TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 30, 2014

Cprian Majura Musiba Jr anauliza Je? UNAZIJUA ...AHADI KUMI ZA MWANA TANU!…

  •  
    UNAZIJUA ...AHADI KUMI ZA MWANA TANU!…
    TANU ni chama kilichotuletea ukombozi kutoka kwa wakoloni na kila Mtanzania aliipenda Siasa hii chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere kwani ilijali utu, ilikuwa ikiwainua wanyonge na ililenga kulijenga Taifa katika misingi ya usawa, na ulipotakiwa kujiunga na chama hizi ndizo ahadi kumi ulizotakiwa kuziahidi ili utakapotenda kinyume cha hapo uchukuliwe hatua

    Ahadi kumi za mwana TANU zilikuwa kama ifuatavyo.

    i. Binadamu wote ni ndugu zangu na Dunia ni moja

    ii. Nitaitumikia nchi yangu na binadamu wenzangu wote kwa unyenyekevu na moyo wa upendo na huruma

    iii. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, maradhi, na dhuluma hapa nchini na duniani pote.

    iv. Rushwa ni adui wa haki, sitatatoa wala kupokea Rushwa.

    v. Cheo ni dhamana . sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

    vi. Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

    vii. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu na dunia yenye haki na amani.

    viii. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

    ix. Nitakuwa raia mwema wa Tanzania, Afrika na Dunia nzima.

    x. Nitakuwa mtii kwa Raisi na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Ulitakiwa kuapa hivyo unapojiunga na chama, hali hii ilipelekea watu hawa kuwa na uzalendo wa kweli walilipenda Taifa na walijitolea kwa dhati kulitumikia, swali la kujiuliza ni je ?

    Ni commitment gani tunayoiweka tunapojiunga na vyama vya siasa leo!!!

No comments:

Post a Comment