Mkurugenzi
 wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza(kushoto) akimkabidhi Jezi Rais
 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kwaajili 
ya Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa 
Women Cup yanayotarajiwa kutimbua vumbi tarehe 1 January 2015.
Na Josephat Lukaza – Lukaza Blog
Mkurugenzi
 wa makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza amkabidhi jezi Rais wa TFF, Mh
 Jamal Malinzi kwaajili ya michuano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake 
yajulikanayo kama Taifa Women Cup ambayo yanatarajiwa kutimua Vumbi 
tarehe 1 Januari 2015 huku Mechi ya Uzinduzi ikiwakutanisha timu kutoka 
Mwanza na Musoma mechi ambayo itapigwa katika Dimba la CCM Kirumba, 
Jijini Mwanza.
Kampuni
 ya Proin Ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya ambayo yanatarijiwa 
kutimua Vumbi Mnamo tarehe 1 Januari 2015. Proin Imeamua kudhamini 
mashindano hayo kwa lengo la Kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa 
Wanawake ambapo baadae wachezaji bora wataweza kuingia katika Timu ya 
Taifa ya Wanawake.
Vilevile
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mh Jamal Malinzi 
amewataka pia makampuni mengine Kujitokeza katika Kudhamini Mashindano 
haya yanayotarajiwa kuanza tarehe 1 Januari 2015 kwa lengo la Kuweza 
kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake huku pia wakipata fursa ya
 Kujitangaza kibiashara kwasababu mpira wa miguu ni mchezo ambao 
unapendwa sana na watu wengi hivyo ni dhahiri kabisa Kuwa Makampuni 
mengi yakidhamini mashindano haya yataweza kufikia malengo yao kwa 
kujitangaza.
No comments:
Post a Comment