Inspekta
 Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya 
makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama 
barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni
 mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa 
kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit 
Nsimeki  anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa 
kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa 
anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
Wengine
 ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) 
Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa 
Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda 
amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa 
kamanda wa Polisi  Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma 
amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi
 ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi 
 Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga 
anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa 
upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David 
Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa 
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma 
Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .
Aidha,
 aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi 
(SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa 
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela 
anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa 
upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi 
anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa
 upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na 
aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa 
Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum 
Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa 
Polisi (SP) Awadh Haji   anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa 
Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi 
ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke. 
Wengine
 ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James
 Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu 
wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe  Buzema anakwenda
 kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki 
Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi  (ASP) Prackson Kibogoyo 
anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa 
Trafiki Mkoa wa Njombe,   Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho 
Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.    
Mabadiliko
 hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi 
la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma 
bora ya usalama. 
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
No comments:
Post a Comment