Wagonjwa wadaiwa kunyanyaswa kingono katika hospitali za Uingereza.
Mlipuko wa kisiri wa unyanyasaji wa 
kingono katika hospitali za Uingereza umegunduliwa huku takwimu mpya 
zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600 yaliripotiwa kwa polisi katika 
kipindi cha miaka mitatu iliopita.
Kumbukumbu zilizopatikana na gazeti la 
The Guardian chini ya sheria ya uhuru wa habari zinaonyesha ongezeko la 
asilimia 50 ya ripoti za unyanyasaji wa kingono kwa kutumia nguvu katika
 hospitali tangu mwaka 2011.
Unyanyasaji huo unashirikisha visa 157 
vya ubakaji.Takwimu za unyanyasaji huo katika hospitali zilitolewa na 
vituo 38 vya polisi kati ya vituo 45 nchini Uingereza.
Wagonjwa hospitaliniRipoti hiyo inadai kuwa mashambulizi 1,615 yanayojulikana yanafanyika katika kliniki za kibinafsi,na vituo vyengine vya afya.
Wagonjwa hospitaliniRipoti hiyo inadai kuwa mashambulizi 1,615 yanayojulikana yanafanyika katika kliniki za kibinafsi,na vituo vyengine vya afya.
Lakini viongozi wa mashtaka wanasema 
kuwa hadi asilimia 90 ya visa vya unyanyasaji haviripotiwi swala 
linaloonyesha kwamba takwimu za ukweli huenda ziko juu zaidi.
No comments:
Post a Comment