
Bibi kizee mmoja huko mkoani Mbeya ambae jina lake halikuweza kufaamika 
mara moja, amekutwa ameanguka nje ya kanisa akiwa uchi wa mnyama kwa 
kile kilichodaiwa alikuwa anawanga.
Kikongwe huyo alionekana ni mwenye kuishiwa nguvu pia kuhema sana, 
alipozinduka alijikuta amezingirwa na watu asubuhi huku akiwa ni mwenye 
woga wa wingi wa watu hao. Katika kumuhoji haraka haraka alieleza kuwa 
alikuwa anasafiri safari zake za usiku kutokea mkoani Morogoro kuelekea 
Ruvuma na alipopita maeneo hayo ya kanisa alijikuta anavutwa na kitu 
asichokijua ndipo kukapelekea kuanguka kwake.
Watu wa maeneo ya bibi huyo alipoanguka hawakuweza kumtambua na 
kuonekana hakuwa anaishi hapo ndipo walipomuuliza anakotoka na akajibu 
kuwa anatokea mkoani Morogoro na alikuwa anaenda Ruvuma kikazi yaani 
kazi zake za kishirikina.
Tukio la wachawi kuanguka karibu na maeneo ya makanisa mkoa wa Mbeya 
hutokea mara kwa mara na hivi inajiidhirisha kuwa nguvu za giza 
zinazotawala maeneo mbalimbali mbele ya mungu hufifishwa kama 
yaliyomkuta kikongwe huyu.
No comments:
Post a Comment