MWENYEKITI wa klabu wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, ameagiza Polisi ‘Marafiki’ kuwakomesha Baada ya
kumtimua kocha Mkuu wa timu yake
 na baada ya kubwaga chini sekretariati ya klabu hiyo, Mwenyekiti wa 
Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga) 
Bw, Yusuf manji, ameamua 
kuwafanyizia baadhi ya waliokuwa watumishi wa Klabu hiyo akiwemo Beno 
Njovu, Katibu Mkuu aliyepita. 
 Wakandamizwe haswa  kulingana na 
mawasiliano yaliyonaswa na makachero wetu kati ya Mwenyekiti huyo na 
viongozi wa juu wa Klabu hiyo, Manji amewapa maelekezo wanasheria wake 
na Sekretariati ya sasa kuwafungulia mashtaka Sekretariati iliyopita  
kwa madai  ya  ufujaji pesa, huku akiwataka viongozi hao kutumia 
‘marafiki’ zao waliooko katika jeshi la polisi ‘kuhakikisha 
wanashugulikiwa.
Katika mawasiliano hayo kupitia email ya tarehe 22 Desemba , 
Manji pia anamwagiza mtu 
aliyetambulika kuwa mhasibu  anayaenda kwa jina la Amit kugharamia 
‘maagizo hayo yote’, na kumpa taarifa kila siku. Vyombo vya habari 
kutumika Manji pia  ameagiza wafanyakazi hao wazamani ‘wachafuliwe’  
kupitia kampeni kali magazetini, huku akielekeza ‘Press Release’ yenye 
saini yake itolewe ikionesha ‘masikitiko
yake’.
Adhabu mbele, hukumu nyuma Huku 
akitoa maagizo wafanyakazi hao washugulikiwe ipasavyo na polisi 
‘marafiki’ zake, Bwana Manji ametupilia mbali haki za wafanyakazi hao 
kusikilizwa kukiwa hakuna uchunguzi wowote uliokwishafanyika kuhusu 
madai yake dhidi ya watumishi hao zaidi ya hisia zake mwenyewe na 
Sekretariati mpya inayotekeleza kila alitakalo bila kuhoji. 
Maagizo yazua mpasuko ndani ya kamati tendaji
Kufuatia maagizo ya Manji, mmoja wa watumishi wapya 
aliyetambulika kama Frank Chacha alitekeleza maamuzi hayo ambayo 
mwenyekiti huyo alikuwa amesema hayapingiki wala hayahojiki kwa email 
yake, huku wakifungua kesi katika kituo cha Polisi kati Dar es salaam na
 kufanikiwa kuweka wafanyakazi wawili ndani huku wakiendelea kumuwinda 
Beno Njovu  Lakini masaa  machache baada ya hatua hizo, kuna dalili kuwa
 baadhi ya viongozi ndani ya klabu hiyo wanapinga vikali hatua hizo za 
Manji na wametishia ‘kuaachia’ ngazi.
Mpasuko huo ndani ya Yanga umedhihirishwa na email kutoka kwa 
Bwana Omar, Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala akimjulisha Manji kuwa 
jana Jumanne, baada ya kutekeleza maagizo ya Mwenyekiti huyo alipokea 
simu kutoka kwa  Isaac Chanji, mjumbe wa
Kamati Tendaji akitishia kuwa  
hatua ambazo zilikuwa zimeshachukuliwa zilikuwa za hatari kwa Klabu hiyo
 na kuwa yeye Chanji na wajumbe wengine wengelazimika kuwaachia akina 
Omari na Chacha timu hiyo.
Kikosi kazi cha Fullshangwe 
kilipomtafuta Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji Simu yake ilikuwa 
ikiita bila majibu lakini hakikuishia hapo kilitafuta msemaji wa Klabu 
hiyo Bw. Jerry Muro ambaye alijibu kwamba kesi hiyo inawahusu 
wafanyakazi wa zamani wa Yanga hivyo yeye hawezi kuzungumzia zaidi 
lakini shauri hilo lileripotiwa polisi na baada ya uchunguzi wa poilisi 
taarifa rasmi kuhusu tuhuma zinazowakabili wafanyakaizi hao wa klabu ya 
Yangza wa zamani  itatolewa na jeshi hilo.
……………………………………………………………………….
Maswali Tata
Kufuatia hatua hii ya Manji mtu 
unaweza kujiuliza maswali kadhaa: Je kwa nini Yanga inakuwa na kesi kila
 wakati? Gharama za kesi hizi, ambazo nyingine siyo za lazima, si mzigo 
usiokuwa na faida kwa Yanga? Mara
wachezaji, makocha, na Sekretariati za nyuma. 
Ni dhahiri kuwa hata kama kesi 
hii ya sasa ina msingi wowote, basi uchunguzi ungetangulia. Lakini, 
labda kwa jeuri ya hela, Manji ameshawahukumu watumishi wale na ni wazi 
kuwa yuko tayari hata kupindisha sheria ili afikie lengo lake. Lengo la 
Manji hasa ni nini? Anajaribu kuwaadhibisha hawa watumishi kweli au ni 
kujenga hoja za Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo unaotegemewa kufanyika 
Januari 2015 kwa
kujenga mazingira ya kuwasahaulisha wanachama wa Yanga baadhi ya  ahadi alizotoa na ambazo hadi sasa
bado ni ahadi hewa  tu?

No comments:
Post a Comment