Mahakama
 moja ya Misri imepunguza hukumu ya watu wanane waliodaiwa kushiriki 
katika ndoa ya watu wa jinsia moja kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja.
Mwezi Uliopita ,wanane hao walipatikana na hatia ya kuchochea uasherati.
Walishtakiwa
 baada ya kanda moja ya video kusambaa katika mitandao ikiwaonyesha 
wakisherehekea katika boti moja lililokuwa mto Nile huku wanaume wawili 
wakionekana wakivalishana pete na kukumbatiana.
Watu hao baadaye walikataa kwamba ilikuwa harusi ya watu wa jinsia moja.
Ushoga ni kinyume na utamaduni wa Misri ,ijapokuwa si kinyume na sheria.
Wanaharakati
 wa kupigania haki za kibinaadamu wanasema kuwa kampeni dhidi ya mashoga
 imeimarishwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni nchini Misri.

No comments:
Post a Comment