Waziri
 mkuu nchini Malaysia amesitisha ziara yake nchini Marekani na kurejea 
nyumbani kuweza kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na janga la mafuriko 
mabaya tangu miaka kumi iliyopita.
Uamuzi huo wa Najib Razak 
unafanyika baada ya shutuma dhidi ya serikali kwa kukosa kutangaza hali 
ya hatari kwenye majimbo matano yaliyo kaskazini mashariki mwa nchi.
Kupanda kwa haraka kwa viwango vya maji kumewalazimu zaidi ya watu 100,000 kuhama makwao.
Watu watano waliuwa.
Mvua zaidi inatarajiwa kunyesha katika maeneo ya kusini mwa nchi saa zinazokuja.
Bwana Razak alishutumiwa baada ya picha zake alizokuwa akicheza gofu na rais wa Marekani Barack Obama kusambaa mitandaoni.


No comments:
Post a Comment