TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, April 24, 2016

[ NAPE ATAJA MAJIPU MANNE KATIKA SANAA NCHINI,AHIDI KUYATUMBUA



Na Woinde Shizza,Arusha

Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja
mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini
na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali
itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji
wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za
wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na
tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii
maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza
ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.
“Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni
uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema
Nape

Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya
kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake
atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia
wasanii hao pamoja na kulinda haki zao.

Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii
nchini pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa
kazi za msanii maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba
na kusema kwamba familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi
sasa kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218
zilitengenezwa nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi
kufikia 14,00 huku akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua
kwa kasi nchini na kuongeza ajira .

Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon
Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia
kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

“Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa
wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba

Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la
uharamia wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba
wafanyabiashara na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali
vya luninga kwa lengo la kuinua sekta hiyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One
Mining Ltd ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal
Shabhai alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo
ni kutoa mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata
ili kuinua sekta ya ajira nchini.

No comments:

Post a Comment