Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu 
abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki
 kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kwneye ferry hiyo walipiga simu 
kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na 
upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani 
nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa 
umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe
 .
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.

No comments:
Post a Comment