Kaimu
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. 
Elisante Olegabriel aliyesimama akifungua Mkutano Baadhi ya wasambazaji 
wa Filamu nchini (hawapo pichani)kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu, wa
 pili kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bi. 
Joyce Fissoo.Mkutano huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam(Picha na 
Benjamin Sawe)
 Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel
 (hayupo pichani) akifungua Mkutano wa wasambazaji wa Filamu nchini 
kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar 
es Salaam.
Katibu
 Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo aliyasimama 
akifafanua jambo kwa wadau wa usambazaji wa Filamu nchini wakati wa 
Mkutano wa Baina yao na Serikali uliofanyika jijini Dar es 
Salaam,wakwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel na wa kwanza kushoto ni 
Kaimu Mwanasheria wa Wizara Bw. Patrick Kipangula.
=========================================
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imewapongeza wasambazaji 
na wadau wa filamu nchini kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha, 
kuhabarisha na kufundisha maadili ya mtanzania huku wakichangia katika 
pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua 
mkutano wa serikali na wasambazaji wa filamu nchini jana jijini Dar es 
Salaam kujadili uporomokaji wa bidhaa za filamu nchini. 
“Tunathamini sana kazi mnayoifanya, Serikali inawajali na ipo 
tayari kushirikiana nanyi kwa kazi nzuri mnayoifanya hivyo ni vema 
kufanya mkutano huu kuwa wa kisanyansi kwa kuangalia gharama mnazotumia 
kuandaa bidhaa za filamu ili kuweza kukua kibiashara na kukuza uchumi wa
 nchi” amesema Pro. Gabriel.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
 Bibi Joyce Fisoo amesema kuwa Bodi haitaruhusu bidhaa zilizo chini ya 
kiwango kupelekwa kwa watanzania kwa daraja la bei ya chini pamoja na 
soko huria kwani hakuna uhuria usio na mipaka.
Bibi Fisoo amesema kuwa wananchi 
siyo dust bin wanapaswa kupelekewa kazi bora na zenye hadhi kwani Bodi 
inahitaji kujiridhisha kuhusu viwango vya filamu hizo na kuheshimu fedha
 za watanzania kwa kuwauzia kazi bora zinazoendana na thamani ya fedha 
zao. 
Aidha Mwenyekiti wa wasambazaji wa bidhaa za filamu nchini Bw. 
Emmanuel Miamba amewataka wadau na wasambazaji wa filamu nchini kuwa 
wakweli, wazalendo, pasipo kuogopa kitu chochote na kuangalia maslai ya 
wasambazaji wote na kama wataona uwekezaji katika kazi za filamu haulipi
 basi wawekeze katika masuala mengine na sio kushusha bei kuua tasnia ya
 filamu nchini.
Naye Bw. Chacha Matula kutoka Jembe entertainment amewaomba 
wasambazaji kuwa na umoja na mshikamano utakaowawezesha kushirikiana kwa
 pamoja na serikali kusitisha uporomokaji wa bei za filamu na 
kuwadhibiti watu wanaotaka kuua kampuni za wasambazaji wadogo nchini.
No comments:
Post a Comment