Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali Mkoani Arusha Imewataka
 wakazi wa Mkoa huo Kuhakikisha kuwa wanaendelea kudumisha Amani,Umoja 
na Mshikamano sanjari na kujitolea katika kufanikisha shughuli za 
kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na katibu Tawala wa mkoa huu Addo Mapunda wakati akiongea na wanahabari  ofisini kwake ambapo alisisitiza
wakazi wa mkoa huu  kufuata sheria kanuni na taratibu za nchi ikwemo usafi wa mazingira.
Aliwatahadharisha wananchi hao 
kutofuata mkumbo na kujihusisha na ushabiki wa baadhi ya vyama vya siasa
 ambavyo vimekuwa vikiendesha siasa za chuki,udini na uhasama jambo 
ambalo limekuwa likiwagawa wananchi katika makundi na kupelekea uwepo wa
 vitendo vya uvunjifu wa amani.
“napenda kuwakukumbusha wananchi
 wa mkoa wa Arusha kuwa suala la maendeleo sio la Serikali pekee bali ni
 jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa nashiriki kikamilifu katika 
shughuli za kujiletea maendeleo”alisema Mapunda.
Akizungumzia shule za Sekondari 
za Kata amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu na tayari umaliziaji
 wa majengo ya maabara na vyumba vya madarasa uko katika hatua za mwisho
 kabisa kukamilika na kuwataka wananchi kuepukana na dhana potofu kuwa 
shule za Kata hazina viwango vizuri vya ufaulu wa wanafunzi.
Mapunda amesema kuwa Mkoa wake 
umejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi hata mmoja 
aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani ambaye atakosa 
kujiunga na shule kwa uhaba wa vyumba vya madarasa kwani mkoa umejipanga
 kikamilifu kukabiliana na changamoto hiyo.
Kuhusu suala la uchaguzi  wa 
serikali za mitaa alisema kuwa anashukuru uchaguzi huo umekwenda kwa 
mafanikio na kuwa wananchi walipewa fursa zxa kuwachaguwa viongozi 
wanaowataka.
“Kikubwa ni wananchi kupewa fursa za kuwachagua viongozi 
wanowataka bila ya kuwepo 
shinikizo hali ambayo imekuwa ikichangia uvunjifu wa Amani ndio maana 
umeona mkoa huu hauna matukio ya uvunjifu wa amani kama ilivyokuwa 
kabla”

No comments:
Post a Comment