TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 5, 2014

HATIMAYE ZOEZI LA KUWACHAGUA WASHIRIKI WA MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA LAANZA RASMI. FOMU ZAIDI YA 4,000 ZAKUSANYWA

2A 
Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo unavyo fanyika ili kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha Plus/Mama shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.
…………………………………………………………………………………….
    Fomu zaidi ya 4,000 za Mama Shujaa Maisha Plus zakusanywa
    Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake 20 na vijana 45
 Zoezi la kuchaguwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo  ambapo zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki.
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema zoezi la kupitia fomu litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi Alhamisi tarehe 6 Februari 2014. “Majaji walioteuliwa wana kazi kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000 ambazo tumekishwazipokea na nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Baada ya uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja na vijana 45 ambao watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia kuchambuwa fomu na vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Jinsia. “
Jopo la majaji linajumuisha waliobobea kwenye masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya jamii.
 Majaji ni kama wafuatavyo:
Rose Tesha Meneja Programu ya Maisha Salama shirika la VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 ; Francis Bonda Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus, Edmund Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoro mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa jinsia kutoka shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri wa mnyororo wa thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea Lushoto, Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha Plus 2012.
Washiriki  wa Maisha Plus msimu huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha Fedha za kitanzania Milioni 25.

No comments:

Post a Comment