Mbunge wa Jimbo la Chalinze, 
Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi 
Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana
 na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya
 kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri 
shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha 
maafa zaidi hadi itakapojengwa upya. 
  Mbunge wa Jimbo 
la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara 
katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi 
wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.
Watioto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji 
mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa 
Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya
 sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa 
hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la
 mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea mnara
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
Ridhiwani akihutubia mkutano wa 
hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi  
kuboresha barabara na mawasiliano ya simu
Ridhiwani Kikwete akisisitiza 
jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Kwa Mduma wakati wa ziara 
yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata ya Kibindu
No comments:
Post a Comment