TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 5, 2014

NGUMI ZA NELSON MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP ZAFUNGULIWA KAWE

Bondia Fabian Gaudence kushoto akipambana na Hussein Mnimbo  wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yabayofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Gaudence alishinda mpambano huo kwa pointi

Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma  kushoto  akimtupia makonde Hafidhi Kassimu wa Ngome
wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika
Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam
 

 

Bondia Part Kimweri kutoka Tanga  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Jabir wa Ngome Dar
wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika
Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Kimweri alishinda mpambano huo kwa pointi

Baadhi ya viongozi wakifuatilia mashindano hayo
Mkeni wa heshima katikati Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete akiwa na viongozi wa Shilikisho la mchezo wa ngumi za Ridhaa nchini kulia ni Rais wa shilikisho hilo Mutta Rwakatare  makamu wa rais Lukelo Willilo na
Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
MAREFARII MABONDIA NA VIONGOZI WAKISUBILI KUFUNGULIWA KWA MASHINDANO HAYO
Nwa BFT Antony Mwangonda akiwa na makamu wa Rais Lukelo Willilo
…………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelson Mandela Open Championship  yameanza kutimua vumbi katika

Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam


akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa hali ya juu Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini ‘BFT’ Lukelo Willilo ‘amesema mashindano hayo kwa sasa yameboreshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia hawavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;’


Zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa hawavai kofia wanapigana vichwa wazi  ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bure tu hakuna kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo ambayo yanahusisha mikoa mbalimbali nchini


Mashindano haya yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinaanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku michezo ndiyo itakuwa ikiisha


Katika ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence 
akimsambalatisha Hussein Mnimbo

9 KANEMBWA WATAKIWA KUWASILISHA UTETEZI

tff_LOGO1 Wachezaji tisa wa Kanembwa JKT pamoja na timu yao wanaolalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumpiga mwamuzi Peter Mujaya wanatakiwa kujitetea mbele ya Kamati ya Nidhamuitakayokutana Jumapili (Februari 9 mwaka huu).

Utetezi huo unaweza kuwa wa mdomo kwa walalamikiwa kufika wenyewe mbele ya kamati itakayokutana saa 4 kamili asubuhi au kuuwasilisha kwa njia ya maandishi.

Kamati ilikutana jana Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko dhidi ya wachezaji hao na timu yao kwa tukio hilo lililotokea Novemba 2 mwaka jana kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Stand United FC iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Wachezaji hao ni Abdallah Mgonja, Bariki Abdul, Philipo Ndonde, Mbeke Mbeke, Mkuba Clement, Mrisho Mussa, Nteze Raymond, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu. Mlalamikiwa mwingine ambaye naye anatakiwa kujitetea ni timu ya Kanembwa JKT.

Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, Kamati hiyo baada ya kusikiliza malalamiko dhidi ya wahusika na kupokea ushahidi wa aina mbalimbali kutoka kwa mlalamikaji imesema ili iweze kutenda haki katika shauri hilo ni lazima walalamikiwa wapate fursa ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo iliyokutana kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa imesema imesikitishwa na vitendo vya fujo ndani ya mpira wa miguu, na kuwataka watu wasijihusishe na aina yoyote ya fujo.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JAKAYA KIKWETE ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA UTAWALA ZA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UNOFANYWA NA KIKOSI CHA UJENZI CHA JESHI LA MAGEREZA, MJINI DODOMA

image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maelezo ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kibwana Kamtande (wa kwanza kushoto) alipotembelea hivi karibuni Mjini Dodoma(wa kwanza kulia) ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda(wa pili kulia) ni Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge. Mhe. William Lukuvi. image_1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda(katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Kibwana Kamtande kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea kufanya ukaguzi wa Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mhe. Rais ameonyesha kuridhishwa na kasi ya ukarabati unaofanywa na Jeshi l Magereza kupitia Shirika lake la Magereza.
  image_2
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Kibwana Kamtande(wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wanasimamia kwa karibu Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalokarabatiwa na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza ambapo hivi karibuni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameridhishwa na kasi ya ukarabati wa Jengo hilo alipotembelea Mjini Dodoma(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). photo
Hatua mbalimbali iliyofikiwa  ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Mjini Dodoma ambapo hivi karibuni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alifanya ukaguzi wa Ukarabati wa Jengo hilo na kurudhishwa na kasi ya Ukarabati huo unaofanywa na Jeshi la Magereza kupitia Kikosi chake cha Ujenzi kilicho chini ya Shirika la Magereza.

TASWIRA YA MCHEZO KATI YA SIMBA NA MTIBWA SUGAR KATIKA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO

Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba Kilichoanza Dhidi ya Mtibwa
Nyuma Kuanzia Kushoto: Kocha Msaidizi Seleman Matola,Tambwe,Amri Kiemba,Joseph Owino,Jonas Mkude,Musoti.Mbele Kushoto:Singano,Awadhi,Haruna Chanongo,Ivo Mapunda,Rashid Baba Ubaya,Haruna Shamte.
Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Nyuma kuanzia Kushoto:JumaLuizio,Shaban Nditi, Hassan Ramadhan,Ally Shomary Salim Mbonde.Mbele Kuanzia Kushoto : Jamal Mnyate,Said Mkopi,Shaban Kisiga, Husein Sharif,Salvatory Mtebe,Mussa Mgosi.
Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
Rashid Baba Ubaya Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Mtibwa Sugar Said Mkopi.
Kipa wa Mtibwa Hasani Sharifu
Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo
Golikipa wa Timu ya Mtibwa Sugar Hussein Sharif Akiwa Ameokoa Moja ya Purukushani katika Lango Lake.Akishihudiwa na Beki wake Salim Mbonde Pamoja na Mshambuliaji wa Simba Khamisi Tambwe.
Simba wakishangilia Goli lao lilofungwa na Khamis Tambwe Bao lililofungwa dakika 50 ya mchezo.
Mpira Umemalizika Mtibwa 1 -1 Simba. Goli la Mtibwa Sugar Lilifungwa dakika ya 18 ya Mchezo bao Lililofungwa na Mussa Mgosi .Hadi Mapumziko Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa Goli Hilo Moja.Kipindi cha Pili Mpira ulianza kwa kasi Simba walishambulia Lango la Mtibwa mara kwa mara Na kujipatia bao la Kusawazisha katika dakika ya 50 ya Mchezo.Katika Mchezo Mchezaji wa Mtibwa Shaban Nditi Alionyeshwa kadi Nyekundu Dakika ya 69 baada ya Kutoa maneno Machafu kwa Mwamuzi.Dakika ya 72 Said Ndemla anaingia Kuchukua nafasi ya Haruna Shamte,Dakika ya 75, Juma Mpakala Aliingia Kuchukua nafasi ya Jamal Mnyate.Dakika ya 87 wanafanya mabadiliko ya mwisho, aliingia Abdallah Salum Kuchukua nafasi Mgosi..

WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR YABADILISHANA MAJENGO NA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ).

01
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakitia saini makubaliano ya ubadilishanaji  majengo ya Taasisi hizo mbili katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya Kiislamu ya PBZ Mpirani mjni Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Abrahamani Mwinyi. 02
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili ambapo PBZ itachukua jingo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi na Wizara ya Biashara itachukua Jengo la Makao Makuu ya sasa ya PBZ la Darajani 03
Baadhi ya Maofisa wa PBZ wakiangalia utiaji saini wa makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Benki hiyo na iliyokuwa Ofisi ya Shirika la Biashara ya Magari lililochini ya Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
04
Picha ya pamoja ya maafisa wa PBZ na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko baada ya kumalizika hafla ya makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Taasisi hzo mbili iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya kiislamu ya PBZ Mpirani mjini Zanzibar.

05
Jengo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa ajili ya kujenga Makao Makuu Mapya ya Benki hiyo. 06 
Jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) liliopo Darajani Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

IGP MANGU AFANYA MABADILIKO KWA BAADHI YA MIKOA

db950-3Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
 
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki  anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
 
Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi  Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
 
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi  Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .
 
Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
 
Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji   anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
 
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe  Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi  (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,   Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.   
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.
 
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi

RAIS AZUGUMZA NA WATANZANIA,WAZIRI WA AFYA NA KUALIKWA CHAKULA KWA MAKAMO WA RAIS WA INDIA

TA1A2250
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii wa India Shri Ghulam Nabi Azad, alipowasili katika hoteli ya Oberoi Mjini New Delhi alipofikia Rais na Ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini India,[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2255
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa India Shri Ghulam Nabi Azad, alipowasili katika hoteli ya Oberoi Mjini New Delhi alipofikia Rais na Ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini India,[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2259
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake wakizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa India  Shri Ghulam Nabi Azad,na Viongozi aliofuatana nao walipofika katika hoteli ya Oberoi Mjini New Delhi alipofikia Rais na Ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini India,[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2267Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini India wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao jana katika ukumbi wa jengo la Hotel ya Ashok Mjini New Delhi,akiwa katika ziara nchini India ya siku tisa katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2270
Viongozi wa Ujumbe wa Rais na Vingozi wa Watanzania Nchini India  pamoja na wanafunzi wanaosoma  kupata fani mbali mbali nchini India,wakimasikiliza  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa nasaha zake wakati walipokutana jana katika ukumbi wa Hotel ya Ashok Mjini Nwe Delhi India, [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2274
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Watanzania Wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbali mbali nchini India, jana katika ukumbi wa Hotel the Ashok mjini New Delhi,akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na mashirikiano na nchi hiyo,(kulia wa kwanza) Waziri wa Uwezeshaji,Vijana wanawake na Watoto,Bi Zainab Omar Mohamed,Mama Mwanamwema Shein,na (kushoto) Balozi wa Tanzania nchini India John W.H.Kijazi, [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2279
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim,Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee na Balozi wa Tanzania nchini India John W.H.Kijazi, ni miongoni mwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara nchini India,pichani wakimsikiliza Rais wakati alipozungumza na watanzania katika ukumbi wa The Ashok Hotel Mjini New Delhi jana. [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2335
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa picha ya pamoja na Watanzania wanaosoma nchini India baada ya mazungumzo ya  pamoja nao jana katika ukumbi wa The Ashok Hotel Mjini New Delhi akiwa katika ziara ya Kiserikali. [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2339
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa picha ya pamoja na Watoto baada ya mazungumzo ya  pamoja na Watanzania  jana katika ukumbi wa The Ashok Hotel Mjini New Delhi India akiwa katika ziara ya Kiserikali. [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2350
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,(kulia) wakiwa picha ya pamoja na Makamo wa Rais wa India Mohammed Ansari na Mkewe Salma Ansari,walipoalikwa chakula cha usiku jana katika ukumbi wa Hayderabad House, Mjini New Delhi akiwa katika ziara ya Kiserikali. [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2379 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,  wakisalimiana na Viongozi wa Serikali ya India wakati wa hafla ya chakula cha usiku jana kilichoandaliwa na  Makamo wa Rais wa India Mohammed Ansari na Mkewe Salma Ansari,katika ukumbi wa Hayderabad House, Mjini New Delhi akiwa katika ziara ya Kiserikali. [Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2417 
Makamo wa Rais wa India Mohammed Ansari na Mkewe Salma Ansari, wakisalimiana na ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipowatambulisha jana wakati wa chakula cha usiku katika ukumbi wa Hayderabad House, Mjini New Delhi  katika ziara ya Kiserikali Nchini India. [Picha na Ramadhan Othman,India.]

Juma Nkamia –Naibu Waziri mpya,Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo


images
Na Eleuteri Mangi (MAELEZO)
Ni siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amuapishe Mheshimiwa Juma Nkamia kuitumika Serikali kama Naibu Waziri katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kwa taaluma, Naibu Waziri Nkamia ni mwanahabari ambaye amesomea na kufanya kazi ya habari kwa kipindi kirefu kabla ya kuingia katika Ubunge ambao umemuwezesha kuteuliwa kuwa waziri.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika wizara hiyo,   Nkamia alisema anamshukuru  Rais Kikwete kwa kumteua na kumpa dhamana hiyo na kuahidi kuwa atasaidiana na Waziri wa wizara hiyo kutimiza majuku ya wizara katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya nne.
 
“Kama kiongozi mwenye mamlaka ndani ya wizara hii, nipo tayari kushirikiana na viongozi wenzangu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara zote zinazounda wizara hiyo”, alisema.
 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaundwa na idara kuu nne za kisekta ambazo ni Idara ya Habari, Idara ya Vijana, Idara ya Maendeleo ya  Utamaduni na Idara ya Maendeleo ya  Michezo.
Kwa kuwa tasnia ya habari ni miongoni mwa idara zilizo chini ya wizara hii, Nkamia alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na wadau wa habari ikiwemo kusimamia maslahi ya waandishi wa habari nchini.
 
“Ukitaka kujua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika nchi yeyote ile, jaribu kuvifanya  vyombo hivyo kuanzia redio, televisheni na magazeti visifanye kazi hata kwa muda wa saa moja tu uone ni hasara kiasi gani na hatari kiasi gani zitatokea katika nchi ile” alisema Nkamia.
 
 Alisema anaheshimu na anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini na atafanya nao kazi vizuri kwa kipindi chote atakachokuwa wizarani hapo.
Alisema kuwa anatambua kuwa  waandishi wa habari wanafanya  kazi katika mazingira magumu wakati wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo  tatizo la “ukanjanja” na lugha mbalimbali zinozotolewa juu yao.

Dk.Shein aendelea na ziara yake India.

TA1A1758
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia taa iliyotengenezwa na Akinamama wa Zanzibaar Kisiwani Pemba alipotembelea Chuo cha Barefoot kinachotoaa mafunzo ya Amali kwa wanawake pekee katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan ncchini India akiwa katika siku ya pili ya ziara yeke katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.]
TA1A1772
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (mwenye suti nyeusi katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Barefoot kinachotoaa mafunzo ya Amali kwa wanawake pekee katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan nchini India pamoja na ujumbe wake akiwa katika siku ya pili ya ziara yake katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A1795
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( katikati)akiwa na Viongozi wa  Chuo cha Barefoot kinachotoaa mafunzo ya Amali kwa wanawake pekee katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan nchini India pamoja na ujumbe wake akiwa katika siku ya pili ya ziara yake katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2020
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiingia katika  Makumbusho ya Hawa Mahal  Mji wa Jaipur Jimbo la Rajastan nchini India  akiwa katika siku ya pili ya ziara yeke katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2030
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiingia katika  Makumbusho ya Hawa Mahal  Mji wa Jaipur Jimbo la Rajastan nchini India  akiwa katika siku ya pili ya ziara yeke katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2096
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiingia Vitu mbali mbali vya kihistiroa katika  Makumbusho ya Hawa Mahal  Mji wa Jaipur Jimbo la Rajastan nchini India  akiwa katika siku ya pili ya ziara yeke katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] TA1A2098 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiingia Vitu mbali mbali vya kihistiroa katika  Makumbusho ya Hawa Mahal  Mji wa Jaipur Jimbo la Rajastan nchini India  akiwa katika siku ya pili ya ziara yeke katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.]