Kufuatia
 kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At 
,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya
 ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana 
ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo 
moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka 
serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika 
ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa 
imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini 
Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji 
wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la 
utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha 
nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari 
uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka 
bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria 
ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo 
walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye 
askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini 
iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia 
Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa
 ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya 
shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.

No comments:
Post a Comment