Sheikh
 Shariff Matongo  akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake 
 jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)kuhusu  ndoto yake ambayo 
ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.
NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR.
Sheikh
 Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri
 kwa mashekh mbalimbali Duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi 
wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake 
alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba 
likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi
 nje ya nchi kwa kufanya kazi.
Alisema
 katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa  ambaye ameshika 
nyadhifa mbalimbali na  mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh
  alisema ndoto nyingine  kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi 
mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata 
mafanikio  makubwa kwa mwaka utaoanza kesho.
Vijana
 wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana hivyo 
wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa  itapita lakini kutakuwa na
 vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.
‘’Ndoto
 yangu  niliooteshwa sikukaa nayo peke yangu, niliweza kupata ushauri 
kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa  Abhu Dhabi,Mufti wa 
Nigeria  na wengine wote wakaniambia suala hilo nisikae 
nalo,niwashirikishe na Watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff 
Matongo.
Sheikh
 Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na 
bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.
Alisema
 ndoto hizo ni lazima kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa watu 
wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali 
ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment