Frank Mvungi- Maelezo
Serikali imesema haina Ugomvi na vyombo vya habari hapa nchini kama ambavyo baadhi ya vyombo
hivyo vimekuwa vikiripoti.
Akizungumza
 leo katika ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano  wa 
Serikali Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella 
Mukangara alisema haoni sababu ya kuingia kwenye ugomvi na wadau muhimu 
kama vyombo vya habari.
“Kuna
 wanaozunguka zunguka wakieleza kwamba kuna ugomvi kati yetu na vombo 
vya habari, mkiwasikia wapuuzeni”.alisema waziri Mukangara.
Dkt
 Mukangara alipongeza kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari na 
kuvitaja kuwa wadau muhimu wa Serikali katika kuwaletea wananchi 
maendeleo na kutoa taarifa.
Dkt.Mukangara
 aliongeza kuwa ni jukumu la Maafisa Habari na Mawasiliano kuwaunganisha
 wananchi na Serikali kwa kutoa taarifa zitakazowasaidia wananchi 
kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akifafanua
 zaidi Dkt. Mukangara amesema kuwa Wizara itaendelea kuratibu mikutano 
ya Taasisi za Serikali na Vyombo vya Habari ili kuwapa wananchi fursa ya
 kujua mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.
Katika
 Utaratibu huo  Dk Mukangara amesema mikutano 156 kati ya taasisi za 
Serikali na Vyombo vya Habari ilifanyika  kati ya 204 iliyotarajiwa 
kufanyika katika kipindi cha julai hadi Desemba 2013 ikiwa ni 
utekelezaji wa jukumu la msingi la kuwapa wananchi taarifa kwa wakati.
Pia
 aliwaasa Maafisa Habari na Mawasiliano kote nchini kujituma na kufanya 
kazi kwa weledi ili kuwasaidia Taifa kufikia maendeleo endelevu.
Naye
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel Alibainisha
 kuwa Mafunzo kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuimarisha 
mawasiliano ya Serikali kwa umma.,mafunzo ya vitendo kuhusu matumizi ya 
mitandao ya kijamii na mada kuhusu namna bora ya kutumia na kuendesha 
radio za kijamii.
Kauli
 mbiu ya Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano zaidi ya 100 toka 
Tanzania nzima ni Matumizi ya Tehama na Mitandao ya Kijamii katika 
kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa umma.

No comments:
Post a Comment