TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 20, 2013

KIWANJA KIPYA CHA MARAHA AIRPORT JIJINI DAR ES SALAAM

1a 2 3 4 5 6 7 8 9 10a 10b 11

NANI MTANI JEMBE!! KIVUMBI JUMAMOSI OKWI ATUA YANGA KUWAKABILI SIMBA


1 
Okwi katikati baada ya kuwasili JNIA akiwa na Katabaro kulia na Bin Kleb kushoto jioni hii na chini akionyesha jezi namba 25.

Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
HABARI ya mjini kwa muda huu ni kwamba; mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel Anord Okwi amewasili alasiri  ya leo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam tayari kwa kuanza kazi ya kuitumia klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Okwi ametia miguu Tanzania saa 9:30  kwa ndege na kulakiwa na viongozi wa Yanga ambao walikuwa na uchuku wa kupokea jembe lao la kazi.
Waandishi wa habari walikuwa na uchu wa kusikia kauli ya Okwi na ndipo muda ukafika baada ya nyota huyo kutoka nje ya uwanja wa JNIA ambapo alisema amekuja Yanga kufanya kazi.
Alipoulizwa sakata lake la usajili, Okwi alifungua mdomo wake kwa mara nyingine na kusema; “Mimi nimekuja kufanya kazi, hayo mengine hayanihusu, zipo mamlaka zinazohusika na zitajua la kufanya”.
Cha kufurahisha Okwi amewasili akiwa tayari ameshavalia jezi ya Yanga, namba 25 mgongoni.
Akizungumza uwanjani hapo, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema Okwi anakwenda moja kwa moja katika hoteli ya Protea kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kesho kutwa ya Nani Mtani Jmebe dhidi ya Simba sc, uwanja wa Taifa.
Wakati Okwi akiwa amewasili, taarifa iliyopatikana kutoka mtandano wa MTNFootball.com  mchana wa leo imeeleza kuwa kaimu mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho la soka nchini Uganda FUFA, Decolas Kiiza amethibitisha kuwa FIFA wamemruhusu Okwi kujiunga na Yanga.
“Ndiyo tuliandika barua FIFA na walisema mchezaji yuko huru kuuzwa”. Kiiza aliuambia mtandao wa MTNFootball.com.
Mapema wiki hii Mkurugenzi mkuu wa FUFA, Edgar Watson alisema wameiandika FIFA barua kuhitaji maelezo zaidi juu ya suala la Okwi.
Okwi aliuzwa na Simba katika klabu ya Etoile Du sahel ya Tunisia januari mwaka huu kwa kitita cha dola 300, 000 za kimarekani, lakini hakudumu katika klabu hiyo kwa madai ya kutolipwa haki zake na kuamua kurejea kwao Uganda.
Okwi baada ya kurejea kwao Uganda alikaa miezi sita bila kucheza na ndipo shirikisho la  kandanda la Uganda (FUFA) likasimama kidete kumpigania aruhusiwe kureja nyumbani na kujiunga na Sport Club Villa ya Uganda `Majogoo wa Kampala`  ili kulinda kiwango chake.
Kwa usajili wa Okwi, Yanga imetimiza wachezaji watano wa kigeni kwa maana ya washambuliaji Didier Kavumbagu, Khamis Friday Kiiza, beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima.
Sakata la Okwi lilifikishwa FIFA na mpaka sasa Etoile Du Sahel hawajailipa Simba Sc fedha za mauzo ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye akili kubwa ya mpira na kasi alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda katika michuano ya CECAFA Chellenge jijini Nairobi na kuonesha kiwango cha juu na sasa ametua Jangwani.
Yanga wamefanya usajili huo kwa lengo la kuimarisha kikosi chao kabla ya kuanza kampeni za ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
Mpaka sasa wametangaza kumsajili Juma Kaseja, Hassan Dilunga na leo hii Okwi imetia nanga katika rada zao.

MAMA SALMA APOKEWA KWA SHANGWE BAADA YA KURUDI NA TUZO YA UONGOZI KUTOKA DUBAI

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja kumpokea tarehe 19.12.2013IMG_1779 (1) 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi IMG_1790 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ofisi za WAMA, ambako mamia ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya kumpongeza baada ya kurudi na Tuzo ya uongozi aliyopokea huko Dubai tarehe 18.12.2013.IMG_1795 
Baadhi ya wananchi walioshiriki mapokezi ya Mama Salma wanaonekana wakimsikiliza wakati alipokuwa akiwahutubia katika viwanja vya WAMA tarehe 19.12.2013.IMG_1834 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi waliofika kumpokea aliporejea kutoka Dubai tarehe 19.12.2013.  Mama Salma alienda huko kupokea Tuzo ya uongozi ulitukuka kutokana na kazi anazofanya kupitia Taasisi yake kwa ajili ya elimu kwa wanaotoka katika mazingira magumu, afya ya mama na mtoto pamoja na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.IMG_2046 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiongea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Raymond Mushi wakati wa shamrashamra za kumpokea Mama Salma baada bya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kupokea TUZO ya uongozi uliotukuka. Tuzo hiyo hutolewa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi, (CELD).
IMG_2026 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza na wananchi waliofika kumpokea kwenye ofisi za WAMA tarehe 19.12.2013.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

RAIS DKT. KIKWETE AENDA MAREKANI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA

kikwe
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatano, Desemba 18, 2013, kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za uchunguzi wa afya yake na kwa kutilia maanani siku za kusafiri kwenda Marekani na kurudi nchini, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo, Desemba 26, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013

IDDY MNYEKE AMPANIA COSMAS CHEKA DESEMBA 31

Bondia Iddy Mnyeke  akipambana na Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala  Amana CCM Dar es salaam mabondia hawo watapanda ulingoni kuwakabili wapinzani wao ambapo Mnyeke atacheza na Cosmas Cheka na King class mawe atazidunda na Mohamed Kashinde desemba 31 katika ukumbi wa msasani klabu  kulia ni kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Picha na BLOG YA SUPER D

Na Mwandishi Wetu 
BONDIA Iddy Mnyeke  yupo katika mazoezi mazito akijiandaa na mpambano wake na Cosmas Cheka utakaofanyika desemba 31 katika ukumbi wa msasani klabu jijini ar es salaam 
 
akizungumzia mpambano huo mnyeke amesema cheka ni mtoto mdogo sana anazani anaweza kusafiria nyota ya kaka yake ajue ameingia anga nyingine hivyo ata kiona cha mchema kuni kwa  mimi sio kama mabondia aliewai kuwashinda  
Mnyeke ambaye anafanya mazoezi katika kambi ya ilala jijini Dar es salaam ameongeza kwa kusema siku hiyo watu waje kwa wingi wangalie anavyo mchakaza na kuongeza kuwa waje yeye na kaka yake ili apate msaada wakati atakapo mwangusha chini kwa ngumi kali misri ya nondo 
ambazo zitakazo msambalatisha raundi za awari kwani yeye ni cha mtoto kwake

Katika mchezo huo kutakuwa na michezo mingine ambapo  bondia  Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’  ataoneshana ubabe na Mohamed Kashinde,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine ni kati ya Fransic Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga kutoka Kenya 
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU NA UTAWALA BORA ZANZIBAR AWEKA JIWE LA MSINGI LA KITENGO KIPYA CHA UTIBABU WA UTI WA MGONGO NA UBONGO

01 (2) 
 Jengo jipya la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo linalojengwa kwa mashirikiano ya Serekali ya Spen na ya Zanzibar.03 (1) 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame (wakatikati) akiongozana na viongozi mbalimbali kuweka jiwe la msingi la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, sherehe hiyo imefanyi Mnazi mmoja Hospitali Mjini Zanzibar.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATUNUKU SHAHADA ZA UZAMILI KWA WAHITIMU TAASISI YA NELSON MANDELA ARUSHA

IMG_7192  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, akiwa kwenye maandamano ya wahitimu wa shahada ya uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.IMG_7153 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.IMG_7184  
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha akimkabidhi zawadi maalum Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.IMG_7161 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ,  akimtunuku Clarence Msafiri mhitimu wa shahada ya uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.IMG_7212
IMG_7205 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa shahada ya Uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.
(Picha na OMR