TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 31, 2014

waziri wa uchukuzi akutana na wafanyabishara wanaotumia bandari ya dar es salaam Jana.

unnamed1Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe, akisisitiza jambo alipokutana na wafanyabishara wanaotumia bandari ya Dar es Salaam (hawapo pichani), katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),janaunnamedMeneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Award Massawe, akisistiza jambo, wakati Waziri wa Uchukuzi, alipokutana na Wafanyabishara wanaotumia bandari ya Dar es Salaam jana asubuhi katika ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam..
unnamed2 
Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA), Edward John Urio, akisisitiza jambo wakati wa Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe, alipokutana na wafanyabishara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), jana asubuhi. (Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI : KUSITISHA USHUSHWAJI WA BEI ZA FILAMU KWA KAMPUNI YA STEPS

index
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment. wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu. Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

TATHMINI YA PAPA KAIJAGE KUHUSU MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI KWA MWAKA 2014…

unnamed
​​BENDI MPYA•Vijana Ngwasuma ilizinduliwa ndani ya Letasi Lounge (zamani Business Park ,Victoria) Ijumaa ya tarehe 07-Mar-2014.•Yamoto Band yazinduliwa rasmi tarehe 21-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.•Utalii Band yazinduliwa Ijumaa ya tarehe 26-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa MRC (Mikocheni Resort Centre) •Kundi la Chuchu Sound liliibuka tena na kupiga show kadhaa katika ukumbi wa Max Bar Ilala. Baadaye kwa sababu kadhaa bendi ikapotea.•Pia kulikuwa na bendi ambazo sio mpya lakini ndani ya mwaka 2014 ziliundwa upya. Bendi hizi ni Victoria Sound  na Ruvu Stars.•Bendi nyingine zilizoanzishwa ndani ya mwaka 2014 ni JJ Band, bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe. Pia kuna Ruby Band. Bendi hizi 2 zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2015. UZINDUZI WA ALBUM MPYA•Extra Bongo walizindua album ya “Mtenda Akitendewa” Jumamosi ya tarehe 22-Feb-2014 ndani ya Dar Live Mbagala.•Talent Band (ya Hussein Jumbe) wazindua album ya “Kiapo Mara Tatu” Jumatano ya 30-Apr-2014 ndani ya Kisuma Night Pub, Temeke (zamani Sugar Ray)•Christrian Bella azindua album ya “Nani Kama Mama” ndani ya Mzalendo Pub Jumamosi ya tarehe 30-Aug-2014•Tarsis Masela katika viunga vya Ten Lounge (Business Park) Victoria azindua album ya “Acha Hizo” Ijumaa ya tarehe 21-Nov-2014•Mashujaa Band yazindua album ya “Ushamba Mzigo” kwenye ziara za mikoani. KILI MUSIC AWARD•Kili Music Award 2014 ilifanyika Jumamosi ya tarehe 03-May-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 8  vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo; 1. Mwimbaji Bora wa Kiume-Jose Mara (Mapacha Watatu) 2. Mwimbaji Bora wa Kike-Luiza Mbutu (Twanga Pepeta) 3. Rapa Bora-Fergusson (Mashujaa Band) 4. Wimbo Bora-Ushamba Mzigo (Mashujaa Band) 5. Bendi Bora-Mashujaa Band 6. Mtunzi Bora-Christian Bella (Malaika Music Band) 7. Producer Bora-Amorosso 8. Hall of Fame (Individual)-Hassan Rehani Bitchuka (Mlimani Park Orchestra) WANAMUZIKI WALIOFARIKI•Mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed “MCD” afariki dunia Jumatatu ya tarehe 27-Jan-2014•Mpiga bass wa Vijana Jazz, Maulid Mwangia afariki Jumatano tarehe 12-Mar-2014 na kuzikwa Alhamis tarehe 13-Mar-2014•Mwanamuziki mkongwe Muhiddin Gurumo afariki dunia Jumapili ya tarehe 13-Apr-2014 na kuzikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe Jumanne ya tarehe 15-Apr-2014•Mpiga gitaa wa Skylight Band,Chili Challa wa Skylight Band afariki dunia tarehe 17-Apr-2014.•Amina Ngaluma “Japanese” afariki tarehe 15-May-2014 akiwa mji wa Phuket, Thailand.•Mwanamuziki DIGITAL wa FM Academia afariki Ijumaa tarehe 18-Jul-2014.•Ally Rashid “Mwana Zanzibar” ambaye mara ya mwisho alikuwa mpuliza sax wa Msondo Ngoma afariki tarehe 10-Oct-2014.•Suzuki Sauti ya Malaika aliyepigia Extra Bongo katika album ya “Mjini Mipango” alifariki tarehe 15-Oct-2014•Mwanamuziki Khamis Kayumba “Amigoulaus” afariki tarehe 09-Nov-2014.•Mwanamuziki Shem Ibrahim Kalenga afariki dunia 15-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 16-Dec-2014 katika makaburi ya Kisutu.•Mnenguaji Aisha Madinda afariki dunia tarehe 17-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 19-Dec-2014. MATUKIO MENGINE MAKUBWA•Mdahalo wa kwanza wa aina yake wa kujadili muziki wa dansi wafanyika katika ofisi za TBC Jumamosi ya tarehe 05-Apr-2014 chini ya u-moderator wa Dacota Khamis, kuhudhuriwa na wadau karibia 30 na kuonyeshwa live na TBC2 na baadaye kuonyeshwa recorded na TBC1 kwenye kipindi cha “Nyumbani ni Nyumbani”•Bendi ya Msondo Ngoma yafanya sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 50. Maadhimisho yalianza Ijumaa ya tarehe 10-Oct-2014 ndani ya Leaders Club na kuhitimishwa TCC Chang’ombe Jumamosi ya tarehe 01-Nov-2014. Pia wanamuziki wa bendi walikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, Alhamis ya tarehe 30-Oct-2014. •Kwa mara ya kwanza tukio la “Usiku wa Msanii” lafanyika tarehe 25-Oct-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Marehemu Father Kanuti alipewa tuzo ya Humanitarian Award.•Tarehe 09-Dec-2014, siku ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru na miaka 52 ya Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla maalum iliyofanyika katika viwanja vya ikulu atoa nishani maalum kwa kundi zima la Atomic Jazz Band ya Tanga. Tuzo hiyo ni ya miaka 50 ya Muungano ya daraja la nne. Aliyepokea kwa niaba ya kundi ni mzee Stephen Hiza (Mgosingwa). Atomic Jazz Band imepewa nishani hiyo kutokana na kazi yao kubwa katika kulihamasisha taifa kuenzi muungano hususan kwa kupitia wimbo wao wa “Tanzania Yetu”.•Mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika mara mbili kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment. Mara ya kwanza ulifanyika siku ya sikukuu ya Eid Mosi (Eid al-Fitr) tarehe 25-Jul-2014 ndani ya TCC Chang’ombe. Mara ya pili umefanyika pia TCC Chang’ombe Christmas tarehe 25-Dec-2014. Kwenye mpambano wa mara ya pili, kwa mara ya kwanza tukio limesindikizwa na bendi ya Vijana Jazz Pambamoto “Saga Rumba”.•MAONYESHO YA PAMOJA: Bendi 3 za FM Academia, Mapacha Watatu na Ruby Band zapiga pamoja Ijumaa ya tarehe 19-Dec-2014 ndani ya Mzalendo Pub. Yamoto Band mara kadhaa imefanya maonyesho ya pamoja kwa kupiga pamoja na Mapacha Watatu, Skylight Band na Twanga Pepeta. Pia Mlimani Park Orchestra wamepiga pamoja mara kadhaa na Machozi Band ya Lady Jaydee. Ruby Band walipiga pamoja na Twanga Pepeta Jumapili ya tarehe 28-Dec-2014 ndani ya Leaders Club•Onyesho la Miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta lililokuwa lifanyike Jumamosi ya tarehe 20-Dec-2014 limeahirishwa hadi tarehe 31-Jan-2015 kutokana na kifo cha mnenguaji Aisha Madinda.•Mechi ya mpira wa miguu kati ya kundi la BONGO DANSI na kundi la WATANASHATI WA MUJINI lafanyika katika viwanja vya Leaders Club Jumapili ya tarehe 23-Nov-2014. Matokeo yalikuwa suluhu 0-0. Kundi la BONGO DANSI mara kadhaa limefanya ziara ya kumtembelea Nguza Vicking na Papii Kocha ambao wapo gerezani Ukonga. •Tarehe 26-Dec-2014, umoja wa wanamuziki wa dansi katika viwanja vya Karimjee wafanya dua maalum ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete ili hali yake ya kiafya iimarike.

NAKUSHAURI RAIS WANGU KIKWETE, MUACHE MUHONGO AMALIZE KIBARUA CHAKE

Rais Jakaya Kikwete
Said Mwishehe
PANAPO MAJAALIWA ya Mungu, kesho tunaungana na mataifa mengine duniani kusheherekea mwaka mpya wa 2015.
Hivyo, kwa hesabu za kalenda ya mwaka 2014, leo hii tunamaliza muda uliobaki kabla ya kuingia mwaka 2015.
Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuendelea kutupa pumzi yake. Ametujaalia afya njema. Hili ni jambo la kushukuru.
Pia nitumie nafasi hii kutoa pole kwa ndugu, rafiki na jamii zetu ambao leo hii hatunao tena. Wametangulia mbele za haki.
Hiyo inatokana na mapenzi yake muumba wa mbingu na ardhi. Tuwaombee dua njema huko waliko.Mbele zao, nyuma zetu.
Wakati tunakaribia kuingia mwaka 2015, nitumie nafasi hii kuowambea wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
Imani yangu Mungu atawaponya na kuwarejesha kwenye afya njema na hatimaye kuendele na ujenzi wa taifa.
Wakati tunajiandaa kuupokea mwaka mpya, kuna mambo mengi ambayo yametokea kwenye mwaka huu wa 2014.
Yapo ambayo yametunufaisha kama taifa lakini wakati huo huo yapo ambayo yametufedhehesha.
Mwaka 2014 ulikuwa mwaka wa matukio mengi katika nyanja mbalimbali. Nikiri kuna mambo ya kujivunia na kuna mambo ya hovyo ambayo yametokea kwenye taifa hili ambalo linaendelea na juhudi za kusaka maendeleo yake.
Sote ni mashahidi Watanzania kwa nafasi zao mbalimbali wameendelea na ujenzi wa taifa leo. Wameendelea kudumisha umoja na mshikamano wao.
Wameendelea kuungana kupigania maisha yao. Ni watu ambao hawataki kukataa tamaa. Wanafanya kila juhudi kuhakikisha taifa linasonga mbele.
Nikiri kauli ambayo inaliumiza taifa hili ni kuendelea kuimba wimbo wa “Sisi maskini”. Wimbo ambao kwangu mimi unaniumiza kichwa. Sitaki hata kuusikia. Sitaki kuusikia kwasababu ni sehemu ya adui wetu wa maendeleo yetu.
Sisi maskini ni kauli ambayo imetukwamisha kwa miaka mingi sasa. Hata mwaka huu wa 2014, kauli ya sisi maskini imeturudisha nyuma.
Kujiita kila siku maskini ndio matokeo yake tunashinda kuishi maisha ya kuendelea kuomba misaada. Kisa tu nchi yetu eti maskini.
Kwangu naamini sisi si maskini ila huenda tunakosa mipango na usimamizi mzuri wa kufikia malengo yetu.hili ndilo tatizo ambalo linatusumbua kwa miaka mingi.
Mwaka 2015 ni mwaka wa kubadili mitazamo na fikra zetu. Tukitumia vema rasilimali zetu, tutapiga hatua. Kila kitu tunacho.tunachotakiwa ni mipango na usimamizi mzuri. Tuache akili za kuwa tegemezi kwa kila jambo.
Inashangaza tunapokuwa na msitu mkubwa wa misitu kama ule wa Sao hili Iringa halafu kijiti cha kusafishia meno kinatoka China. Ama kweli!
Inasikitisha kuona imefika mahali eti kila kitu lazima kitoke nje. Kasumba hii inatokana na yale yale ambayo wengi yametutawala kwenye akili zetu kuwa lazima tuwe tegemezi.
Hatupaswi kuwa na akili hiyo kwa mwaka 2015. Ni mwaka wa kutafakari kama taifa nini tufanye ili tusonge mbele.
Kwa bahati mbaya tumekuwa na kundi kubwa ambalo linatumia muda mwingi kupiga soga vijiweni kwa ajenda ambazo hazina mashiko ya kimaendeleo. Ni rahisi kusikia watu wanajadili nani kavaa nini. Fulani analula nini?
Wanaojadili tunapigaje hatua kama taifa ni wa chache. Hata hao tunaowategemea kutupigania wamekuwa wa kuishi kwa matukio. Likija tukio hili wamo, likija lingine wamo.Mafundi wa kuongoa kuliko kutenda.
Inasikitisha sana.Tumeyaona hayo mwaka 2014.Si vizuri yakajirudia tena mwaka 2015. Kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa, ndio kosa. Tusimamie kama nchi tuangalie maisha yetu. Tumetoka wapi na tunakwenda wapi.
Tukisoma vitabu vya historia tunaambia Tanzania na China zilianza harakati za kusaka maendeleo mwaka mmoja. Nenda leo China kaingalie.
Hatufanani nayo kwa namna yoyote ile.Watu tulianza nao kwenye harakati za kutafuta maendeleo, eti leo tunawapigia magoti kuwaomba msaada.
Wachina wameijenga nchi yao.Wameamua kusimama kidete kuhakikisha taifa lao linapiga hatua na kuwa lenye nguvu duniani.  Sishangai Marekani inapokwenda kuomba misaada ya kifedha China.
Kwetu sisi maendeleo yetu yamekuwa ya mwendo wa kinyonga. Wananchi wamekata tamaa ya maisha. Kila kukicha wanasema afadhali ya jana. Ndio maisha ambayo tumeamua kuishi.
Imefika mahali Wachina wameamua kuja nchini kwetu na kufanya kazi ambazo tumeshindwa kuzifanya. Nenda Kariakoo jijini Dar es Salaam, Wachina wanauza maua.Wanauza karanga.
Inasikitisha inapofika mahali hata karanga tunashindwa kuuza. Tunasibiri Wachina waje wauze. Halafu tumebaki kupiga kelele tu.Tumefika mahali pabaya.
Sifa ya taifa kupiga hatua za maendeleo linahitaji kuwa na siasa safi, utawala bora, ardhi na watu.
Nikiri tunaweza kuwa tumekosa siasa safi na uongozi bora lakini tuna ardhi ya kutosha na watu. Kwa bahati mbaya watu wapo lakini kasi ya maendeleo haiendani na idadi yetu.
Kitendo cha kukosa siasa safi imefika mahali, wanasiasa wengi wametugeuza kama vile kichwa na mwendawazimu. Wanatuongopea watakavyo.
Wanajua hatuna tunaloweza kulifanya. Hakika mwaka 2014, licha ya kufanya mambo ya maendeleo, yapo ambayo tunapaswa kujiepusha nayo mwaka 2015.
Msomaji wa safu hii, baada ya kutoa maelezo hayo ambayo kwangu mimi kwa siku ya leo ni kama utangulizi sasa nije kwenye ajenda yangu ya Jumatano ya leo.
Ajenda yenyewe ni hili sakata la Escrow.Sakata ambalo limekuwa gumzo kwenye kila kona ya nchi yetu. Limekuwa likizungumza na kila mtu. Kama hulizungumzi wewe basi analizungumza mwenzio.
Sakata la Escrow limetikisa nchi yetu kwa sehemu kubwa. Sote tunafahamu mjadala huo wa Escrow unatokana na utata wa fedha wa sh. bilioni 306 zilizopo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, wajanja kuamua kuzichukua.
Wanasiasa wa kada mbalimbali wamekuwa wakilizungumza hilo kwa kina. Wamekuwa wakipambana kwa hoja. Wamekuwa wakijadili na kuelezea umma kuhusu fedha hizo.
Nikiri mwaka 2014, mjadala wa Escrow kwangu mimi naona ulikuwa ni mjadala uliochokuwa sehemu kubwa ya mazungumzo kuliko mijadala mingine.
Ni kweli kulikuwa na mjadala kuhusu Katiba mpya lakini ujio wa sakata la Escrow umefunika kabisa mazungumzo ya Katiba inayopendekezwa.
Kwa kuwa hata wanasiasa wetu nao wanaishi kwa matukio. Wengi wao wameachana na ajenda ya Katiba mpya ambayo wananchi wanahitaji kuelimisha licha ya wao wenyewe kujisomea Katiba inayopendekezwa kabla ya kufanya uamuzi kwa kupiga kura ya ndio au hapa.
Leo hii ili mwanasiasa aonekane amezungumza jambo la maana basi anaamini akizungumzia Escrow ndio nyota ya siasa inasafishika.
Sina tatizo na wanasiasa ambao wamelizungumzia sakata hilo hadi hapa lilipofikia. Tunajua Bunge limetoa maazimio nane kwa Serikali.
Maazimio ambayo kwa sehemu kubwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inatakiwa kuamua kwa kuchukua hatua dhidi ya wanaohusishwa na uchotaji fedha wa Escrow.
Ndio maana aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema ameamua kuachia ngazi.
Uamuzi huo unatokana na ukweli kwamba ushauri wake kisheria hakueleweka. Jaji Werema anasema amechafua hali ya hewa.
Pia tunafahamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi naye amsimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi. Kisa sakata hilo hilo la Escrow.
Nani ambaye hafamu kama aliyekuwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka naye ametemwa kwenye baraza la mawaziri.
Kilichomuondoa ni kupokea fedha za Escrow.Prof. Tibajuka aliwekewa kwenya akaunti yake binafsi sh. bilioni 1.6.
Wakati mjadala huo unaendelea, hakuna mwanasiasa ambaye ameweza kupata ujasiri wa kuliambia taifa fedha hizo ni za umma au si za umma. Nani mwenye fedha hizo?.
Ujasiri ambao wanasiasa wetu walio wengi wanao hadi sasa ni kwamba sh. bilioni 306 za Escrow ni za umma. Wamesema hivyo wakiwa bungeni na wanaendelea kusema hivyo nje ya Bunge.
Kwangu mimi na hata kwa Watanzania wengine, nimefurahishwa na hotuba ya Rais Kikwete.Hotuba ambayo aliitoa Desemba 22 mwaka huu. Alikuwa anazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Kama kiongozi wa nchi ameonesha kulifahamu vema suala hilo. Akatumia nafasi hiyo kuelezea historia nzima ya sakata la Escrow.
Akaeleza namna ambavyo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na IPTL walivyokuwa wanalipa.
Pia, akaeleza namna ambavyo akaunti ya Tegeta Escrow iliovyofunguliwa hadi hatua ya IPTL na wanahisa wenzake kuuziana hisa na kisha kufunga akaunti ya Tegeta Escrow na kuchukua fedha zilizomo.
Rais Kikwete baada ya kutoa maelezo mengi ya kueleweka pengine kuliko yale yaliyokuwa yanatolewa na wanasiasa walio wengi akatumia nafasi hiyo kuwahakikishia Watanzania kuwa fedha hizo ni za IPTL.
Rais Kikwete katika hotuba yake alisema”Fedha hizo ni za IPTL maana ni malipo ambayo yalikuwa yanalipwa kutoka Tanesco ambazo ni tozo la uwekezaji, lakini toafuti yake fedha zilikuwa zinawekwa kwenye akaunti maalumu”.
Kimsingi hotuba ya rais imejibu swali la msingi ambalo Watanzania wengi walikosa kulisikia.Pamoja na kusema fedha hizo ni za IPTL bado akauthibitisha umma kuna kodi ya Serikali ndani yake.
Hivyo tunapoumaliza mwaka 2014, naamini rais amesema kile ambacho wengi tulipaswa kukisikia.Akasisitiza uchunguzi ufanyike na kisha sheria ichukue mkondo wake.
Akaagiza mamlaka zinazohusika na uchunguzi zitakapokamlisha taarifa , yeye atakuwa na uamuzi wa kufanya.
Baada ya kulifafanua kwa kina suala hilo, rais akatumia nafasi hiyo kuweka wazi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amemuweka kiporo.
Bwana we! kauli hiyo ya Prof.Muhongo kuwekwa kiporo imeamsha hasira za wanasiasa hasa za wapinzani.
Wametoa matamko ya kumtaka Rais Kikwete kumuwajibisha Prof.Muhongo kwa kumuondoa kwenye nafasi hiyo.
Wengine wametangaza kufanya maandamano nchi nzima.Najiuliza sababu za  msingi za kufanya maandamano hayo.
Najiuliza hivi wanaotaka Prof.Muhongo aondolewe kwenye nafasi hiyo ni kweli wanashinikiza kwa maslahi ya Taifa au kwa maslahi binafsi.
Hapa kuna siri kubwa, ambayo wenye kumshinikiza rais amuondoe Prof.Muhongo kwenye nafasi ya uwaziri wanaijua. Nani ambaye hajui kazi ambayo imefanywa na Prof.Muhongo kwenye wizara hiyo.
Amefanya mambo makubwa kwa maslahi ya nchi.Waziri Muhongo kwa usimamizi wake mzuri umeme umekwenda kwenye vijiji mbalimbali vya nchi yetu.
Nimezunguka wilaya za nchi hii 129 hadi sasa.Naiona kazi ambayo Prof.Muhongo ameifanya katika nishati ya umeme.
Nani ambaye hajui umuhimu wa nishati ya umeme kwa wananchi. Misimamo yake katika wizara hiyo imefanikisha ujenzi wa bomba la gesi.Angekuwa Waziri legelege , bomba la gesi kutoka Mtwara kuja(kwenda) Dar es Salaam lisingejengwa.
Alijua anasimamia maslahi ya taifa.Pia najua kwenye eneo la gesi amekasirisha wengi.Wapo ambao hawataki hata kumsikia.Leo si wakati wake kuzungumzia hilo.
Wanasiasa wanataka rais amuondoe Prof.Muhongo, hivi waziri mwingine ambaye atakwenda kwenye wizara hiyo na kukaa kwa miezi nane iliyobaki ya utawala wa rais Kikwete anakwenda kufanya jambo gani kubwa.
Kuna dhambi gani Waziri Muhongo akiachwa amalizie muda ambao Rais Kikwete ameubakisha.
Kwa kuwa tunaingia mwaka 2015, ni bora niseme ukweli maana utaniweka huru.Naamini sioni sababu ya kumuondoa Waziri Muhongo Wizara ya Nishati na Madini.
Tangu amekuwa Waziri wa Nishati na Madini Waziri Muhongo amefanya kazi kubwa na nzuri.Hata hao ambao leo wanamuandama wanajua.
Nikiri najua, haya ninayoeleza kuna watu nawakera lakini ni bora niwe huru kwenye kile ninachoamini.
Kauli ya Mwishehe, kaushauri Rais wangu, Rais Jakaya Kikwete , nakuomba umuache Waziri Muhongo amalizie kazi anayoifanya kwenye wizara hiyo.Binafsi sioni mahali ambapo Waziri Muhongo amechukua fedha za Escrow.
Sioni mahali ambapo Waziri Muhongo ameshauri fedha zitoke. Waziri Muhongo msimamo wake unajulikana wazi kuhusu fedha hizo.
Kwa bahati mbaya wanasiasa wetu wameng’ang’ania tu kumtaka rais amuondoe Muhongo badala ya kutoa suluhu ya nini kifanyike ili hayo ambayo yanatokea na kusababisha taifa kushindwa kuchukua kodi yake yasijirudie.
Wanasiasa wanashindana kuita vyombo vya habari kumshinikiza rais kumuondoa Waziri Muhongo.
Naamini na ndio ukweli wanafanya hivyo si kwasababu ya maslahi ya taifa , bali wanafanya hivyo kwa msuko mwingine. Ipo siku nitausema.Kwenye hili nitasimamia ukweli.
Kwenye siasa za Tanzania kuna mambo huwa yanakera sana. Moja ya mambo yanayokera ni pale mtu anaposimama kujifanya anapigania maslahi ya taifa kumbe, kichwani kwake anawaza tofauti.
Kuna wakati huwa najiuliza kwanini , wanashinikiza Prof. Muhongo aondolewe. Nawaza weee , lakini napata majibu tofauti tofauti. Moja ya jibu ambalo huwa nalipata ni kwamba wanaogombea urais nao wana yao kwenye hilo.
Tena si wa CCM tu, bali hata wa upinzani. Wanaona sakata la Escrow ni karata ya mwisho ya kufanikisha malengo yao.
Wengine wanaamini kupitia sakata hilo itakuwa njia rahisi ya kuiangusha Serikali ya Rais Kikwete bungeni.
Hivyo, kila mmoja analiangalia kivyake na si kweli wote wanaopigania hilo ni kwa ajili ya maslahi ya taifa. Ingekuwa ni maslahi ya taifa wangetuambia kwenye sh. bilioni 306 za Escrow za umma ziko sh. ngapi?
Nimalizie kwa kueleza tunaingia mwaka 2015, tudumishe upendo, umoja na mshikamano wetu. Najua wapo ambao watakaosema nimetumwa. Sijatumwa. Sitajali.
Kubwa zaidi kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake kwa kile anachokiamini anaweza kuchangia alau kidogo hasa kwa kuzingatia mwaka 2014 umebakisha saa chache tu wa uhai wake.
Karibu mwaka 2015, nitumie nafasi hii kuwataka mafanikio mema kwenye mwaka wa uchaguzi wanasiasa wote. Mwaka ambao kila anayetaka kugombea udiwani, ubunge au urais anarudi kuomba kura kwetu.
Nawaheshimu wanasiasa wote na wa vyama vyote. Kwenye ukweli nipo pamoja nanyi na kwenye uongo nitakuwa kando yenu.
Tuwasiliane 0713833822

HUYU NDIYE RAIS WA TANZANIA 2015.

Mpalule ShaabanUrais Sio Cheo, Urais ni Utumwa, Urais ni Msalaba Mzito, Rais anatakiwa kuwa Mtumishi wa Watu kwa sababu anabeba Masalaba wa Watu Wote, Rais ni Baba wa Watu Wote, anayetakiwa kuwajali Watoto Wake Wote, asiyekubali Kula Wakati Kuna Watu Miongoni mwa Watoto Wake Wakilala na Kushinda Kwa NJAA, IKULU NI MZIGO MZITO, watanzania Tayari Wenyewe Wameona na Kuyashuhudia Maneno ya BABA wa TAIFA, na kila Uzito na Ujazo Wake, Kipimo cha Uzito wa IKULU, ni Tofauti na Kipimo cha uzito wa nafasi Yoyote Kwa Uzani, Kimawazo, Kiutendaji, na Uwajibikaji wa KILA mmoja Umeonekana, Watanzania Siyo Karungu Yeye Kwamba Wao Vichwa kisha Watanzania ni Magamba wanaingia na Kutoka, Nikichungulia tu niko nje na nikichungulia tu niko ndani, KIRAIS RAISI, IKULU siyo mahala pa Kukimbilia ila SERA ndo zinampeleka mtu IKULU, Wananchi wakishamkkubali, kwa SERA zake, katika yale anayowambia wananchi kisha akayatakeleza na wananchi Watampa URAIS, URAIS aununuliwi kama Karanga, Kwamba izi ni njugu Tutauziana kwa Mafungu, URAIS wowote unaonunuliwa siku zote ikumbukwe ipo Siku Utakuja KUUZWA, Tunapomchagua mtu kuwa Rais ni kwamba tunamwambia awe mtawala wetu, awe juu yetu kwa Mamlaka ya kila jambo, mwenye maamuzi ya Mwisho, mwenye kutenda juu ya HAKI na SHERIA, kwa Faida ya Wananchi anatakiwa kutenda na si VINGINEVYO. IKULU SIYO PANGO LA WAFANYABIASHA, IKULU SIYO SEHEMU YA KWENDA KUPUMZIKA, IKULU SIYO SEHEMU YA MISIKITI, IKULU SIYO SEHEMU YA MAKANISA, IKULU SIYO SEHEMU YA MIGAO NA MIGAHAWA, IKULU SIYO SEHEMU YA WAHUNI, NA IKULU SIYO SEHEMU YA MATAMBIKO, IKULU NI MAHAPA PATAKATIFU. PA PATAKATIFU. RAIS ANATAKIWA KUWA MTAKATIFU ZAIDI YA SALA NA IBADA, Mpenda AMANI, mtetezi wa haki, Mpigania Maendeleo ya Watu Wake, Jemedari, Kamanda, Mwenye Nguvu Kimwili, Kiroho na Kimawazo, asiyeyumbishwa na jambo, Mwenye kutoa Maamuzi Sahihi, Rais atakiwi kuwa na Makundi, Rais atakiwi kuwa Mbaguzi, Rais atakiwi kuwa mwenye Uroho na Madaraka, Rais atakiwi kuwa mchochezi, Rais atakiwi kuwa Mwenye Tamaa na Uroho wa kujilimbikizia Mali, Rais atakiwi kuwa Mwenye Hasira na Mwenye Maamuzi ya Haraka, Rais atakiwi kusema Uwongo, na Rais atakiwi KUPANGIWA, Rais atakiwi kuwa na Ukabila,Rais atakiwi kuwa na Udini, Rais atakiwi kuwa Muhuni, Rais atakiwi kuwa Mlevi, Rais atakiwi kutoa RUSHWA, Rais atakiwi kupokea RUSHWA, Rais atakiwi Kulala Usiku na Mchana, atakiwi kujulikana Muda wa Kulala na Mtu yeyote Isipokuwa kwa MKE/MUME wake, Rais atakiwi kuwa mtu wa kusafiri safiri, atakiwi kuruhu au kushiriki Uovu, Rais atakiwi kuzoeleka, Rais atakiwi kuipenda Nafsi yake kuliko ya watu wake, NA URAIS hauna UMRI: 2015

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA WATANZANIA WOTE WAMETAKIWA KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA KWA UTULIVU

 Mwonekano wa jiji siku ya Leo Posta na Mnazi Mmoja
 Upanga
 Posta eneo la Bilcana Club
POSTA

GARI LA TAKA LASABABISHA TAFLANI MITAA YA SAMORA JIJINI DAR ES SALAAM.

 
 
Baadhi ya wazoa Taka wa Kampuni hiyo hapo wakijaribu kusukumu gari hilo kati kati ya jiji na kuleta mtafaruku kwa Wapiga Picha ambao walijaribu kuwapiga picha wakiwa kwenye zoezi la kusukuma gari hilo lililokuwa likileta msongamano wa magari kwenye barabara ya mtaa wa Samora, lakini hata hivyo katika tukio mmoja wa wazoa Taka hao baada ya kutoa Upepo wa Bipipiki ya Wanahabari hao, alijukuta akikokotwa mzobe kupelekwa kituo cha Polisi Central kwa kwa kosa la kuwazuia waandishi kufanya kazi zao, sakati hilo limeisha baada ya wazoa taka hao kumpigia mkuu wao ambaye alionekana mwenye busara na kuwaomba waandishi hao kumaliza Tatizo ikiwa ni pamoja na kuwapa onyo wazoa taka hao kuwa ni kosa la Jinai kuwazuia waandishi wawapo kazini.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAFANYA USAFI KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015

Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika Harakati za Kusafisha Mazingira katika kujiandaa kuupokea Mwaka wa 2015, kama walivyokutwa leo na Jicho la Kamera ya Full Utamu.

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA DR. SHEIN RAIS WA ZANZIBAR

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa salamu za mwaka mpya wa 2015 kwa  wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla  na kuwatakia mwaka wenye Amani na Utulivu pia mafanikio makubwa ikiwemo ya Uchumi wa Taifa letu,hafla hiyo ilifanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

WAFANYAKAZI WA PPF IDARA YA UENDESHAJI WAFANYA SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM JANA

Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Assumpta Maina Mallya akifungua sherehe iliyoandaliwa na idara yake kwaajili ya kupongezana kwa kazi za mwaka mzima, sherehe iliyofanyika katika hoteli ya Tiffany jijini Dar Es Salaam Jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka idara ya Uendeshaji wakimsikiliza Kwa Makini Mkurugenzi wa Idara hiyo wakati akifungua Sherehe ya Kupongezana kwa Wafanyakazi wa Idara hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Tiffany, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Assumpta Maina Mallya akikata keki kwaajili ya Kuwarisha wafanyakazi wa Idara yake katika Sherehe ya kufunga mwaka iliyoandaliwa na Idara ya uendeshaji na kufanyika katika hoteli ya tiffany Jijini Dar Es Salaam.
Mbaruku Magawa Mratibu wa Ofisi za Kanda za PPF akimrisha Keki Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa PPF, Assumpta Maina Mallya wakati wa sherehe ya kumaliza Mwaka 2014 iliyofanyika Disemba 30, 2014 katika hoteli ya Tiffany.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Assumpta Maina Mallya akimlisha Keki mmoja wa Wafanyakazi wa Idara hiyo.
Muda wa Kufungua Shampeni ukawadia

Arsenal yamlenga Carvalho na Sissoko

Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon William Carvalho anayelengwa na Arsenal.
Arsenal wanadaiwa kumfukuzia William Carvalho.
Kiungo huyo wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 22 anaweza kucheza katika safu ya kati ya ulinzi na amekuwa akilengwa na Gunners kwa mda mrefu licha ya kuwa na bei ghali.
Kilabu ya Sporting Lisbon inataka kitita cha pauni millioni 30 ,lakini kulingana na gazeti la daily mail nchini Uingereza kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kulipa pauni 25.5.
Vilevile Wenger ameripotiwa kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Newcastle Moussa Sissoko kwa kitita cha pauni millioni 9.
Moussa Sissoko wa Newcastle
Wakati huohuo meneja wa Manchester City Manuel Pelegrini anatarajiwa kumununua mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bonny ili kuchukua mahala pake Sergio Aguero ambaye ana jereha la mguu.
Gazeti la Daily Telegraph limeripoti kuwa Manchester City pia inajiandaa kumnunua mshambuliaji huyo kwa takriban pauni millioni 30.
Hatahivyo kulingana na The Times ,Chelsea pia inamtaka mshambuliaji huyo.

Mtoto zeru zeru atekwanyara Tanzania

Mazeru zeru Tanzania
Polisi nchini Tanzania wanasema kuwa wamewakamata watu wanne kutokana na kutekwa nyara kwa msichana mmoja zeruzeru.
Msichana huyo wa miaka 4, Pendo Emmanuelle Nundi alitekwa siku ya jumamosi kutoka nyumbani kwao katika jimbo la kazkazini la Mwanza.
Msemaji wa Polisi Valentino Mlowola amesema kuwa babaake mtoto huyo ni miongoni mwa wanaochunguzwa ,ili kujaribu kujua iwapo bado yuko hai.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa unasema kuwa takriban mazeruzeru 74 wameuawa nchini Tanzania ambapo vipande vya miili yao huuzwa kama vivutio vya bahati kwa takriban dola mia sita.

TMA YATOA TAARIFA JUU YA MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JANUARI, FEBRUARI, 2015 NCHINI

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, kuhusu mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Januari na Februari, 2015 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi, Huduma za Utabiri, Dk.Hamza Kabelwa.
Wana habari wakiwa kwenye mkutano huo leo
============================================

SIKU moja baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa za vipindi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agness Kijazi Dar es Salaam jana wakati akiwasilisha tathmini ya mvua za vuli kuanzia Ocktoba hadi Disemba mwaka huu na mwelekeo wa mfumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi cha Januari na Febduari 2015.
Alisema kutokana na mifumo iliyopo ya hali ya hewa inatarajiwa kusababisha vipindi vya ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo ya Magharib kwenye mikoa ya, Nyanda za juu Kusini-Magharibi na mikoa ya Kusini mwa nchi kuanzia Januari na Febduari 2015.
Hata hivyo alisema kuwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka hususan Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki, Pwani ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa Viktoria na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma mvua zinatarajia kuisha mwishoni mwa Disemba mwaka huu.
Alisema matukio ya mvua katika maeneo ya mvua za nje ya msimu yanatarajiwa katika kipindi cha miezi ya Januari 2015.Hali hiyo inatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Kusini mwa Mkoa wa Pwani na baadhi ya meneo ya Mikoa Arusha , Manyara, Kagera, Geita, Shinyanga na Mwanza.
Dk. Kijazi alisema katika maeneo mengine yaliyosalia yanatarajia kuwa makavu huku maeneo ya Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini-Magharibi, Kusini mwa nchi na Pwani ya Kusini ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
“Izingatiwe kuwa pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa katika maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani, hali hiyo pia itajitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani,” alisema.
Aliongeza kuwa matukio ya vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo wa mvua nchini.
“Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa zaidi na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, magharibi mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani,” alisema.

Mtoto wa miaka 2 aua mama yake nchini Marekani.

Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa mtoto mmoja mdogo mvulana wa miaka miwili amempiga risasi kimakosa mama yake mzazi na kumuua ndani ya duka moja kubwa la uuzaji bidhaa la Wal-Mart.
Maafisa wa usalama wanasema bunduki iliyotumika iliyokuwa imefichwa ilichomoka wakati mvulana huyo alipokaribia na kuligusa begi la mkononi la mama yake mwenye umri wa miaka 29.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Hayden, katika jimbo la Idaho.
Msemaji wa Kaunti hiyo anasema mwanamke huyo alikuwa na kibali cha kumiliki silaha.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2014, MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, D’SALAAM


unnamed Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Mmeta Manyala. unnamed1Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza. unnamed2 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) mara baada ya kutoa hotuba fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015. unnamed3 Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu Watumishi wenzao ambao wametangulia mbele ya haki kwa mwaka huu 2014.
………………………………………………………………………………..
Na Inspekta Lucas Mboje, Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza nchini kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika utendaji wao wa kazi za kila siku ili kuleta ufanisi kazini.
Kamishna Jenerali John Minja ameyasema hayo leo wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka 2015 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Magereza Mkoa wa D’Salaam.
Aidha, amewataka Maofisa, Askari na Watumishi wote kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea bali wawe wabunifu kwa kutumia raslimali zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo.
” Kila mmoja wenu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi kwa bidii, ari na moyo wa kujituma ili kuliwezesha Jeshi kupata ufanisi unaotarajiwa”. Alisisitiza Jenerali Minja.
Wakati huo huo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja pia ametumia fursa hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa Mwaka uliopita 2014 ambapo Jeshi la Magereza limepata jumla ya leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama vile chokaa, mawe, kokoto, mchanga na Murram katika maeneo mbalimbali ya magereza ambayo ni Gereza Wazo Hill – D’Salaam, Gereza Msalato – Dodoma, Kambi Bahi – Dodoma, Gereza Maweni – Tanga, Gereza Lilungu – Mtwara, Gereza Butimba – Mwanza na Gereza Kalilankulukulu – Katavi. Leseni hizo zitatumika kuingia ubia na wawekezaji wenye nia ya kushirikiana na Jeshi katika uchimbaji wa madini.
Pili, Shirika la Magereza limeeingia Mkataba wa ubia na Kiwanda cha Saruji Wazo (Twiga Cement) katika uchimbaji wa madini ya ujenzi Gereza Wazo Hill. Aidha, Kiwanda hicho katika kutekeleza wajibu kwa jamii wametoa msaada wa mifuko ya saruji 1200 na Tzs.100, 000, 000.00 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Gereza Wazo Hill. Pia Shirika la Magereza limeingia makubaliano na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa vituo vya biashara (business malls) kwenye maeneo ya Gereza Kihonda, Morogoro na Gereza Karanga, Moshi. Tatu, Rasimu ya kwanza ya Sera ya Taifa ya magereza imekamilika na tayari imewasilishwa kwenye mamlaka za juu kwa hatua zaidi. Kukamilika kwa sera hiyo kutawezesha Jeshi kutekeleza Mpango Mkakati wa Sera na Maboresho ya Jeshi kwa ujumla.
Pamoja na Mafanikio hayo, Kamishna Jenerali Minja ameelezea maeneo yatakayopewa kipaumbele kwa Mwaka huu wa 2015 ikiwemo Jeshi litaendeleza jitihada za kuimarisha na kuongeza uzalishaji kwenye miradi mbalimbali ya Jeshi la Magereza. Jitihada hizi ni pamoja kutangaza fursa zilizopo ili kuwavutia wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi waje kuingia ubia katika miradi hiyo kwa kuleta mitaji na teknolojia, pia Kuendeleza mikakati ya kupunguza msongamano magerezani
Baraza la kufunga Mwaka na kuukaribisha Mwaka unaofuata ni utamaduni wa siku nyingi ambao unaenziwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Magereza. Baraza la aina hii hufanyika kila Mwaka ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini hupata fursa ya kuongea na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini kupitia Baraza hilo lengo ikiwa ni kufanya tathmini ya yale yaliyojiri katika Jeshi kwa kipindi cha Mwaka unaisha kwa kuzungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza na kutazama matarajio ya Mwaka mpya.