Indonesia imesitisha utafutaji wa ndege ya AirAsia hadi kesho iliopotea
 na takriban abiria 160 waliokuwa wakielekea Singapore kutoka mji wa 
Surabaya nchini Indonesia.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na 
singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya 
Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
Takriban abiria 162 walikuwa wakiabiri ndege hiyo aina ya Airbus 320 wengi wao wakiwa raia wa Indonesia.
Rubani wa chombo hicho anadaiwa kutaka kubadilisha njia ili kuepuka kimbunga lakini hakuomba usaidizi wowote.
Baadhi ya meli katika eneo hilo zinaendelea kuitafuta ndege hiyo,licha ya hali mbaya ya hali ya anga
Familia
 na marafiki wa waathiriwa wamekongamana nchini Singapore na uwanje wa 
ndege wa surabaya wakingojea habari kuhusu ndege hiyo.


No comments:
Post a Comment