-  ASEMA CCM HAIWEZI KUONDOA HOJA YAKE BUNGENI
 
- ASISITIZA MSIMAMO WAKE KWA WAPIGA KURA JIMBONI
 
Na Suleiman Abeid, Nzega 
 
   Mbunge
 wa Nzega mkoani Tabora ,Dkt.Hamisi Kig wangalla,amesema bado ana 
dhamira ya kuwasilisha hoja ya kumng’ oa madarakani Spika  wa B unge, Bi.Anne Makinda .Alisema uvumi ulioenea kuwa hoja yake imeondolewa kwa agizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), hauna ukweli
. 
 Dkt. Kigwangalla aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa 
hadhara ulioshirikisha wakazi wa jimbo hilo na vitongoji vyake 
uliofanyika katika Uwanja wa Parking.Katika
 mkutano huo, Dkt. Kigwangalla aliulizwa swali na mkazi wa jimbo hilo 
kama kweli ana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda, anayetokana na chama chake. 
“Mheshimiwa
 mbunge,naomba utu thibitishie kama una uwezo wa kumng’oa Spika wa Bunge
 (Makinda), kama ulivyotangaza dhamira ya kuwasilisha hoja binafsi 
bungeni ili bunge liweze kumng’oa.
 
“Kwa
 jinsit unavyofahamu utaratibu ndani ya CCM, huna ubavu wa kufanya hivyo
 , inaonesha ulikuwa ukijifurahisha tu,”alihoji mwananchi huyo.
 
Mwananchi
 huyo aliongeza kuwa, kwa kawaida CCM ina utaratibu wa kuzuia hatua 
mbalimbali zinazotaka kuchukuliwa na wanachama wake hivyo alimshauri 
Dkt.Kigwangalla, aacha ne na hoja hiyo kwani hana ubavu wa kumng’oa 
Bi.Makinda.
 
Akijibu
 swali hilo,Dkt. Kigwangalla alisema,si kweli kwamba CCM ina utaratibu 
wa kuondoa kinyemela hoja ambazo haikubaliani nazo ambapo suala la 
kutaka kumng’oa Bi. Makinda lipo ndani ya uwezo wake na kufafanua kuwa, 
hoja hiyo haijaondo lewa na hivi sasa ipo katika hatua za mwisho ili 
iweze kufikish wa bungeni.
 
“Kwa
 hili la kumng’oa Spika wa Bunge,niwaeleze wazi kuwa si kweli linawezaku
 nishinda... hoja imewasilishwa na Bi.Makin da atang’oka kama nikiamua 
kuendelea nayo kwa sababu tayari hoja nimeiwasilisha na nimekidhi 
mashart iyote.
 
“Hivi
 tunavyoongea, hoja yangu tayari imetoka hatua ya kwanz a na kukidhi 
vigezo vyote sasa inaenda hatua y a pili ambayo Kamati ya Bunge ya Haki,
 Maadili na Madaraka ya Bunge,itaamua ho ja yangu iingizwe bungeni au 
isiingizwe,”alisema . 
 
Aliongeza
 kuwa, baada ya hapo utafuata mcha kato wa mwisho ambao ni hoja hiyo 
kufikishwa bungeni na yeye kuiwasilisha rasmi mbele ya Bunge ili 
kufanyiwa uamuzi na wabunge wote kwa kupiga kura na kama atashinda au 
kushindwa,hilo ni jambo lingine.
 
Dkt.Kigwangalla
 alisema uamuzi wa kuondoka au kutoondoka kwa Spika, kutategemea uamuzi 
wa wabunge wenzake na kusisitiza kuwa , CCM haiwezi kuzuia hoja hiyo 
bila ya kupatiwa uamuzi na wabunge wote.
 
Akijibu
 swali ambalo lilihusiana na fedha za ushuru wa huduma zilizotolewa na 
Mgodi wa Dhahabu wa Resolute, ulioko wilayani humo, Dkt. Kigwangalla 
alisema fedha hizo sh. Bilioni 2.340,zililipwa na mgodi huo na sasa 
zimehifadhiwa katika ak aunti maalumu ili baadaye zitumike kama mtaji wa
 kuanzishia Ben ki ya Maendeleo ya Wananchi wa Nzega . 
 
“Fedha
 hizi tulizipigania kwa kiasi kikubwa hadi kuandam ana lakini 
tulifanikiwa kuzipata, niwathibitishie zipo sa lama katika akaunti 
maalumu tuliyoianzisha ili baadaye ziweze kuanzisha Benki yetu ya 
Maendeleo ambayo itaweza kutupa mikopo ya kuendesha shughuli zetu,”a 
lisema .
 
Alisema
 lengo lake ni kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri ili kuwasaidia 
wananchi wa Nzega kubadilisha maisha yao ambapo watu watahamasishwa 
kujiunga katika ushirikaau SACCOS ili waweze kupewa mikopo pia 
zitatumika kununulia mitambo ya kutengeneza barabara na uchimbaji visima
 vya maji. 
 
Gazeti
 moja linalotoka kila siku (si Majira), liliandika habari inayosema Dkt.
 Kigwangalla anadai Bi. Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha malipo 
ya sh. 430,000 kama posho kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, 
tofauti na wajumbe wa kamati nyingine ambao malipo yao ni sh. 180,000 
kwa siku. 
 
Hoja
 hiyo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Tabora 
Mjini, Bw. Ismail Aden Rage (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David 
Kafulila (NCCR-Mageuzi) ambao walidai hawaoni sababu ya kumuondoa Bi. 
Makinda madarakani. 
 
Bw.
 Kafulila alisema hilo ni suala la wana-CCM, kwani Bi. Makinda 
aking’olewa madarakani, mtu ambaye ataziba pengo lake  hawezi kutoka 
upinzani. Hoja hiyo ya Dkt. Kigwangalla iliibua mjadala kwa baadhi ya 
wabunge na wengine kukataa kusaini karatasi ambayo walipelekewa ili 
kuunga mkono. 
 
Mbunge
 wa Ludewa, mkoani Njombe, Bw. Deo Filikunjombe, alisema hoja ya Dkt. 
Kigwangalla imejengwa katika msingi hafifu isiyozingatia masilahi mapana
 ya nchi na mtazamo finyu

 
No comments:
Post a Comment