
 Baadhi
 ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya
 Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya 
namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo 
Tunduma.

 Mkuu
 wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa 
wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la 
Tunduma.

 Baadhi
 ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya
 Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya 
namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo 
Tunduma.

 Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo.
BENKI ya Posta Tanzania (TPB), 
Tawi la Tunduma imetoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Tunduma, wilayani 
Momba. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 100, ililenga
 kuwaelimisha wafanyabiashara hao kuhusu matumiza mazuri ya huduma za 
kibenki, hususan mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Akifungua semina hiyo, Mkuu wa 
Wilaya ya Momba Abiudy Saideya, aliipongeza Benki ya Posta kwa kutoa 
mafunzo ambayo alisema yanawasaidia wafanyabiashara wa Tunduma kukuza 
uelewa wa matumizi sahihi ya huduma zinazotolewa na taasisi za fedha.
Aliwashauri wafanyabiashara 
wachukue mikopo ili kukuza mitaji yao na kuongeza uzalishaji, lakini 
bila kuwa na elimu sahihi juu ya matumizi ya mikopo hiyo faida yake 
inaweza isipatikane. “Nawashauri wafanyabiashara mnaohudhuria semina hii
 kutimia fursa hii kujadiliana na benki ya Posta ili mfikie muafaka 
katika huduma mnazozitaka,” alisema Mkuu wa Wilaya hiyo.
Aidha aliwaasa wafanyabiashara 
kujiepusha na biashara haramu zitokanazo na bidhaa haramu zilizozagaa 
mpakani mwa wilaya yao, kwani kufanya hivyo bishara zao zinaweza 
kutaifishwa na hivyo kupoteza mitaji yao bila kujua.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa 
Mikopo wa Benki ya Posta, Henry Bwogi iliwasisitiza wafanyabiashara hao 
kutembelea tawi la benki hiyo lililopo Tunduma ili kujipatia huduma zote
 za kibenki hususan mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji yao. Pamoja na
 hayo aliongeza kuwa benki ya TPB inatoa mikopo ya aina nyingi, kuanzia 
ile ya vikundi hadi ya wafanyabiashara wakubwa, huku riba zinazotozwa na
 benki hiyo ni nafuu sana.
No comments:
Post a Comment