MAAFISA, ASKARI NA WATUMISHI RAIA WA JESHI LA MAGEREZA WAPATIWA MAFUNZO YA JINSIA, ROMBO GREEN VIEW HOTEL – JIJINI DAR ES SALAAM
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa 
hotuba fupi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Ufunguzi 
wa Mafunzo ya Jinsia kwa Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la 
Magereza, leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel. 
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho 
Desemba 30, 2014(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna 
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura(wa pili kulia) ni Mkuu
 wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, 
Augustino Mboje(kulia) ni Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi wa Magereza, 
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mbarak Semwenza. 
 Baadhi ya Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza 
wanaoshiriki Mafunzo ya Jinsia katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel 
wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku 
mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho Desemba 30, 2014. 
 Mshiriki wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Makao Makuu ya Magereza, Mkaguzi 
wa Magereza, Amina Lidenge akijitambulisha kabla ya Ufunguzi rasmi wa 
Mafunzo ya Jinsia. 
Mtoa
 Mada wa Kwanza kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Magreth 
Mussai akiwasilisha Mada yake kuhusiana na dhana ya Jinsia kama 
anavyoonekana katika picha. 
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma 
Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa, Askari na 
Watumishi raia wa Jeshi la Magereza(waliosimama) mara baada ya Ufunguzi 
rasmi wa Mafunzo ya Jinsia leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo 
Green View Hotel, (kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, 
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura, (wa pili 
kushoto) ni Mtoa Mada wa Kwanza kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na 
Watoto, Bi. Magreth Mussai(wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la 
Wanawake Kingolwila, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Luhembe, 
(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi 
wa Magereza, Augustino Mboje(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la 
Magereza). 
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment