Kijana
 mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja,  usiku wa 
kuamkia leo amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati 
akiingia Club Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam. 
Tukio
 hilo lilitokea majira ya saa tano(5) usiku  ambapo kijana huyu akiwa na
 rafiki zake wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliyokuja 
nayo, walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye kupigwa
 risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana. 
Shuhuda
 wa tukio hilo alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye gari ndogo
 nyeusi ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa mwendo kasi 
sana, kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye gari ilikuwa 
imepaki muda mfupi baada ya kufika eneo hilo.
 shuhuda
 huyo aliendelea kwa kusema alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia 
"pyuuu!!!" bila ya kuelewa ni nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi 
za watu hao waliokuwa wamevamiwa. 
Waliotenda
 tukio hilo walitoweka mara moja eneo la tukio baada ya watu kujaa eneo 
ambalo kijana huyo alipigwa risasi alikuwa ameanguka chini. 
Polisi
 walifika eneo la tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na damu 
nyingi zikiwa zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa 
amewekewa nguo shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana 
ilikuwa ikitoka nyingi sana.
 Walimpakia
 kwenye gari yao kumuwahisha katika hospitali ya jirani ya mwananyamala,
 lakini kijana huyo alifia njiani akikimbizwa kuelekea hospitali
No comments:
Post a Comment