Mjumbe
 wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini na
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi 
la Kilimahewa lililoko katika Kata ya Mwenge Ndugu Mohammed Madodo mara 
baada ya kuwasili katika Tawi hilo kwa ajili ya mkutano na viongozi wa 
Tawi tarehe 28,12.2014
Mke
 wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi 
Mjini Mama Salma Kikwete akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la 
Barabara ya Kawawa lililoko katika Kata ya Matopeni tarehe 28.12.2014.
Mke 
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha 
Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa Halmashauri ya Tawi
 la Kilimahewa huko Lindi Mjini wakati wa ziara yake ya kuyatembelea 
matawi ya CCM wilayani humo tarehe 28.12.2014.
Mke 
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma 
Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi 
Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai aliyemtembelea Mama Salma kwenye Ikulu 
ndogo huko Lindi tarehe 28.12.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI.  
……………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
29/12/2014 Mjumbe wa Halmashauri 
Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi 
mjini Mama Salma Kikwete amewataka vijana kuwa na msimamo na kutokubali 
kutumika katika vurugu zinazohatarisha amani na usalama wa nchi.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais
 Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati 
akifungua shina la  vijana wakeleketwa la kikundi cha Zahanati Kempu 
lililopo Kata ya Rasibura wilaya ya Lindi mjini.
Alisema vijana wengi hawajui 
Historia ya nchi hivyo basi baadhi ya watu wasio na nia njema wanaitumia
 nafasi hiyo kuwarubuni na kuwashawishi kufanya vurugu zinarudisha nyuma
 maendeleo ya eneo husika.
“Msikubali  mkoa wetu wa  Lindi 
kuwa kichaka cha   majaribio na kutumika katika vurugu, kuweni  na 
 msimamo  wa kuitetea amani yetu  kwani mkifanya vurugu matatizo 
yanapotokea ninyi ndiyo mnaoangamia na hao waliowashawishi 
wanawakimbia”. 
Kama atakuja mtu hapa na 
kuwashawishi  kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni sawa hakuna 
atakayezuia tunahitaji kuwa na maendeleo katika mkoa wetu, lakini 
kuwashawishi ili mfanye vurugu na kuharibu vichache tulivyonavyo 
msikubali”, alisema Mama Kikwete. 
Aidha MNEC huyo aliwasisitiza 
vijana kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili waweze kujiletea maendeleo
 yao na ya mkoa huo kwa kuwa vijana  ndiyo wanaotegemewa na ni nguvu 
kazi ya Taifa.
Akisoma taarifa ya kikundi hicho 
Hidaya Chivii ambaye ni Mtunza fedha alisema kikundi hicho kilianzishwa 
 tarehe 5/7/2014 kikiwa na  wanachama 23 kati ya hao wanaume ni 18 na 
wanawake ni watano.
Chivii alisema madhumuni ya 
kuanzishwa kwa kikundi hicho ambacho kinajihusisha na kazi ya kuendesha 
pikipiki  (bodoboda)  kwa upande wa wanaume na ususi kwa upande wa 
wanawake ni kujikwamua na hali ngumu ya maisha na kuweza kujiendeleza.
“Waendesha pikipiki  tunakabiliwa 
na changamoto ya kunyang’anywa pikipiki hasa ifikapo wakati wa uchaguzi 
kwani wamiliki walio wengi ni wanachama wa chama cha Wananchi (CUF)  na 
sisi ni wanachama wa CCM au wanatupa pikipiki zao kwa masharti magumu 
yakiwemo ya kukipigia kura chama chao”, alisema Chivii.
Alizitaja changamoto nyingine 
zinazowakabili kuwa ni  pamoja na kutokuwa na vitendea kazi vyao wenyewe
 na kutokupata mafunzo ya ujasiriamali.
Wakati huo huo Mama Kikwete 
 alifanya vikao na  viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM katika 
matawi ya Kilimahewa na barabara ya Kawawa  na kuwahimiza wajumbe 
 kuendelea  kushikamana na kuwa kitu kimoja ili waweze kufanya kazi zao 
kwa ufanisi zaidi.
Akiwa katika tawi la Kilimahewa 
lililopo Kata ya Mwenge aliwapokea vijana wanne kutoka chama cha 
Wananchi (CUF)  ambao walijiunga na CCM.
Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa 
NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini yupo wilayani humo  kwa ajili ya
 kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na 
viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.




No comments:
Post a Comment