TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 3, 2015

SHULE YA MSINGI KIBINDU HATARINI KUFUNGIWA ,MBUNGE,DIWANI WAHAHA KUMSAKA MKURUGENZI

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
SHULE ya msingi Kibindu,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,ipo hatarini kufungiwa kutokana na vyumba vya madarasa kuanguka na miundombinu yake kuwa chakavu hivyo kuhofiwa kuhatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.
Aidha shule hiyo imekuwa ikiezuliwa baadhi ya majengo yake mara kwa mara kutokana na kutofanyiwa ukarabati tangu shule hiyo ijengwe zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi wa shule hiyo wanakabiliwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa vilivyo bora na imara hali inayosababisha wanafunzi 200 kulundikana katika chumba kimoja.
Akizungumzia hali hiyo mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae yupo katika ziara ya siku 10 jimboni humo akitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo shule hiyo ambayo baadhi ya majengo yake yameanguka ,alisema hayuko tayar kushuhudia wanafunzi wakiendelea kusoma katika mazingira ya hatari.

Ridhiwani alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya kukagua madarasa hayo na kushuhudia vyumba vinne vinavyotumika kuwa hatarini kubomoka kutokana na kutawaliwa na nyufa.
“Nimesikitishwa sana na ningekuwa  na uwezo ningeifunga hii shule isitumike kwani shule inafunguliwa tarehe 14 mwezi huu ,wanafunzi watakuja kusomea wapi ,wakati pia majengo yaliyobakia yanaweza kuanguka wakati wowowte pia,ni lazima juhudi za lazima zifanyike kuokoa maisha ya wanafunzi hawa” alisema Mbunge huyo.
Ridhiwani alisema kuwa atawsiliana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Ibrahim Matovu ili waone ni namna gani wataweza kuelekeza nguvu zao katika shule hiyo ili iwe katika mazingira bora .
Diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya alisema taarifa za uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo tayari amezifikisha ngazi ya halmashauri, ambapo nae kwa upande wake aliomba shule hiyo ifungiwe ili ukarabati ufanyike
Mtendaji wa kijiji Cha Kibindu Juma Mgaza, alisema shule hiyo ina matatizo ya kuezuliwa mara kwa mara wakati wa mvua kutokana na miundombinu yake kuwa chakavu.
Mgaza aliitaka  halmashauri ya wilaya hiyo kufanyia kazi changamoto hiyo kubwa ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi.
Shule ya msingi Kibindu kwa sasa ina wanafunzi 907 wa darasa la kwanza hadi la saba ambao wanatarajia kuanza mhula wa masomo kwa mwaka 2015 wiki ijayo huku ikiwa na vyumba vinne kati ya 14 vinavyohitajika.
Mbali ya hayo vyumba vya madarasa vimeanguka na vingine vimeweka nyufa kubwa ambazo zinahofiwa kuanguka wakati wowowte na kusababisha athari kwa wanafunzi na walimu.

No comments:

Post a Comment