Maafisa
 nchini Marekani wanasema kuwa mtoto mmoja mdogo mvulana wa miaka miwili
 amempiga risasi kimakosa mama yake mzazi na kumuua ndani ya duka moja 
kubwa la uuzaji bidhaa la Wal-Mart.
Maafisa wa usalama wanasema 
bunduki iliyotumika iliyokuwa imefichwa ilichomoka wakati mvulana huyo 
alipokaribia na kuligusa begi la mkononi la mama yake mwenye umri wa 
miaka 29.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Hayden, katika jimbo la Idaho.
Msemaji wa Kaunti hiyo anasema mwanamke huyo alikuwa na kibali cha kumiliki silaha.

No comments:
Post a Comment