Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix 
Ntibenda wa pili kulia akikabidhi hundi  ya shilingi milioni 17na laki 
tano kwa wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market 
wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vijago jijini walizo kopa kwa 
ajili ya kufanya biashara kabla wa soko lya kunguliwa na soko hilo 
mapema mwezi uliopita
Meneja wa  taasisi hiyo Baraka Jekonea akiongea na vyombo vya habari
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda akiongea katika halfa hiyo
=======================================================
 Na:Pamela Mollel 
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda ameipongeza taasisi 
inayotoa huduma za kifedha (FINCA)kwa kuwafutia  zaidi ya milioni 30 
wanachama 35  wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market 
wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vinyago hela walizo kopa kwa 
ajili ya kufanya biashara kabla ya soko loa kunguliwa  mapema mwezi 
uliopita.
Ntibenda alisema  hayo jana wakati akikabidhi hundi  ya 
shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali hao  mbele ya 
waandishi wa habari iliyofanyika eneeo la soko hilo lililoko wilaya ya 
arusha mkoa wa arusha.
Kwa upande wa meneja  taasisi hiyo Baraka Jekonea alisema 
kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuendeleza ujenzi wa  soko hilo I 
benki hiyo in warudi katika hali yao ya zamahi ya biashara .
“Sisikama Taasisi ya Kifedha Finca tumeamua kuwasaidia ili 
tuweze kuwanusuru wahanga hawa kwa janga walilolipata tunaimani kwamba 
watarejea katika hali yao ya zamani kwani tangu wakumbane na changamoto 
hiyo maisha yao yamekuwa magumu sana”alisema Jekonea
Pia alitoa wito kwa 
wafanyabiashara ambao hawajajiunga na taasisi hiyo kufanya hivyo kwa 
kuwa benki hiyo inajali wajasiriamali na kuwataka kujiunga na taasisi ya
 mikopo ili kuweza kupata mikopo ya nafuu.
Kwa upande wake Kaimu 
Mwenyekiti wa soko hilo Hamis Juma alishukuru taasisi kwani pesa hiyo 
itawasaidia sana sana katika kujikwamua na kurejesha hali yao ya awali 
katika biashara yao.
Hata hivyo kabla ya 
msaada   huo walijichangisha kiasi cha shilingili laki nane kwa kila 
muhanga nakufanikiwa kukusanya shilingi milioni mia mbili iliyowasaidi 
kuanza ujenzi wa soko hilo.
Aidha mwenyekiti huyo 
ameomba taasisi nyingine ili kuweza kuwasaidia kuwapatia mitaji ili 
kuweza kuanza upya tena biahsra hiyo ya uuzaji wa vinyago.
No comments:
Post a Comment