TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 3, 2015

PUNGUZO LA BEI ZA HOSTELI KWA WANAFUNZI, ZIPO KIJITONYAMA DAR ES SALAAM, NI OFA KWA 2015. INTA QUALITY HOSTELS (KWA KAKA EMMA)



Na:Mwandishi wetu
Kampuni ya Inter Quality Traders ya jijini Dar es Salaam,na ambayo inamilikiwa na Mzalendo wa Kitanzania, Emmanuel Elisante, imetoa OFA YA PUNGUZO LA BEI  ZA HOSTELI ZILIZOPO KIJITONYAMA DAR ES SALAAM, kwa wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza kulipia kuanzia miezi 4 na kuendelea tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni kuanzia miezi 8.
MKURUGENZI MKUU wa  Inter Quality Traders, Bwana Emmanuel Elisante,  amesema kuwa ofa hizo ni kwa Wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza, kwa lengo la kuwapa unafuu wa maisha wakati wakiendelea kujipanga, “Hostel ni za kisasa na kwa Bei Nafuu kabisa, kama zilivyo ni tofauti na Huduma za Hosteli zingine, maeneo ni mazuri Sinza Mori, Nyuma ya Jengo la Sayansi na Teknolojia na pia Barabara ya Mapambano  Kijitonyama, kwa mwaka huu kutokana na changamoto zinazotukabili na kulikabili Taifa, nimeamua kuchukua uzalendo kwanza wa kuwajali wanafunzi,natoa ofa kwa wale wote wanaoingia kwa mara ya kwanza kulipia ada ya miezi 4 badala ya miezi 8, lakini pia baada ya kukaa na kuzungumza na wanafunzi waliopo, pamoja na mambo mengine ya huduma za hostel walihitaji pia kuweza kuunda timu zao na kuwa na Jezi ili wawe na timu itakayokuwa ikicheza na timu mbali mbali.
Hosteli hizo zinakidhi Mahitaji ya Wasomi hususani wa Vyuo mbali mbali kwa kuwa HOSTELI hizo zinapatikana Maeneo ya Karibu na Barabara kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupata Usafiri kwa Urahisi na kuongeza kuwa Tatizo la Usafiri kwenye Hosteli hizo hakuna.
Lakini katika Hizo HOSTELI hakuna tatizo la Maji, Hakuna tatizo la Umeme kutokana na kuwepo kwa mitambo ya Maji pia Generator kubwa kwa ajili ya kusaidia pale Umeme unapokuwa na tatizo.
Akizungumza na waandishi waliofika kukagua Hosteli hizo Elisante, alisema kuwa dhumuni la kuanzisha hizo HOSTELI inatokana na changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi wa USTAWI wa Jamii, Chuo cha Ardhi, Royal College, Kilimanjaro College Kwa Mama Ngoma, Chuo cha Kodi (ITA), CBE,  na wengine wengi wanaosoma kwenye maeneo ya JIJI la Dar es Salaam kuwa na hitaji hilo.
“Hizi Hosteli kama mnavyoona wenyewe ni salama kwa Usalama wa Wanafunzi wanaoishi hapa, Ulinzi ni wa Uhakika kama mnavyoona, na pamoja na yote tunatambua Umuhimu wa Umeme na Maji kwa hawa wasomi, kwa hiyo masuala hayo tumeyajengea Misingi Imara ya kuhakikisha kwa miaka 8 iliyopita na kwamba wakati wote mahitaji hayo yanakuwapo, lakini pia nimetoa Punguzo la Bei kwa Mwaka huu 2015 kwa kuwa ni mwaka wa upanuzi mkubwa wa hosteli zetu, kwa hiyo nimeamua wateja wetu washiriki baraka hii kwa kuwapa Punguzo Vijana wetu ili waweze kutumia mwanya huo kujipanga vizuri kwa lengo la kukabiliana na Elimu na mafanikio kimaisha kwa ujumla.
Hosteli hizo ambazo ni za kwanza kuwa na Mfumo wa ushirikishwaji wa pamoja katika Michezo, wanafunzi kwa jinsia zao wameunda timu za michezo kwa lengo la kuwa na timu zao zitakazokuwa zinashiriki michezo mbali mbali kwa lengo la kuwafanya wanafunzi kukutana kati yao na wadau mbali mbali.
Pia tumeamua kuwa na timu zetu za michezo kwa wanafunzi wanaoishi hapa, kwa kuwa ni wengi itakuwa ni jambo zuri maana lengo ni wao waishi kama wanafunzi wa chuo kimoja ama watoto wa baba mmoja, na hii itawaunganisha vizuri na kuwapa nguvu na akili zaidi.
Kuhusu vyumba kwenye Hosteli hizo zimegawanywa kutokana na wahitaji wenyewe, kuna vyumba vya watu wane yaani vitanda double 2 na  watu 6, vitanda double 3, vyenye nafasi kubwa kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kujisomea.
Jambo lingine ni uwepo wa Mazingira ya kujisomea yaliyotengenezwa mahususi kukidhi haja za wasomi hao, ambapo kuna Jukwaa kwa ajili ya kusomea usiku na wakati wote bila bughuza yoyote.
Chakula pia kinapatikana kwa bei nafuuu maeneo yote ya hizo hosteli kutegemeana na hitaji la mwanafunzi na chakula anachopenda kutumia kwa wakati huo.
Hosteli hizo zinakidhi mahitaji ya wanafunzi mbali mbali wa jiji la Dar es Salaam, kwa Maana Usafiri wa kutoka maeneo hayo ni mwingi na wa haraka kumwezesha mwanafunzi kuwahi Masomo popote Pale.
Kwa Mawasiliano kuhusu hizo Hosteli tupigie namba hizi hapa. +255-713-276982/+255784125433/+255715301794/+255-767-869133. WOTE MNAKARIBISHWA.

No comments:

Post a Comment