TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 5, 2014

Juma Nkamia –Naibu Waziri mpya,Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo


images
Na Eleuteri Mangi (MAELEZO)
Ni siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amuapishe Mheshimiwa Juma Nkamia kuitumika Serikali kama Naibu Waziri katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kwa taaluma, Naibu Waziri Nkamia ni mwanahabari ambaye amesomea na kufanya kazi ya habari kwa kipindi kirefu kabla ya kuingia katika Ubunge ambao umemuwezesha kuteuliwa kuwa waziri.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika wizara hiyo,   Nkamia alisema anamshukuru  Rais Kikwete kwa kumteua na kumpa dhamana hiyo na kuahidi kuwa atasaidiana na Waziri wa wizara hiyo kutimiza majuku ya wizara katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya nne.
 
“Kama kiongozi mwenye mamlaka ndani ya wizara hii, nipo tayari kushirikiana na viongozi wenzangu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara zote zinazounda wizara hiyo”, alisema.
 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaundwa na idara kuu nne za kisekta ambazo ni Idara ya Habari, Idara ya Vijana, Idara ya Maendeleo ya  Utamaduni na Idara ya Maendeleo ya  Michezo.
Kwa kuwa tasnia ya habari ni miongoni mwa idara zilizo chini ya wizara hii, Nkamia alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na wadau wa habari ikiwemo kusimamia maslahi ya waandishi wa habari nchini.
 
“Ukitaka kujua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika nchi yeyote ile, jaribu kuvifanya  vyombo hivyo kuanzia redio, televisheni na magazeti visifanye kazi hata kwa muda wa saa moja tu uone ni hasara kiasi gani na hatari kiasi gani zitatokea katika nchi ile” alisema Nkamia.
 
 Alisema anaheshimu na anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini na atafanya nao kazi vizuri kwa kipindi chote atakachokuwa wizarani hapo.
Alisema kuwa anatambua kuwa  waandishi wa habari wanafanya  kazi katika mazingira magumu wakati wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo  tatizo la “ukanjanja” na lugha mbalimbali zinozotolewa juu yao.

No comments:

Post a Comment