Na Andrew Chale
USIKU wa Old is Gold taarab  
unatarajiwa kurindima ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, 
kwa wadau kupata burudani ya muziki wa mwambao wa kizamani.
Kwa mujibu wa waandaji wa usiku 
huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin  alieleza kuwa  
ni kila Jumapili  ndani ya ukumbi huo utakuwa na burudani ya kipekee kwa
 nyimbo za mwambao pamoja na ‘surprise’ mbalimbali kwa watakaofika hapo.
“Kila jumapili  kwa kiingilio 
cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao  watashuhudia shoo ya 
Usiku wa Old is Gold ndani ya Safari Carnival” Alisema Asia Idarous
Aliongeza kuwa, mbali na 
burudani ya taarab za zamani  pia kutakuwa na ‘Surprise’ mbalimbali” kwa
 wadau watakaojitokeza kwenye usiku huo.
Aidha,  Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na  Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds
fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo.

No comments:
Post a Comment