Mwenyekiti
 wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Mohd Zidi akifafanua jambo katika
 mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya siku ya 
Mazoezi Kitaifa 01/01/2015 yatakayo fanyika Uwanja wa Amaan 
Zanzibar,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dk Ali 
Mohd Shein,na Ujumbe wa Mwaka huu ni Fanya Mazoezi Imarisha Afya yako 
Epuka Maradhi yasioambukiza.
Muandishi
 wa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza maswali kwa 
Katibu Mtendaji wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Ameri Mohd Makame 
kuhusiana na Maadhimisho ya siku ya mazoezi Kitaifa ambayo yatafanyika 
kwa mara ya kwanza 01/01/2015 Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Muandishi
 wa Habari kutoka Chuchu FM Radio Yahya Saleh akiuliza maswali kwa 
Katibu Mtendaji wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Ameri Mohd Makame 
kuhusiana na Maadhimisho ya siku ya mazoezi Kitaifa ambayo yatafanyika 
kwa mara ya kwanza 01/01/2015 Uwanja wa Amaan Zanzibar.
-Katibu
 Mtendaji wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Amer Mohamed Makame 
akielezea madhumuni ya kufanyika kwa Tamasha la kwanza la siku ya 
mazoezi 01/01/2015 katika ukumbi wa Wizara ya habari Utamaduni Utalii na
 Michezo alipokutana na Waandishi wa Habari Zanzibar. 
Mwenyekiti
 wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Mohd Zidi akifafanua jambo katika
 mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya siku ya 
Mazoezi Kitaifa 01/01/2015 yatakayo fanyika Uwanja wa Amaan 
Zanzibar,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dk Ali 
Mohd Shein,na Ujumbe wa Mwaka huu ni Fanya Mazoezi Imarisha Afya yako 
Epuka Maradhi yasioambukiza.
Na Abdulla Ali-Maelezo Zanzibar
Chama cha mchezo wa mazoezi ya 
viungo Zanzibar (ZABESA) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni 
Utalii na Michezo kimeandaa maadhimisho ya siku ya mazoezi ya kitaifa 
yatakayofanyika Januari 1 mwaka 2015 katika uwanja wa Amani.
Maadhimisho hayo yatakayofanyika 
majira ya Asubuhi yatahudhuriwa na watu mbalimbali ambapo Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Moh’d Shein 
anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari
 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Kikwajuni mjini Zanzibar, Katibu 
mtendaji wa ZABESA Ameir Mohammed Makame amesema maadhimisho hayo 
yatafuatiwa na matembezi yatakayoanzia Uwanja wa Tumbaku, Miembeni 
kupitia Ng’ambu stesheni, Mfereji wa wima, Mikunguni na kumalizia uwanja
 wa Amani.
Amesema lengo la maadhimisho hayo 
ni kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi, kwani ni muhimu kwa mwanadamu
 kimwili na kiakili na husaidia kuimarisha afya zao kwa ujumla.
Akitaja miongoni mwa faida hizo 
katibu huyo amesema ni pamoja na kutanua mifumo ya mishipa ya damu, 
kupunguza mafuta na sukari iliyozidi mwilini na kuimarisha misuli yote 
ya mwili.
“Vyakula tunavyokula mara nyingi 
vinakua havina ubora kwani vinakua na mafuta mengi na kemikali na 
kusababisha matatizo mengi kiafya ikiwemo maradhi ya shindikizo la damu,
 kensa, uzito uliokithiri na mengne mbalimbali” amesema Katibu Ameir.
Aidha alisema matumizi ya 
teknolojia na kukua kwa uchumi kumesababisha watu kukaa kitako kwa muda 
mrefu kuangalia television, kutopenda kutembea na matumizi holela ya 
vyombo vya usafiri hupelekea kupata maradhi yasiyoambukiza kama vile 
presha na kisukari.
Katika shamrashamra ya maadhimisho
 hayo Vilabu vya mazoezi zaidi ya 70 kutoka Tanzania Bara na Visiwani 
vinatarajiwa kuungana pamoja katika maadhimisho hayo.
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed 
Shein ameiasisi Januari mosi kuwa siku ya mazoezi ya kitaifa Zanzibar 
ambapo Wananchi hujumuika na kufanya mazoezi mbalimbali ya Viungo 
ikiwemo kutembea na kukimbia.
Kikundi cha ZABESA kilianzishwa 
rasmi mwaka 2010 na kusajiliwa na mrajisi mkuu wa Serikali ya Mapinduzi 
Zanzibar ambapo ujumbe wa mwaka huu ni;“Fanya mazoezi, imarisha afya 
yako na epuka maradhi yasiyo ya kuambukiza”.
No comments:
Post a Comment