madaktari bingwa pia huduma hizo zinaendelea kutolewa katika Hospitali ya Kibena mkoani humo.

"Tunawashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuitikia wito wetu, leo ni siku ya tatu lakini tumeshawapatia matibabu jumla ya wananchi 267 kati ya hao wagonjwa 13 wamepatiwa huduma ya upasuaji, tunawasihi waendelee kuja kwakua bado tuna siku mbili za kuendelea kuwapatia huduma za afya"alisema Singu.

Amefafanua kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa waliopatiwa matibabu mkoani hapo ni wanawake ambao wengi wao wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo pamoja na mfumo wa mkojo.

Lengo wa mpango huu wa kutumia madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za Kanda ni kuhakikisha kuwa huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa zinawafikia wanachama wa Mfuko huo na Watanzania kwa ujumla popote walipo.

Mpaka sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umepeleka huduma ya madaktari bingwa katika Mikoa 14 ikiwa na lengo la kuhakikisha huduma bora za matibabu zinatolewa kwa usawa.Singu ametoa wito kwa wananchi wa mkoani Njombe kuendelea kujitokeza kwa wingi kujipatia matibabu kwa kuwa huduma hizo zinatolewa kwa gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment