Meneja
 wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa kuna kampeni 
zinaendelea kuwashawishi waamuzi kutoa mamuzi tofauti dhidi ya timu 
yake.
Mourinho amekasirishwa na mwamuzi Anthony Taylor kwa 
kushindwa kutoa penati katika mchezo dhidi ya Southampton ulomalizika 
kwa sare ya bao 1-1.
Kiungo Cesc Fabregas alipewa kadi ya njano 
baada ya kuanguka katika eneo la hatari la Southampton, kwa kukwatuliwa 
na Matt Target na kuoneka na kama amemuhadaa mwamuzi kwa kujiangusha.
Baada
 ya mchezo huo Mourinho alilamika kuwa vyombo vya habari, watangazaji 
mameneja wa timu zingine wote wanatoa shinikizo kwa waamuzi hivyo 
anadhani kuna kampeni inaoendelea dhidi ya timu yake.
"Sijui kwa nini kuna kampeni inaendelea dhidi ya timu yangu ila sijali,kila mtu anajua ile ilikua ni penati."
Mourinho anafahamika Zaidi kwa kwa kauli zake tata ambazo amekua akizitoa mbele ya waandishi wa habari.

No comments:
Post a Comment