TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, April 27, 2016

MADEREVA BODABODA WATAKIWA KUINGIA DARASANI KUELIMISHWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI

Waendesha bodaboda wametakiwa kwenda darasana kupata elimu ya usalama barabarani ili kuweza kuepusha ajali za maramara kwa mara zisizo tarajiwa .Hayo yalibainishwa na diwani wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Usariver Mary Antony wakati akiongea na madereva wa bodaboda hao mara baada ya kuwalipia ada ya mafunzo ya usalama barabarani, madereva 45 wa kata ya usa river.Alisema kuwa ni wajibu wa kila dereva bodaboda kwenda kupata elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara, kwa kusababishwa na uzembe wa madereva hao.“mimi kama diwani wa viti maalumu niliamua kwenda kuwalipia ada ya mafunzo madereva hawa wa bodaboda ili angalau waweze kujua sheria za barabarani na pia waweze kupata leseni, maana hawa wote hawana leseni na si hivyo tu nadhani iwapo madereva hawa watazijua hizi sheria za bara barani, itasaidia kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zinatokea”alisema MaryAlibainisha kuwa ni wajibu wa kila dereva kujua sheria na iwapo atajua sheria watajiamini na pia awatasumbuliwa ata na polisi wa usalama barabarani njiani kwani watakuwa wanajua sheria hivyo ata akiambiwa amefanya kosa ataweza kujua ni kosa kweli au amedanganywa kwakuwa tayari anajua sheria hizi za usalama wa barabarani.Kwa upande wake mmoja wa vijana wa bodaboda wa kata hiyo ya Usariver alisema kuwa anamshukuru diwani huyo kwa kuwasaidia kwani wamejitambua na wanajua sheria na aliwasihi madereva wenzake kwenda mashuleni kujua sheria hizo.Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo wameyapata yatawasaida kujiamini na pia yamewasaidia pia kutowaogopa askari wa barabarani kama zamani ,kwani kwa sasa wanajua sheria ya usalama barabarani na sio hivyo tu katika mafunzo hayo pia wamefundishwa mafunzo ya ulinzi shirikishi ili kuweza kuwatambua wezi na jinsi ya kujiepusha na wateja ambao hawaeleweki 

No comments:

Post a Comment