Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
 na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu 
ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps 
Entertainment. 
wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei 
iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na 
itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika 
tasnia ya filamu. 
Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza
 kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka 
utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, 
Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na 
Biashara.
 IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

No comments:
Post a Comment