Mbunge wa Singida Kaskazini, 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania 
Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo
 wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo 
endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine 
watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila 
atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka 
hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa 
Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia 
kwenye kinyang’anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba 
amekwishafanyakazi zilizotukuka.
“Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni
 nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa 
kazi zetu kwa moto”, alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na 
wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, 
kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa 
tiketi ya CCM”, alisema.
Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra 
mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika 
maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.

No comments:
Post a Comment